Anna Nkya
Member
- Oct 21, 2021
- 69
- 341
Januari 12,22023 , Mbunge mstaafu wa Mbeya kwa tiketi ya CHADEMA , Joseph Mbilinyi alitweet" Nchi inaenda, so far so good. Hakuna tena kuokota viroba Coco, wala raia kutekwa ovyo na state.
Mengine yote yanazungumzika,na tutakutana kwenye mikutano ya hadhara soon. Mungu aendelee kuwapa busara viongozi wetu hawa (Rais Samia, Mbowe na Kinana"
Sugu kaongea ukweli sana.
Kwanza kwa kuangalia namna ambayo Rais Samia aliingia madarakani. Ni ngumu sana nchi kuvuka salama Rais anapoondoka madarakani kwa kufa, kupinduliwa au kujiuzulu. Wengi wanaangukia kwenye vita na machafuko makubwa. Rais Samia Suluhu alituvusha salama.
Pili tuangalie hali aliyoikuta, unachukua nchi kutoka kwa Rais ambaye kuna watu wanamuona kama dikteta, anaminya demokrasia na haki za watu. Rais Samia Suluhu ni mtu mpenda haki, ni mwanadiplomasia wa kweli. Alipoingia hatusikii watu kutekwa, kesi za hovyohovyo na ubabe mwingine. Tunaona sasa vyama vya upinzani vinarudi barabarani. Vikosi vya mabavu vya watoza ushuru havipo, kodi inakusanywa kwa haki na makusanyo yake yameongezeka.
Tatu, hali ya uchumi wa dunia imekuwa na matokeo mabaya kwa nchi yetu. Rais Samia Suluhu akakutana na lawama zisizomhusu kwenye mafuta, kupanda kwa bei za vyakula na bidhaa nyingine.
Lakini yeye ni mstahimilifu, akaja na ruzuku kwenye mafuta, mbolea na hatua nyingi anazochuku kutupunguzia machungu ya kuporomoka kwa uchumi wa dunia.
Bila Mama tungekuwa pabaya.
Asante Rais Samia Suluhu, naungana na Sugu kukupongeza.