Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Msanii maarufu wa muziki wa hip-hop, Joseph Haule, anayejulikana kama Profesa Jay, ametangaza rasmi kuwa atagombea tena ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Akizungumza kwenye kipindi cha The Throne kinachorushwa na redio Crown FM leo Ijumaa, Oktoba 11, 2024, Profesa Jay ameeleza kuwa bado anaamini anazo nguvu za kutosha za kuwatumikia wananchi wa Mikumi.
“Mwenyezi Mungu ameniweka hai, ninaamini ana kazi na mimi, naona bado nina nguvu, na ninaona kuna kazi ya kufanya kwa wananchi wa Mikumi," alisema Profesa Jay.
Ameongeza kuwa atashiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa hivi karibuni na kwamba mwakani atawania tena ubunge ili kuendelea kuwatumikia wananchi wa Mikumi.
Alisema kwa kujiamini, "Naamini siku ya kwenda Mikumi hata Twiga watatoka mbugani kuja kunilaki."
Jambo