Joseph Musukuma: Wazungu wanatuwekea ushoga kwenye chanjo; haiwezekani binti wa miaka 10 avae sidiria

Tuna Wataalamu Wetu wanaothibitisha hizo dawa lakini pia nadhani tuna watu wa kitengo wenye kuweza kufanya independent verification.

On top.of that hizo chanjo.sio Tanzania pekee zipo, Mabadiliko ya kimaumbile sio.kwenye chanjo tuu Bali ni changanyiko wa vitu vingi sana.

Mwisho ndio maana Samia anapambana kununua vifaa tiba,kuwezesha taasisi za kiytafiti za chakula,mifugo na Afya Ili walau hapo baadae let say by 2030-35 huko tuwe na 80% ya dawa made in Tanzania.
 
Kuna matstizo, mengi yenye madhara mi ccm inafanyia wananchi kuliko hata huo ushoga, JPM alitumia pesa nyingi kujenga uwanja wa ndege chato! Usio na faida!
Hauna marejesho ya kiuchumi, unatumia pesa nyingi kujenga apartments wilaya ya kyelwa, Kagera, kila apartment milioni 2 kwa mwezi! Nani, atakaa!? Utaishia kufuga mapaka, popo na njiwa tu!
 
Hawa Wazungu tunawaosingizia ubaya ndio watengeneza Tiba na Vifaa Tiba vinavyotumika nchini. Elimu ya Utabibu biomedical imetoka kwao. Halafu hormone za Ushoga zinaitwaje na ziko Eneo gani mwilini?
 
kama ni hivo kwwnini msitengeneze chanjo zenu?? hiyo akili ya kugundua mngeitumia kutengeneza chanjo zisizo na ushoga
 
Tatizo la kupewa Mdomo mkubwa bila shule.
 
Yaani Msukuma amefanya utafiti?
 
Kwanini Chanjo na sio vyakula na dawa?
Au anatafta Kick ya chanjo
Homoni ni protini mkuu. Haziwezi kuwekwa kwenye chakula kwa kuwa chakula kikipikwa zitakufa (hormones are denatured by heat). Ndio maana huwa zinawekwa kwenye chanjo.
 
Kweli kabisa mkuu. Umesahau midege aliyonunua jpm wakati kila mwaka ATCL inapata mabilioni ya hasara na kupoteza fedha za walipakodi ambazo zingetumika kufanya huduma za jamii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…