Joseph Musukuma: Wazungu wanatuwekea ushoga kwenye chanjo; haiwezekani binti wa miaka 10 avae sidiria

Joseph Musukuma: Wazungu wanatuwekea ushoga kwenye chanjo; haiwezekani binti wa miaka 10 avae sidiria

Hii ndio aina ya wabunge tunaostahili..vichwa maji aidha kwa makusudi au ndio asili yake..

Mzungu aache kushughulika na matatizo yake aje akuongezee mashoga. Kweli?

Na hiyo bora itaingia kwenye hansard ya bunge ila vizazi vijavyo vione wazazi wao tulivyokuwa wapumbavu tusio na mfano
 
Mtu huanza kuonekana and akili pale anapoanza kuhoji (question
Kabla ya kumnanga Msukuma, ni vyema kufuatilia mchango wake kwa makini
asa nini cha ajabu kwa binti wa miaka kumi kuota matiti yani had sayansi darasa la sita haijatusaidia puberty kwa mtoto wa kike kwa kawaida inaweza kuanza had na umri wa miaka nane
 
Kuna uwezekano mkubwa wazungu wanatuwekea homoni za ushoga kwenye chanjo.
Ushoga unaingia kupitia chanjo? Hii nchi tuna reasoning mbovu sana. Tafiti kafanya kwani yeye ni mtaalamu wa public health?

Mambo ya ukuaji wa mwili unahusiana nini na ushoga? Angesema obesity au ulaji mbovu sawa ila hakuna connection kati ya mtu kunenepa mapema na kuwa shoga!!

JPM ndio alikua baba wa conspiracy, alipinga chanjo ya Covid 19 ilihali alikua anatumia moyo wa betri wa beberu huyo huyo anayesema chanjo zake ni feki!!
 
Mtu huanza kuonekana and akili pale anapoanza kuhoji (questioning).

Kabla ya kumnanga Msukuma, ni vyema kufuatilia mchango wake kwa makini
It's nonsense, kuhoji ni kufanya tafiti sio kutoa assumptions eti ndio akili. Lini ameingia maabara kuprove hilo? Yaani mimi niamke niseme Wanawake kuota ndevu ni dalili ya usagaji basi nakua na akili kisa kuhoji?
 
Hizo Hormones za USHOGA zinafahamika ua zinaitwaje kwa kisayansi.

Halafu hao watoto wa miaka 7 - 8 wenye maziwa makubwa wako mitaa gani .... maana wengine hajuawaona huko mitaani. AU hizi ni consipirous theories .... maana Watanzania kila kitu kinaleta Ushoga. Colgate zilisambazwa mashuleni tukaambiwa zinaleta ushoga, chakula cha msaada kwa watoto wa shule kule Dodoma nao tukaambiwa ni unaleta ushoga .... sasa basi tupunguze kuagiza bidhaa kutoka nje.
Mpunguze kuagiza bidhaa nje kwa akili zipi mlizonazo za kujitegemea ?

Rais wenu mwenyewe muda wote hatulii nchini kwake, kazi kuzurura kwenye mataifa ya watu kwenda kuomba omba.
 
Back
Top Bottom