GE2025 Joseph Mbilinyi (Sugu) afunguka mabadiliko wanayoyahitaji, awapongeza pia Askofu Gwajima na Polepole

GE2025 Joseph Mbilinyi (Sugu) afunguka mabadiliko wanayoyahitaji, awapongeza pia Askofu Gwajima na Polepole

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,775
Reaction score
2,891
Wakuu tusubiri madini kutokea Kanda ya Nyasa hapo saa 7


View: https://www.youtube.com/watch?v=uKYw8JinUVc

===

Sugu anabainisha kuwa hadi hakuna hatua zozote zilizochukuliwa licha ya watu kupotea akiwemo Deus Soka na wenzake. Aidha ameeleza kuwa dola imeendelea kuonesha ubabe kwa kufanya mambo mbalimbali ikiwemo kufungia makanisa na kuwanyima raia haki yao ya kuabudu.

Sugu anaeleza kuwa uhuru wa watu kutoa maoni yao unabanwa ambapo kwa sasa watu wanabanwa iwapo watatoa maoni tofauti.

"Kuna kitu sasa kinaitwa Doria mitandaoni, polisi eti wanapita mitandaoni kuwatafuta wakosoaji wa serikali" - Sugu

Sugu amesisitiza kuwa kuzunguzma yale yanayoendelea ni jukumu letu sote si jukumu la wanasiasa wala wanachadema peke yake.

"Nchi hii ikiharibika hasara ni kwa Watanzania wote na vizazi vyetu, sasa tusikubali vizazi vya huko mbele vije kushangaa hii nchi ilikuwa na watu wa aina gani" - Sugu

Aidha Sugu amesema anatumbua kazi kubwa ya Bishop Gwajima na Humphrey Polepole kwa kufanya kazi njema sana hivi karibuni.

"Hata kama kuna records za kauli na matendo yao huko nyuma ambayo hatukabiliani nayo. Hatukubaliani na walivyoshiriki kupora chaguzi za huko nyuma, lakini wametoka wametubu wanazungumza kwa niaba ya nchi" - Sugu

Sugu amezijataja reforms wanazozitaka ni kuwa;

Matokeo ya Urais yaweze kupingwa mahakamani.
Rais asitue mkurugenzi wala watendaji wengine wa tume ya uchaguzi
Mawakala wasiapishwe na wakurugenzi na badala yake waapishwe na vyama vyao
Mawakala waruhusiwe kuingia na simu vituoni ili wawe na uwezo wa kuwasiliana na wagombea wanaowawakilisha
Mawakala wapewe fomu za matokeo halali kwenye vituo vyao
Sugu ameshauri tume huru ya Taifa ya uchaguzi isitishe mchakato wa uchaguzi hadi pale reforms zinazotakiwa zipatikane.
 
Ingekuwa vipi by Mwana FA

Nawaza mambo kwa kina lakini majibu sina.
 
Back
Top Bottom