Joseph Kabila atangazwa kuwa kiongozi wa kundi jipya la kijeshi na kisiasa DRC

Ndoto za Julius Nyerere, Che Guevara na mzee Laurent Kabila zatimia

Ben_Bella_a_la_Havane_-_Cuba.jpg

Ben Bella in Havana with Fidel Castro and Ernesto "Che" Guevara. Image via Wikimedia Commons

Che Guevara in the Congo​

BYDAVID SEDDON
Che Guevara's expedition in the Congo, though ill-fated, stands as a crucial example of anti-imperialist solidarity.

che-congo.jpg

Che Guevara in the Congo
Guevara then embarked on a tour of African states, visiting Algeria, then Mali, Congo-Brazzaville, Senegal, Ghana, Dahomey, Egypt, and finally Tanzania.

In Dar es Salaam, he met Laurent Kabila, who sought his help maintaining the liberated areas in the Congo’s east and southeast; in Cairo, he met Gaston Soumaliot, who wanted men and money for the Stanleyville front; and in Brazzaville, he met Agostinho Neto, who requested Cuban support for the Angolan liberation army, the People’s Movement for the Liberation of Angola (MPLA). Guevera was excited by these potentially effective liberation struggles and the role Cuba could play in them.

In February 1965, he flew to Beijing to see what help the Peoples’ Republic of China might provide for the Congolese rebellions. There he met Chou en Lai, who had taken his own tour of ten African countries between December 1963 and February 1964. Soon after meeting Che, Chou made a second visit to Algiers and Cairo, where he may have met the Congolese rebel leaders.

In June, he flew to Tanzania, where he certainly had an audience with both Kabila and Soumaliot.

On April 1, 1965, after a final meeting with Castro at the guerrilla base in Havana, Guevara flew with a small advance guard first to Moscow and then to Cairo, and on to Dar es Salaam.

The new Cuban ambassador, Pablo Rivalta, greeted Guevara and his soldiers at the airport outside Dar es Salaam.

12 October 2026
University of Dar es Salaam
Tanzania

PUBLIC LECTURE - UDSM

Dr. Abunuwasi L. Mwami -Julius Nyerere was a petty bourgeoisie [Bepari Uchwara]

View: https://m.youtube.com/watch?v=Sis0UIqlHos

TOKA MAKTABA :
Kinshasa

Laurent Kabila mzee wa kutoka Sumbawanga kama alivyokuwa anajulikana na majirani zake jijini Dar es Salaam

TOKA MAKTABA :

5 June 2025

Rare Interview of President Laurent Kabila of the Democratic Republic of Congo

View: https://m.youtube.com/watch?v=1s-C4FYIfQ4

Kuzaliwa Novemba 27, 1939, Kongo ya Ubelgiji baadaye Zaire (sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo)
Kifo Januari 18, 2001, Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Laurent-Désiré Kabila mwaka 1996, alipokuwa kiongozi wa Alliance des forces démocratiques pour la libération du Congo-Kinshasa (AFDL-CK).
1791889437378.png

Laurent-Désiré Kabila alikuwa mwanasiasa wa Kongo na kiongozi wa waasi aliyeishi uhamishoni nchini Tanzania kwa miongo kadhaa kuanzia miaka ya 1960s. Alikuwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuanzia 1997 hadi 2001.

Kabila alishiriki katika siasa kuanzia miaka ya 1960 na akaunda Chama cha Mapinduzi ya Watu (PRP) mwaka wa 1967. Kabila aliongoza maasi ya kutumia silaha dhidi ya mamlaka kuu mara kadhaa, ikiwa ni pamoja na mwishoni mwa miaka ya 1970.
1791889502134.png

Akiwa kiongozi wa kundi la upinzani la Alliance des forces démocratiques pour la libération du Congo-Kinshasa (AFDL-CK), Kabila aliongoza uasi mkubwa wa kijeshi uliokuwa katika sehemu za mashariki mwa nchi kuanzia kipindi cha vuli ya 1996. Katika majira ya kuchipua ya 1997, aliteka mji mkuu Kinshasa bila upinzani mkubwa na akawa rais mpya wa nchi hiyo, ambayo aliipa jina jipya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DR Congo.

Hata hivyo, uasi katika sehemu za mashariki ndani ya nchi ya DR Congo uliendelea, na Kabila hakuwahi kupata udhibiti kamili wa nchi hiyo.

Mgogoro huo hatimaye uligeuka kuwa vita vya kwanza vya bara bara Afrika ambapo mataifa ya Zimbabwe, Rwanda n.k yalipeleka majeshi, ambapo Kabila mwenyewe akawa mwathirika. Aliuawa katika ikulu ya rais ya jijini Kinshasa mnamo Januari 2001.

Joseph Kabila Kabange
Kuzaliwa Juni 4, 1971

standard_compressed_Joseph_Kabila_April_2016.jpg

Born 4 June 1971).President of the Democratic Republic of Congo, 2001–2019. Born at Hewa Bora II, the oldest son of Laurent Kabila was educated in Tanzania and at Beijing University. He returned to Congo with his father in 1997, becoming head of the military in 2000. Upon his father's murder, he assumed the presidency. Committed to bringing stability to his country, he negotiated a cease‐fire to end one of Africa's bloodiest civil wars in 2002. He was confirmed in elections in 2006 that were monitored by international observers, and regarded to be remarkably fair. Nevertheless, Kabila struggled to appease his major opponent, Jean‐Pierre Bemba, and to assert his government's authority in the eastern part of Congo

Joseph Kabila
Na Idara ya Mambo ya Nje ya Marekani .
Leseni: Imeangukia katika eneo wazi (Umiliki wa umma)
Joseph Kabila ni mwanasiasa wa Kongo ambaye alikuwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuanzia Januari 2001 hadi Januari 2019. Muhula wa pili wa Kabila, na kulingana na katiba, urais uliisha rasmi mnamo Desemba 31, 2016. Uchaguzi ulifanyika mwaka wa 2018, na kwa sasa Kabila, kama rais wa zamani, ni seneta wa maisha.

Joseph Kabila ni mtoto wa jenerali wa zamani wa waasi na rais Laurent-Désiré Kabila na Sifa Mahanya. Pamoja na dada yake pacha Jaynet, familia ikahamia uhamishoni Tanzania, kusoma elimu ya msingi sekondari na kutumikia JKT kwa mujibu wa sheria. Huko pia alipata mafunzo ya kijeshi, na kisha akawa mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda .

Joseph Kabila aliletwa kama kamanda wa jeshi la waasi la baba yake lilipoanzisha mashambulizi ya kijeshi dhidi ya dikteta wa Zaire Mobutu Sese Seko mnamo 1996. Laurent Kabila alipoteka mji mkuu Kinshasa , akamwondoa Mobutu madarakani na kubadilisha jina la nchi hiyo kuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph alitumwa China kwa mafunzo zaidi ya kijeshi. Kwa kuzingatia kukaa kwake nje ya nchi mara nyingi na Mfaransa dhaifu , mara nyingi amekuwa akikosolewa kwa kutokuwa " Mkongo halisi ".

Kazi ya kisiasa​

Joseph Kabila alirudi DR Congo mwaka wa 1998, na akateuliwa kuwa mkuu wa jeshi la nchi hiyo. Mnamo Januari 16, 2001, Laurent Kabila aliuawa, na mnamo Januari 26 mwanawe aliapishwa kuwa rais. Mnamo 2006, alishinda uchaguzi wa rais dhidi ya mgombea wa upinzani Jean-Pierre Bemba , kisha mnamo 2011 dhidi ya Étienne Tshisekedi .

Uchaguzi mpya wa rais ulipangwa kufanyika mwaka wa 2016, na Joseph Kabila, ambaye amehudumu rasmi kwa mihula miwili, alizuiwa kikatiba kugombea tena uchaguzi. Wakati huo huo, hakuhitaji kugombea kwa mara tatu kabla ya rais mpya aliyechaguliwa, jambo lililomfanya Joseph Kabila aahirishe uchaguzi. Kwa hivyo, Kabila alishutumiwa kwa kuiba uchaguzi ili kutumia mwanya huu katika sheria, ambao ulisababisha maandamano na ghasia katika sehemu kadhaa za nchi mnamo 2017. Sababu rasmi ya kuahirisha uchaguzi ilikuwa ukosefu wa pesa na usajili wa wapiga kura katika sehemu zilizoathiriwa na migogoro nchini.

Vipaumbele vya kisiasa​

Akiwa mkuu wa jeshi, Kabila alikuwa kitovu cha Vita vya Pili vya Kongo (1998–2003), ambavyo vilihusisha nchi kadhaa jirani. Hata hivyo, machafuko na milipuko midogo ya vita imeendelea kuikumba mashariki mwa Kongo, na mwaka wa 2016 machafuko pia yalizuka katika jimbo la kati la Kasai .

Katika taaluma yake ya kisiasa, Kabila ametetea hasa "barabara ya kuelekea usasa" kwa kuzingatia miundombinu , uundaji wa ajira, elimu, na afya. Wakati wa muhula wake kama mkuu wa nchi, hii pia ilisababisha ubinafsishaji wa makampuni kadhaa ya zamani ya kitaifa na sekta ya elimu kutokana na ukosefu wa uwekezaji wa umma. Pia alitambuliwa kwa kuzuia vita vingine vikubwa kuzuka wakati wa utawala wake.

Kabila na familia yake ya karibu wamepata kiasi kikubwa cha pesa kupitia makampuni mbalimbali binafsi, ambayo mara nyingi yanapatikana nje ya nchi katika kilimo, madini, mawasiliano ya simu, usafiri wa anga na usimamizi wa mali.

Joseph Kabila ana mke kwa jina Marie Olive Lembe di Sita. Wanandoa hao wana watoto wawili: Sifa na Laurent-Désiré
 
View attachment 3689799
Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Joseph Kabila, ametangazwa kuwa kiongozi wa kundi jipya la kijeshi na kisiasa linaloitwa Front pour la Refondation de la Nation (FRN), hatua inayoweza kubadili mwelekeo wa mgogoro wa kisiasa na kiusalama unaoendelea mashariki mwa nchi hiyo.

Kundi hilo lilitangazwa Oktoba 12, 2026, katika mji wa Goma, jimbo la Kivu Kaskazini, eneo ambalo limekuwa chini ya udhibiti wa waasi wa M23 tangu Januari 2025.

FRN imeundwa kama muungano wa kisiasa na kijeshi unaojumuisha viongozi wa makundi yaliyokuwa yakishirikiana ndani ya muungano wa Alliance Fleuve Congo (AFC) na waasi wa M23. Tangazo hilo linaashiria hatua mpya katika uhusiano kati ya Kabila na makundi yanayopambana na Serikali ya Rais Félix Tshisekedi.

Soma pia: Joseph Kabila na hoja 10 dhidi ya utawala wa sasa wa DRC chini ya Tshisekedi

Kabila kuongoza muungano mpya

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa wakati wa kutangaza kuundwa kwa FRN, Kabila ameteuliwa kuongoza muungano huo, huku viongozi wengine wenye ushawishi katika AFC/M23 wakipewa nafasi za uongozi.

Miongoni mwao ni Corneille Nangaa, aliyekuwa kiongozi wa AFC na mkuu wa zamani wa Tume Huru ya Uchaguzi ya DRC, pamoja na Bertrand Bisimwa, kiongozi wa kisiasa wa M23, na Sultani Makenga, mmoja wa makamanda wakuu wa kijeshi wa kundi hilo.

Nangaa na Bisimwa wametajwa kuwa miongoni mwa makamu wa rais wa muungano huo, huku Makenga akitajwa kuwa mkuu wa majeshi ya kundi jipya. Claude Ibalanky, mshauri wa muungano huo, ndiye aliyewasilisha taarifa kuhusu kuundwa kwake katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Goma.

Taarifa zilizotolewa na viongozi wa FRN zinaeleza kuwa muundo huo mpya unalenga kuunganisha nguvu, rasilimali na uwezo wa makundi yanayoshiriki katika muungano huo ili kutekeleza malengo yao ya kisiasa na kijeshi.

Wapinga utawala wa Tshisekedi

Katika maelezo yake kuhusu madhumuni ya kuanzishwa kwa FRN, Ibalanky alisema muungano huo unalenga kuunganisha na kuratibu nguvu za upinzani dhidi ya Serikali ya Kinshasa, ambayo wanaituhumu kwa utawala wanaoueleza kuwa wa kimabavu.

Viongozi hao wamesema wanataka kurejesha misingi ya Jamhuri inayofanya kazi kwa ufanisi na kuleta mwelekeo mpya wa kisiasa nchini humo. Hata hivyo, kauli zao zimeibua wasiwasi kutokana na kutaja wazi uwezekano wa kutumia nguvu katika kutekeleza malengo yao.

Kauli hiyo inaweka wazi msimamo wa muungano huo dhidi ya Serikali ya Tshisekedi, huku ikiibua maswali kuhusu athari zake kwa juhudi za kutafuta suluhu ya amani katika eneo la mashariki mwa DRC.

View attachment 3689800a​

Historia ya mvutano kati ya Kabila na Tshisekedi​

Kabila aliongoza DRC kuanzia mwaka 2001 hadi 2019, kabla ya kukabidhi madaraka kwa Tshisekedi baada ya uchaguzi wa mwaka 2018 uliokuwa na malalamiko na utata kuhusu matokeo yake.

Katika miezi ya hivi karibuni, Serikali ya Kinshasa imekuwa ikimtuhumu Kabila kuunga mkono waasi wa AFC/M23, madai ambayo amekuwa akiyakanusha. Hata hivyo, kuonekana kwake Goma na kutangazwa kwake kuwa kiongozi wa FRN kunaongeza uzito wa nafasi yake katika mabadiliko ya kisiasa na kijeshi yanayoendelea mashariki mwa nchi hiyo.

Katika hotuba yake iliyotolewa siku chache kabla ya tangazo la FRN, Kabila aliikosoa Serikali ya Tshisekedi kwa kile alichokitaja kuwa rushwa, utawala usioridhisha na kushindwa kudhibiti hali ya usalama mashariki mwa DRC. Pia alikosoa makubaliano ya Serikali kuhusu rasilimali za madini na Marekani.

Kwa upande mwingine, Kabila amekabiliwa na changamoto za kisheria nchini humo. Mahakama ya kijeshi ilimhukumu kifo akiwa hayupo mahakamani baada ya kupatikana na hatia katika kesi iliyohusisha uhaini, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu. Kabila amepinga mashtaka hayo, akidai kuwa yana misingi ya kisiasa.

Athari kwa usalama na mazungumzo ya amani​

Kuundwa kwa FRN kunatokea wakati juhudi za kidiplomasia za kumaliza mapigano mashariki mwa DRC zikiendelea, huku mapigano kati ya vikosi vya Serikali na waasi yakiendelea kuathiri usalama wa wananchi.

Umoja wa Mataifa na mataifa kadhaa ya Magharibi yamekuwa yakiishutumu Rwanda kwa kuunga mkono M23, madai ambayo Serikali ya Rwanda imeyakanusha. Mgogoro huo umeongeza mvutano wa kikanda na kuifanya hali ya usalama mashariki mwa DRC kuwa suala linalohitaji ushirikiano wa nchi jirani na wadau wa kimataifa.

Kuingia kwa Kabila katika nafasi ya uongozi wa muungano unaojumuisha viongozi wa AFC/M23 kunaibua maswali kuhusu mustakabali wa mazungumzo ya amani, muundo wa uongozi wa waasi na uwezekano wa kuongezeka kwa mapigano.

Hata hivyo, tangazo la kuundwa kwa FRN pekee halithibitishi kuwa kundi hilo limeanzisha operesheni mpya ya kijeshi. Hatua zitakazofuata, msimamo wa Serikali ya Kinshasa na mwitikio wa wadau wa kikanda vitakuwa muhimu katika kubainisha mwelekeo wa mgogoro huo.

Kwa sasa, kuanzishwa kwa FRN na uteuzi wa Kabila kuwa kiongozi wake ni mabadiliko muhimu katika siasa za DRC, yakimweka rais huyo wa zamani katika nafasi ya moja kwa moja zaidi ndani ya muungano unaopinga Serikali iliyopo madarakani.
Kabila hakutosheka na madaraka baada ya kutawala kwa miaka takribani 20.

Ameamua kuungana na Rwanda(M23) mahasimu wake wa zamani Ili kumpinga Tshekedi.

Haya ni matokeo ya kumpora Martin Fayulu Urais wake.

zitto junior JokaKuu Tresor Mandala
 
Sijaelewa uliyoyaandika, ngoja nikatafute habari hii kwenye vyombo vya nje.
 
Maisha haya Bwana, Sisi tuna miaka 40 hadi 50 tumeshakata tamaa ya maisha tumewaachie wengine ila jamaa around 60 bado anapambana na anaona future bado ipo Sana tu
 
Kabila hakutosheka na madaraka baada ya kutawala kwa miaka takribani 20.

Ameamua kuungana na Rwanda(M23) mahasimu wake wa zamani Ili kumpinga Tshekedi.

Haya ni matokeo ya kumpora Martin Fayulu Urais wake.

zitto junior JokaKuu Tresor Mandala
Bro kajificha ficha ,mwishooni kaamua kujitokeza rasmi, leo hii m23 wamekua maswahiba wake
 
Yeye amekua raisi miaka 18, kasahau nini huyo jamaa?
Wakongomani hawawezi kuja kupata maendeleo na amani nchini kwao, sababu ni ndogo tuu, kama ilivyo kwa majirani wao Tanganyika. Akili za viongozi ni ndogo sana. 😊
 
Hapo kufanya mkataba na marekani ndio chanzo hicho maana ulaji umeingiliwa huyo ndie mfadhili wa vikundi hivyo ili aendelee kupiga madini waafrika hawana cha kupoteza ikifika kwenye swala la kutetea ugali
 
Back
Top Bottom