Jose Mourinho: Mtu mwenye akili zake anaielewa hali ya Manchester United

Jose Mourinho: Mtu mwenye akili zake anaielewa hali ya Manchester United

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
_100530253_gettyimages-933085886.jpg


Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema watu wenye "ubongo" na "fikira za kuelewa mambo ya msingi" wanafahamu na kuelewa kwamba klabu hiyo imo kwenye kipindi cha mpito.

Mourinho ameshutumiwa mara kwa mara kutokana na mtindo wake wa uchezaji ambao unadaiwa kutokuwa na ubunifu hata kidogo na pia kutoangazia uchezaji wa kushambulia.

Shutuma zilizidi baada ya United kuondolewa michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na klabu ya Sevilla ya Uhispania.
"Naelewa masikitiko ya kutupwa nje ya michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, lakini sielewi kitu kingine chochote kamwe," Mourinho alisema alipokuwa anahojiwa na CNN.

"Katika historia ya soka kote duniani, na si England pekee, kila wakati umekuwa na klabu kubwa zaidi zikipitia kipindi cha mpito, na unakuwa na klabu nyingine kubwa zaidi zikiwa na vipindi vinavyoendelea vya ushindi kwa muda mrefu, na hizi huwa ni kama awamu katika klabu yoyote ile."

United, wamo nafasi ya pili Ligi Kuu ya Uingereza nyuma ya Manchester City lakini pengo kati yao ni alama 16.

City huenda wakatawazwa washindi wa ligi kwenye debi ya Manchester itakayochezewa uwanja wa Etihad mnamo 7 Aprili.

Baada ya United kufuzu kwa nusu fainali Kombe la FA kwa mara ya 29 kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Brighton Jumamosi, Mourinho aliwashutumu wachezaji wake akisema "waliogopa kucheza" na pia akatilia shaka sifa zao kama wachezaji binafsi.

Mkesha wa mechi hiyo, Mourinho, ambaye ni meneja wa zamani wa Chelsea, alitoa hotuba ya dakika 12 kutetea kazi yake United.

Mourinho alikuwa ameshinda kombe ndogo la klabu bingwa Ulaya, Europa League na pia KOmbe la Ligi msimu wake wa kwanza akiwa United.

Katika mahojiano na CNN aliongeza: "Ukiangalia Ligi ya Premia tuko na timu moja, klabu moja ambayo imejiandaa vyema sana kutushinda kwa miaka kadha iliyopita, na tuna klabu 18 nyuma yetu. Klabu moja mbele yetu, na 18 nyuma yetu.

"Bila shaka, katika siku zijazo tungependa kuwa na klabu 19 nyuma yetu lakini huu ndio uhalisia, uhalisia kwa watu wenye ubongo, walio na uwezo wa kufikiria mambo ya kimsingi, walio na ufahamu kuhusu jinsi mchezo huu ulivyo, kwamba tuko katika kipindi cha mpito.

"Na kuwa katika kipindi cha mpito na bado kufanikiwa kutimiza kwa mfano yale tuliyoyatimiza msimu uliopita, kushinda vikombe, na kufanikiwa kutimiza yale tunayojaribu kuyatimiza msimu huu, ambayo ni kujaribu bado kushinda kombe na kujaribu kumaliza wa pili ... Nafikiri tuko katika nafasi nzuri."

Chanzo: BBC Swahili
 
Man city imejipanga kwa muda gani?
Jose yuko Man U kwa muda gani?

Gurdiola ana muda gani City?

Matokeo yao na position zao zikoje
 
Inamaana man u iko
Kwenye kipindi cha mpito kuliko
Ilichopitia Kwa Moyes na van gal????
 
Hakuna kocha aliyewahi kufanikiwa kwa kutokuw na maelewano mazur na wachezaji so mou haache chokochoko ili kuokoa kibarua chake
 
Mbona mou yuko vizuri tu ?
Mnataka silverware kila msimu ?
 
Asepe hana jipya kwakweli timu inaogopa kucheza aache ujinga
 
Yule kocha wa Barca cjui Enrique, Joachim Low, kocha wa Atl Madrid ht Tot au wa Juventus
tuchukulie huyo wa atltc na tott wanamafanikio gami kwa misimu miwili mfurulizo tangu wameingia ktk clab hizo wanazo fundisha? ukukingamisha na mou tangu ameshika club..
 
Man city imejipanga kwa muda gani?
Jose yuko Man U kwa muda gani?

Gurdiola ana muda gani City?

Matokeo yao na position zao zikoje
guardiola anakuja man city hawa watu wapo
1. Aguero
2. De bruyne
3. Fernandinho
4. company
5. silva
6. sterling
7. otamendi

sihitaji kuelezea mchango wa hao watu unaujua mwenyewe, position ambayo angalau mou alikuwa na advantage kwa pep labda ni golikipa de gea ni mzuri kuliko hart, ila kulikobakia kote Man city walikuwa vizuri zaidi.

ukiangalia majembe ya Man U sasa hivi wengi ni waliosajiliwa, Hatuna beki kama Baily, Hatuna Midfiled kushinda Matic na Pogba, Hatuna striker Kushinda Lukaku, wachezaji wapya wanahitaji muda kabla na wao hawajakuwa visiki.

kuna exception chache kama Valencia, Martial, lingard na Rashford wanafanya vizuri kiasi, ila huwezi wafananisha na hao wa juu wa city.
 
De brunyne aliuzwa na Mou
Wachezaji hao hao akipewa Gurdiola baada ya msimu atakuwa na vikombe vingi sana kwa kabati
Kwangu Mimi Jose zilipendwa
Alitakiwa kuwa Man u miaka 9 ilopita
 
guardiola anakuja man city hawa watu wapo
1. Aguero
2. De bruyne
3. Fernandinho
4. company
5. silva
6. sterling
7. otamendi
De brunyne aliuzwa na Mou
Wachezaji hao hao akipewa Gurdiola baada ya msimu atakuwa na vikombe vingi sana kwa kabati
Kwangu Mimi Jose zilipendwa
Alitakiwa kuwa Man u miaka 9 ilopita

Hapo juu ni swali na jibu.
 
Back
Top Bottom