Joseph Selasini atimuliwa NCCR Mageuzi

Hapa hautaitwa MSALITI, bali utaitwa MSALITI ikiwa tu utatumia njia ambayo haipo ktk makubaliano ya taratibu za uwasilishaji wa mawazo hayo.

Na hapa ndipo wanasiasa wengi wanapokosa wakidhani ama wataongeza umaarufu ktk chama au kuitafuta Huruma badala ya kuwa uvumilivu wa kuendelea kushawishi kwa njia walizokubaliana ktk kundi.
 
Mkuu siasa ni itikadi lakini utashi wa mwanadamu hubadilika badilika Leo unaweza mkakubaliana hivi lakini kesho akabadilika kimtizamo juu ya jambo Hilo hilo mlilokubaliana jana.........Mimi nadhani kama amejipambanua kuwa hayuko pamoja na nyinyi katika Hilo hawezi kuitwa mnafiki......
 
Nakubaliana na wewe kabisa kwamba itikadi ya mwanadamu inaweza kubadilika tofauti na chama alichomo,

Tatizo lililopo kwa wanasiasa wetu ni kwamba, anapoona kuwa itikadi yake haiendani na chama alichojiunga anashindwa kuchukua hatua ambazo ni sahihi. Ama ajiondoe kwa uungwana au abakie lakini hapa akiendelea kuwa mvumilivu wa kuitafuta (njia sahihi iliyo rafiki na taratibu za chama) ya kumwezesha kuchopeka wazo lake la itikadi yake au mageuzi mengineyo.

Wanasiasa wanapoona huko walikoingia hakupo kama walivyo dhani hukurupuka na kuanza kutumia vyombo vya habari kutukana na kuandaa mbinu kharam za kupinduana.

Huu ni usaliti uliokubukh
 
Mpango ulikuwa Selasini apindue meza Ili awapokee COVID watapotimuliwa.

Hadi sasa pa kwenda hawana, mrema wafanyie hisani wamama Hawa!!!!
 
Duh aende TLP sasa

Maana wanasiasa wanahama kama

Wanacheza drafti tu

Ova
Ndio tujue kuwa siasa ni kazi tu ya kuingiza kipato kama kazi nyingine yeyote ile !! Habari ya kuwapigania wananchi hizo huwa ni abracadabra tu !!! Tusikate tamaa hakika Muumba yu pamoja nasi !! Ukiona giza limezidi ujue karibu kunapambazuka !!
 
Kwa unataka alichokifanya Selasini tukiiteje labda?
 
Aende kwa wasaliti wenzie ACT
 

..Ni tatizo la jamii nzima ya Watanzania.

..Wengi hatujalelewa ktk utamaduni wa kushindana kwa hoja bila kutukanana au character assasination.

..Tangu enzi za Tanu na baadae Ccm na sasa vyama vingi utamaduni wa kuitana majina mabaya umelelewa hapa nchini.

..Kwa mfano, Tanu walipopishana na Shekhe Takadiri wakaanza kumuita " Takadiri mtaka dini" badala ya kujadili hoja zake na kuzipangua.

..Oscar Kambona alipotofautiana na Nyerere hatukujadili hoja zake badala yake Tanu wakaanza kumuimba " Kambona kaolewa ulaya.."

..Hali hiyo imeendelea kiasi kwamba imekuwa ndio UTAMADUNI wetu. Unaweza kuiona hata hapa JF ambapo hoja nyingi huishia kwa wachangiaji kutupiana vijembe, au kutukanana.
 
Asante ndugu kwa kuchukua muda wako na kunitanabaisha kinaga ubaga.......sitaki kutoka mbali na msingi wa maelezo yako kwani ulichokiandika kimeakisi ukweli mzima wa hali ilivyo kwenye jamii yetu na Jf ikiwa ni sehemu ya jamii hiyo.........

Muendelezo wa hali hii inakuja Kuzaa jamii ya watu wanafiki.....na jamii ya watu wanafiki inazaa watu wasaliti wasio aminika.......bado tuna safari ndefu....
 
Mapinduzi ndo utaratibu
 
Ukiwa mwanasiasa unayehama kwa tamaa ya cheo,au fursa lazima utaaibika wakati ukifika.
 
Ni Kamanda Suzan Masselle na.Joseph Selasini ambao walikuwa wabunge wa Chadema kabla hawajaunga mkono juhudi za Nccr mageuzi

Wabunge hawa Wastaafu hawahitajiki tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…