Joseph Kabila atangazwa kuwa kiongozi wa kundi jipya la kijeshi na kisiasa DRC

sijui ni kwa nini binadamu wengine kama huyu wa kwetu pia huwa wana-feel sooo entitled, i mean, kabila alikuwa raisi wa kongo dr kwa miaka 18, ni nini amesahau huko? ni kipi ambacho atakifanya kipya wakati alikuwa na hiyo nafasi kwa miaka 18? wakati mwingine i am for assassinations kwa takataka aina hii, USA na west wako sawa kabisa wanavyo-assassinate akina ayatola, sadamu huseni, gadafi na watoto wake, arresting of maduro na hata huku kwetu afrika ingependeza kama wangefanya assassinations za hawa watu ...
 
Ila Africa we have a long way to go aisee, Hemu imagine someone who has been in power for over 15 years then Ghafla after his retirement he turns to be a rebel leader Mtu ambae alipaswa kuwa statesman anaenda Kuwa rebel leader can you imagine?

Sasa during his regime atakuambia kuwa vipi alikuwa sio sehemu ya sabotage ili nchi isitulie? Kwasababu Congo imekuwa ovyo Sana na Marais wote wanaokaa Juu wanasahau kabisa nini kimewapeleka Kwenye Power, Congo is a failed state

No wonder they sentenced him to death in absentia
Wewe unadhani huko ulaya kabla ya vita vya pili vya dunia hali ilikuaje?

Hiyo nchi ya kongo ni kubwa sana tatizo linaanzia hapo!

Mwenye backup ya wananchi ndiye atakayeshinda hiyo vita. Kibaya zaidi Tshishekedi aliuza mgodi kwa mmarekani wananchi hawawezi kuwa upande wake.

Tegemea vita kamili hapo
 
Taifa la DR Congo na historia ya balkanization duniani, vichecheo vya taifa kuvunjika vipande vipande:

Balkanization (au Balkan ) nimchakato wa kugawanya eneo, nchi, au mfumo mkubwa katika sehemu ndogo, ambazo kwa kawaida ni uadui au zisizo na ushirikiano.

Asili na Historia ya balkanization
  • Jina: Neno hili linatokana na Rasi ya Balkan Kusini-mashariki mwa Ulaya. "Balkan" linatokana na neno la Kituruki la Ottoman lenye maana ya safu ya milima yenye miti.
  • Mizizi ya Kihistoria: Neno hilo lilipata umaarufu mwanzoni mwa karne ya 20 kufuatia kuporomoka kwa Milki ya Ottoman, Vita vya Balkan (1912-1913), na Vita vya Kwanza vya Dunia, wakati eneo hilo lilipogawanyika katika makundi ya majimbo yanayoshindana.
  • Mifano ya Kawaida: Kuvunjika kwa Milki ya Ottoman, mabadiliko ya mpaka baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia, na kuvunjika kwa Yugoslavia kwa vurugu katika miaka ya 1990.

Sababu na Vichocheo
  • Mgawanyiko wa Kikabila na Kitamaduni: Tofauti kubwa katika lugha, mila, au urithi.
  • Migogoro ya Kidini: Mivutano inayotokana na imani inayozuia umoja wa utambulisho wa kitaifa.
  • Utaifa na Kujitenga: Vikundi vya wenyeji vinavyodai kujitawala au uhuru kutoka kwa mamlaka kuu.
  • Kuanguka kwa Nguvu Kuu: Kudhoofika au kuanguka ghafla kwa himaya kuu, serikali, au muungano wa kisiasa.

Matumizi na Viendelezi vya Kisasa
Ingawa awali ilikuwa neno la kijiografia na kisiasa, balkanisation sasa inatumika kuelezea mgawanyiko wa mifumo isiyo ya kimwili:
  • Vyombo vya Habari na Intaneti: Kugawanyika kwa hadhira katika vyumba vya mwangwi vilivyotengwa au majukwaa tofauti ya mtandaoni.
  • Siasa: Mgawanyiko mkubwa wa vyama ambapo pande zinazopingana za kisiasa zinakataa kuafikiana.
  • Teknolojia na Miundombinu: Viwango visivyoendana, mifumo iliyogawanywa (kama vile udhibiti wa trafiki ya anga au sarafu tofauti za kitaifa).
 
Litakalo ibuka hapo itakua bonge Moja la tatizo, ukabila utaibuka sana
 
Kama umesoma kitabu cha machiaveli the prince

Kabila anatumia wanajeshi wa kukodi, hiyo vita atashinda kwa muda ila ataishi kwa mateso sababu hao M23 watataka kuvuna kwa wingi kile walichokipigania kwa miaka mingi jambo ambalo hataliweza sababu litawafanya wakongo waishi maisja magumu kuliko sasa na kuchochea uasi mwingine
 
Basi atakua hajajifunza kwa Baba yake, alipokubali kuwatumia kadogoo kutoka Rwanda kumpeleka Kinshasa,
 
View attachment 3689799
Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Joseph Kabila, ametangazwa kuwa kiongozi wa kundi jipya la kijeshi na kisiasa linaloitwa Front pour la Refondation de la Nation (FRN), hatua inayoweza kubadili mwelekeo wa mgogoro wa kisiasa na kiusalama unaoendelea mashariki mwa nchi hiyo.

Kundi hilo lilitangazwa Oktoba 12, 2026, katika mji wa Goma, jimbo la Kivu Kaskazini, eneo ambalo limekuwa chini ya udhibiti wa waasi wa M23 tangu Januari 2025.

FRN imeundwa kama muungano wa kisiasa na kijeshi unaojumuisha viongozi wa makundi yaliyokuwa yakishirikiana ndani ya muungano wa Alliance Fleuve Congo (AFC) na waasi wa M23. Tangazo hilo linaashiria hatua mpya katika uhusiano kati ya Kabila na makundi yanayopambana na Serikali ya Rais Félix Tshisekedi.

Soma pia: Joseph Kabila na hoja 10 dhidi ya utawala wa sasa wa DRC chini ya Tshisekedi

Kabila kuongoza muungano mpya

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa wakati wa kutangaza kuundwa kwa FRN, Kabila ameteuliwa kuongoza muungano huo, huku viongozi wengine wenye ushawishi katika AFC/M23 wakipewa nafasi za uongozi.

Miongoni mwao ni Corneille Nangaa, aliyekuwa kiongozi wa AFC na mkuu wa zamani wa Tume Huru ya Uchaguzi ya DRC, pamoja na Bertrand Bisimwa, kiongozi wa kisiasa wa M23, na Sultani Makenga, mmoja wa makamanda wakuu wa kijeshi wa kundi hilo.

Nangaa na Bisimwa wametajwa kuwa miongoni mwa makamu wa rais wa muungano huo, huku Makenga akitajwa kuwa mkuu wa majeshi ya kundi jipya. Claude Ibalanky, mshauri wa muungano huo, ndiye aliyewasilisha taarifa kuhusu kuundwa kwake katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Goma.

Taarifa zilizotolewa na viongozi wa FRN zinaeleza kuwa muundo huo mpya unalenga kuunganisha nguvu, rasilimali na uwezo wa makundi yanayoshiriki katika muungano huo ili kutekeleza malengo yao ya kisiasa na kijeshi.

Wapinga utawala wa Tshisekedi

Katika maelezo yake kuhusu madhumuni ya kuanzishwa kwa FRN, Ibalanky alisema muungano huo unalenga kuunganisha na kuratibu nguvu za upinzani dhidi ya Serikali ya Kinshasa, ambayo wanaituhumu kwa utawala wanaoueleza kuwa wa kimabavu.

Viongozi hao wamesema wanataka kurejesha misingi ya Jamhuri inayofanya kazi kwa ufanisi na kuleta mwelekeo mpya wa kisiasa nchini humo. Hata hivyo, kauli zao zimeibua wasiwasi kutokana na kutaja wazi uwezekano wa kutumia nguvu katika kutekeleza malengo yao.

Kauli hiyo inaweka wazi msimamo wa muungano huo dhidi ya Serikali ya Tshisekedi, huku ikiibua maswali kuhusu athari zake kwa juhudi za kutafuta suluhu ya amani katika eneo la mashariki mwa DRC.

View attachment 3689800a​

Historia ya mvutano kati ya Kabila na Tshisekedi​

Kabila aliongoza DRC kuanzia mwaka 2001 hadi 2019, kabla ya kukabidhi madaraka kwa Tshisekedi baada ya uchaguzi wa mwaka 2018 uliokuwa na malalamiko na utata kuhusu matokeo yake.

Katika miezi ya hivi karibuni, Serikali ya Kinshasa imekuwa ikimtuhumu Kabila kuunga mkono waasi wa AFC/M23, madai ambayo amekuwa akiyakanusha. Hata hivyo, kuonekana kwake Goma na kutangazwa kwake kuwa kiongozi wa FRN kunaongeza uzito wa nafasi yake katika mabadiliko ya kisiasa na kijeshi yanayoendelea mashariki mwa nchi hiyo.

Katika hotuba yake iliyotolewa siku chache kabla ya tangazo la FRN, Kabila aliikosoa Serikali ya Tshisekedi kwa kile alichokitaja kuwa rushwa, utawala usioridhisha na kushindwa kudhibiti hali ya usalama mashariki mwa DRC. Pia alikosoa makubaliano ya Serikali kuhusu rasilimali za madini na Marekani.

Kwa upande mwingine, Kabila amekabiliwa na changamoto za kisheria nchini humo. Mahakama ya kijeshi ilimhukumu kifo akiwa hayupo mahakamani baada ya kupatikana na hatia katika kesi iliyohusisha uhaini, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu. Kabila amepinga mashtaka hayo, akidai kuwa yana misingi ya kisiasa.

Athari kwa usalama na mazungumzo ya amani​

Kuundwa kwa FRN kunatokea wakati juhudi za kidiplomasia za kumaliza mapigano mashariki mwa DRC zikiendelea, huku mapigano kati ya vikosi vya Serikali na waasi yakiendelea kuathiri usalama wa wananchi.

Umoja wa Mataifa na mataifa kadhaa ya Magharibi yamekuwa yakiishutumu Rwanda kwa kuunga mkono M23, madai ambayo Serikali ya Rwanda imeyakanusha. Mgogoro huo umeongeza mvutano wa kikanda na kuifanya hali ya usalama mashariki mwa DRC kuwa suala linalohitaji ushirikiano wa nchi jirani na wadau wa kimataifa.

Kuingia kwa Kabila katika nafasi ya uongozi wa muungano unaojumuisha viongozi wa AFC/M23 kunaibua maswali kuhusu mustakabali wa mazungumzo ya amani, muundo wa uongozi wa waasi na uwezekano wa kuongezeka kwa mapigano.

Hata hivyo, tangazo la kuundwa kwa FRN pekee halithibitishi kuwa kundi hilo limeanzisha operesheni mpya ya kijeshi. Hatua zitakazofuata, msimamo wa Serikali ya Kinshasa na mwitikio wa wadau wa kikanda vitakuwa muhimu katika kubainisha mwelekeo wa mgogoro huo.

Kwa sasa, kuanzishwa kwa FRN na uteuzi wa Kabila kuwa kiongozi wake ni mabadiliko muhimu katika siasa za DRC, yakimweka rais huyo wa zamani katika nafasi ya moja kwa moja zaidi ndani ya muungano unaopinga Serikali iliyopo madarakani.
Ameshiba, akae pembeni na wengine washibe
 
Taifa la DR Congo na historia ya balkanization duniani, vichecheo vya taifa kuvunjika vipande vipande:

Balkanization (au Balkan ) nimchakato wa kugawanya eneo, nchi, au mfumo mkubwa katika sehemu ndogo, ambazo kwa kawaida ni uadui au zisizo na ushirikiano.

Asili na Historia ya balkanization
  • Jina: Neno hili linatokana na Rasi ya Balkan Kusini-mashariki mwa Ulaya. "Balkan" linatokana na neno la Kituruki la Ottoman lenye maana ya safu ya milima yenye miti.
  • Mizizi ya Kihistoria: Neno hilo lilipata umaarufu mwanzoni mwa karne ya 20 kufuatia kuporomoka kwa Milki ya Ottoman, Vita vya Balkan (1912-1913), na Vita vya Kwanza vya Dunia, wakati eneo hilo lilipogawanyika katika makundi ya majimbo yanayoshindana.
  • Mifano ya Kawaida: Kuvunjika kwa Milki ya Ottoman, mabadiliko ya mpaka baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia, na kuvunjika kwa Yugoslavia kwa vurugu katika miaka ya 1990.

Sababu na Vichocheo
  • Mgawanyiko wa Kikabila na Kitamaduni: Tofauti kubwa katika lugha, mila, au urithi.
  • Migogoro ya Kidini: Mivutano inayotokana na imani inayozuia umoja wa utambulisho wa kitaifa.
  • Utaifa na Kujitenga: Vikundi vya wenyeji vinavyodai kujitawala au uhuru kutoka kwa mamlaka kuu.
  • Kuanguka kwa Nguvu Kuu: Kudhoofika au kuanguka ghafla kwa himaya kuu, serikali, au muungano wa kisiasa.

Matumizi na Viendelezi vya Kisasa
Ingawa awali ilikuwa neno la kijiografia na kisiasa, balkanisation sasa inatumika kuelezea mgawanyiko wa mifumo isiyo ya kimwili:
  • Vyombo vya Habari na Intaneti: Kugawanyika kwa hadhira katika vyumba vya mwangwi vilivyotengwa au majukwaa tofauti ya mtandaoni.
  • Siasa: Mgawanyiko mkubwa wa vyama ambapo pande zinazopingana za kisiasa zinakataa kuafikiana.
  • Teknolojia na Miundombinu: Viwango visivyoendana, mifumo iliyogawanywa (kama vile udhibiti wa trafiki ya anga au sarafu tofauti za kitaifa).

12 October 2026

Eric Mboma - Matatizo ya DRC ni Zaidi ya Uchimbaji Madini

Mvemba Phezo Dizolele ktk mazungumzo exclusive anazungumza na Eric Mboma,

View: https://m.youtube.com/watch?v=8IRFdXTrTtk

Mvemba Phezo Dizolele speaks with Eric Mboma, a Congolese citizen, a prominent businessman

Mazungumzo hayo yanachunguza vikwazo vinavyokabili uchumi wa Kongo, ikiwa ni pamoja na mapengo ya miundombinu, upatikanaji mdogo wa mitaji, taasisi dhaifu, na sekta kubwa isiyo rasmi. Dizolele na Mboma pia wanachunguza ushindani unaokua wa kimataifa kuhusu hitaji la madini ya shaba, kobalti, na rasilimali zingine za kimkakati za Kongo

Eric Mboma anasema kwamba mustakabali wa DRC hautategemea tu kuvutia uwekezaji, bali pia kuimarisha taasisi, kupanua upatikanaji wa mtaji, kupata mikakati ya kivitendo kuweza kuongeza thamani zaidi ya maliasili zinazochimbwa ndani ya nchi, na kugeuza mawazo na maandiko kabambe kuwa utekelezaji mzuri kivitendo.

Source : Advisory Dizolele
 
View attachment 3689799
Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Joseph Kabila, ametangazwa kuwa kiongozi wa kundi jipya la kijeshi na kisiasa linaloitwa Front pour la Refondation de la Nation (FRN), hatua inayoweza kubadili mwelekeo wa mgogoro wa kisiasa na kiusalama unaoendelea mashariki mwa nchi hiyo.

Kundi hilo lilitangazwa Oktoba 12, 2026, katika mji wa Goma, jimbo la Kivu Kaskazini, eneo ambalo limekuwa chini ya udhibiti wa waasi wa M23 tangu Januari 2025.

FRN imeundwa kama muungano wa kisiasa na kijeshi unaojumuisha viongozi wa makundi yaliyokuwa yakishirikiana ndani ya muungano wa Alliance Fleuve Congo (AFC) na waasi wa M23. Tangazo hilo linaashiria hatua mpya katika uhusiano kati ya Kabila na makundi yanayopambana na Serikali ya Rais Félix Tshisekedi.

Soma pia: Joseph Kabila na hoja 10 dhidi ya utawala wa sasa wa DRC chini ya Tshisekedi

Kabila kuongoza muungano mpya

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa wakati wa kutangaza kuundwa kwa FRN, Kabila ameteuliwa kuongoza muungano huo, huku viongozi wengine wenye ushawishi katika AFC/M23 wakipewa nafasi za uongozi.

Miongoni mwao ni Corneille Nangaa, aliyekuwa kiongozi wa AFC na mkuu wa zamani wa Tume Huru ya Uchaguzi ya DRC, pamoja na Bertrand Bisimwa, kiongozi wa kisiasa wa M23, na Sultani Makenga, mmoja wa makamanda wakuu wa kijeshi wa kundi hilo.

Nangaa na Bisimwa wametajwa kuwa miongoni mwa makamu wa rais wa muungano huo, huku Makenga akitajwa kuwa mkuu wa majeshi ya kundi jipya. Claude Ibalanky, mshauri wa muungano huo, ndiye aliyewasilisha taarifa kuhusu kuundwa kwake katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Goma.

Taarifa zilizotolewa na viongozi wa FRN zinaeleza kuwa muundo huo mpya unalenga kuunganisha nguvu, rasilimali na uwezo wa makundi yanayoshiriki katika muungano huo ili kutekeleza malengo yao ya kisiasa na kijeshi.

Wapinga utawala wa Tshisekedi

Katika maelezo yake kuhusu madhumuni ya kuanzishwa kwa FRN, Ibalanky alisema muungano huo unalenga kuunganisha na kuratibu nguvu za upinzani dhidi ya Serikali ya Kinshasa, ambayo wanaituhumu kwa utawala wanaoueleza kuwa wa kimabavu.

Viongozi hao wamesema wanataka kurejesha misingi ya Jamhuri inayofanya kazi kwa ufanisi na kuleta mwelekeo mpya wa kisiasa nchini humo. Hata hivyo, kauli zao zimeibua wasiwasi kutokana na kutaja wazi uwezekano wa kutumia nguvu katika kutekeleza malengo yao.

Kauli hiyo inaweka wazi msimamo wa muungano huo dhidi ya Serikali ya Tshisekedi, huku ikiibua maswali kuhusu athari zake kwa juhudi za kutafuta suluhu ya amani katika eneo la mashariki mwa DRC.

View attachment 3689800a​

Historia ya mvutano kati ya Kabila na Tshisekedi​

Kabila aliongoza DRC kuanzia mwaka 2001 hadi 2019, kabla ya kukabidhi madaraka kwa Tshisekedi baada ya uchaguzi wa mwaka 2018 uliokuwa na malalamiko na utata kuhusu matokeo yake.

Katika miezi ya hivi karibuni, Serikali ya Kinshasa imekuwa ikimtuhumu Kabila kuunga mkono waasi wa AFC/M23, madai ambayo amekuwa akiyakanusha. Hata hivyo, kuonekana kwake Goma na kutangazwa kwake kuwa kiongozi wa FRN kunaongeza uzito wa nafasi yake katika mabadiliko ya kisiasa na kijeshi yanayoendelea mashariki mwa nchi hiyo.

Katika hotuba yake iliyotolewa siku chache kabla ya tangazo la FRN, Kabila aliikosoa Serikali ya Tshisekedi kwa kile alichokitaja kuwa rushwa, utawala usioridhisha na kushindwa kudhibiti hali ya usalama mashariki mwa DRC. Pia alikosoa makubaliano ya Serikali kuhusu rasilimali za madini na Marekani.

Kwa upande mwingine, Kabila amekabiliwa na changamoto za kisheria nchini humo. Mahakama ya kijeshi ilimhukumu kifo akiwa hayupo mahakamani baada ya kupatikana na hatia katika kesi iliyohusisha uhaini, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu. Kabila amepinga mashtaka hayo, akidai kuwa yana misingi ya kisiasa.

Athari kwa usalama na mazungumzo ya amani​

Kuundwa kwa FRN kunatokea wakati juhudi za kidiplomasia za kumaliza mapigano mashariki mwa DRC zikiendelea, huku mapigano kati ya vikosi vya Serikali na waasi yakiendelea kuathiri usalama wa wananchi.

Umoja wa Mataifa na mataifa kadhaa ya Magharibi yamekuwa yakiishutumu Rwanda kwa kuunga mkono M23, madai ambayo Serikali ya Rwanda imeyakanusha. Mgogoro huo umeongeza mvutano wa kikanda na kuifanya hali ya usalama mashariki mwa DRC kuwa suala linalohitaji ushirikiano wa nchi jirani na wadau wa kimataifa.

Kuingia kwa Kabila katika nafasi ya uongozi wa muungano unaojumuisha viongozi wa AFC/M23 kunaibua maswali kuhusu mustakabali wa mazungumzo ya amani, muundo wa uongozi wa waasi na uwezekano wa kuongezeka kwa mapigano.

Hata hivyo, tangazo la kuundwa kwa FRN pekee halithibitishi kuwa kundi hilo limeanzisha operesheni mpya ya kijeshi. Hatua zitakazofuata, msimamo wa Serikali ya Kinshasa na mwitikio wa wadau wa kikanda vitakuwa muhimu katika kubainisha mwelekeo wa mgogoro huo.

Kwa sasa, kuanzishwa kwa FRN na uteuzi wa Kabila kuwa kiongozi
TPDF mlioko DRC fanyeni mazoezi ya kutosha.
Unawaongelea wale SAMIDRC waliotimuliwa na M23 huko Goma?
Bro kajificha ficha ,mwishooni kaamua kujitokeza rasmi, leo hii m23 wamekua maswahiba wake
Hivi Kabila akija Tz atakamatwa na kukabidhiwa kwa Serikali ya Drc kama Mhalifu?..

JokaKuu zitto junior
 
Back
Top Bottom