JOSEPH SELASINI:MAISHA YANA SIRI KUBWA,TUSIMDHARAU TUMPE POLE

JOHNGERVAS

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2016
Posts
1,487
Reaction score
2,599
Anaandika Mbunge mstaafu wa Jimbo la Rombo

Eti kuna wanaomlaumu kwa kuwa hakujenga kwao.
Kwao ni wapi? kwa baba yake ni kwao? Kwa wajomba ni kwao? Yaani awajengee kaka/ wifi zake? Mimi naona sio sawa.
Lakini kuna anayejua maisha ya kwao? Kula kwao, elimu, matibabu nk?
Kwani haiwezekani huyu binti LULU DIVA nisiyemjua lakini namsoma tu kwenye vyombo vya habari ndiye pekee Mungu aliyempa kakipato kanakotegemewa na familia yote?
Kipato cha familia nyingi maeneo hayo zinajulikana. Minazi michache inayowawezesha kuuza madafu machache, miti kadhaa ya machungwa tunda la msimu, miti michache ya mifenesi nk
Nampongeza mtoto huyu wa kike ambae ktk familia alijitokeza kwa kipaji chake na kulea wenzake.
Kumuuguza mzazi aliyelala kitandani miaka nane(
😎
sio mchezo pamoja na huduma myingine nyingi za familia.
Nani asiyejua kipato cha wasanii? Nadhani wanaomdharau hasa wanaume tujitafakari sana. Huyu alitetea kwanza uhai wa mamake kwa kila njia halali na labda haramu.
Baadala ya kumdharau, kumkashifu, na kumbeza yafaa kumpa pole kwa msiba na kumpongeza.
Kitu alichohitaji mama yake kwa miaka nane haikuwa nyumba bali dawa.
Pole binti na
hongera

sana kwa kutimiza wajibu wako.
Nawajua wanaume waliokamatwa na wake zao na kuwasusa wazazi na ndugu zao kiasi cha kushindwa hata kupata mlo wa siku na wakafariki bila hata panadol.
Tujitafakari sana kabla ya kuelekeza mashambulizi yasiyo na maana kwa mtu yeyote.
 
tatizo milioni 500 alizotaka kama mahari huku akijua ni Laki mbili
Umechanganya madesa mkuu, huyu aliyefiwa na mama yake sio huyo wa mahari ya 500mil.
Ila kimsingi hawa watu/wasanii au machawa wa wasanii wanapenda kujionyesha maisha yao mtandaoni ni ya juu sana wakati kialisi sio kweli.
Ndio maana wakipata matatizo kama magonjwa au msiba watu wanaconcentrate kwenye mambo mengine kama nyumba, hali ya wazee kijijini mfano nguo walizovaa, vyoo ,barabara ya kuelekea home huko bushi
 
Naungana na Selasini, ila tatizo hawa wasanii wanajishaua na kujionesha kuwa wanafanikio makubwa mitandaoni na kuwa na maringo!
Wajifunze kuweka privancy za maisha yao na wasipende kuropoka kuwa wanamafanikio makubwa wawapo hasa kwenye interviews za vyombo vya habari!
Haiingii akilini msanii anaulizwa mahari yako ni kiasi gani, anajibu kwa kujishaua huku kabinua mdomo eti million 200!
 
Unakua unapata akili unakuta Baba na Mama hawana pa kuishi kifupi familia haina makazi na wewe ndio mtoto mkubwa.....ujenge nyumba ya familia, ujenge nyumba yako mwenyewe yakuishi wakati huo huo uwe unaendesha daily life ya familia wazee, wadogo zako na wewe mwenyewe na famili yako SIO KAZI NDOGO hii..

Africa ngumu sana hii, kama wewe umefanikiwa maisha yanakwenda shukuru Mungu...maana kuna wenzako wanapambana zaidi yako wewe lakini bila bila...
 
Asikufanganye mtu. Kwa wale wanaotegemea kuzikwa sehemu zao za asili kujenga nyumba presentable Ni muhimu.
Ni Kama kuvaa chupi japo watu hawaioni lkn Ni muhinu sana kuivaa.
Wapo wajomba wajenge lulu bado anajitahangaikia sana na alikuwa akiuguza mama yake
 
Unakua unapata akili unakuta Baba na Mama hawana pa kuishi kifupi familia haina makazi na wewe ndio mtoto mkubwa.....ujenge nyumba ya familia, ujenge nyumba yako mwenyewe yakuishi wakati huo huo uwe unaendesha daily life ya familia wazee, wadogo zako na wewe mwenyewe na famili yako SIO KAZI NDOGO hii..

Africa ngumu sana hii, kama wewe umefanikiwa maisha yanakwenda shukuru Mungu...maana kuna wenzako wanapambana zaidi yako wewe lakini bila bila...
Ndio ike ya kujidanganya kika mtoto na sahani yake kumbe unaumiza watoto
 
Wapo wajomba wajenge lulu bado anajitahangaikia sana na alikuwa akiuguza mama yake
Kama unategemea kuzikwa juu ya mifupa ya mtu kwenye makaburi ya Kinondoni, ruksa kutokujenga home.
Lakini Kama unataka ukapumzishwe na watu wa ukoo wako, acha kutegemea wajomba. Jenga kajumba matofali ya kuchoma, weka umeme, Rudi mjini kula Bata na michepuko.
 
Kwenye maisha kila mtu anapitia magumu yake, kuwa na magumu pia hakumfanyi mtu kushindwa kufurahia ya duniani angalau siku ziende.... Kuwa na kipato ni jambi lingine na kufanya maendeleo ni jambo lingine....

Wengi humu inawezekana tuna mafanikio lakini ukiangalia mafanikio yamekuja either kwa kupata chaneli fulani fulani au bahati ya kusomeshwa na kupata kibaru uhakika wakipato monthly...

Wapo wasio na channeli wala network za kuingiza hela kubwakubwa, wapo ambao hawajakwenda shule wanaunga maisha mtaani na wanategemewa...kinachopatikana ni kidogo cha kula, kulala, matibabu...kufanya extra kama kujenga, kununua magari unakuta mtu inamhitaji hata 30yrs to 40yrs..

Mfumo wa maisha ya kitanzania unalimitations sana juu ya upatikanaji wa kipato halali...watanzania wengi vipato vyetu ni vya ujanja ujanja na sio maisha halisi...ndio maana wengi ukiwapigia hesabu halisi utakuta ni wahujumu uchumi..
 
Unakua unapata akili unakuta Baba na Mama hawana pa kuishi kifupi familia haina makazi na wewe ndio mtoto mkubwa.....ujenge nyumba ya familia, ujenge nyumba yako mwenyewe yakuishi wakati huo huo uwe unaendesha daily life ya familia wazee, wadogo zako na wewe mwenyewe na famili yako SIO KAZI NDOGO hii..

Africa ngumu sana hii, kama wewe umefanikiwa maisha yanakwenda shukuru Mungu...maana kuna wenzako wanapambana zaidi yako wewe lakini bila bila...

Mkuu kuna kupambana tujikwamue kwenye nafasi ya chini tuliyokuwepo kwenda nafasi nzuri.
Tatizo ni la hawa watu wanaojisifia mitandao vitu vya kijinga na sio vya msingi.
Kama huyo aliyefiwa juzi kuna interview yake niliiyona anaeleza vitu alivyotupia wigi la milioni na zaidi,cheni milioni 2na zaid,nguo za milioni na zaidi,handbag mbili milioni na viatu, sijui saa hereni alikuwa anajisifia amevaa vitu vya zaidi ya milioni 8.
Ukiangalia kwa makini unakuta sio kweli,sasa mtu kama huyo akipata matatizo watu wanakumbuka kauli zao kama hizo na kuanza kuwazodoa
 
Kama unategemea kuzikwa juu ya mifupa ya mtu kwenye makaburi ya Kinondoni, ruksa kutokujenga home.
Lakini Kama unataka ukapumzishwe na watu wa ukoo wako, acha kutegemea wajomba. Jenga kajumba matofali ya kuchoma, weka umeme, Rudi mjini kula Bata na michepuko.
Inategemea na uwezo wangu sina najengaje?ukoo mzima wameshindwa jenga nijenge mie maisha yangu yenyewe ya kusua sua
 
Mkuu kuna kupambana tujikwamue kwenye nafasi ya chini tuliyokuwepo kwenda nafasi nzuri.
Tatizo ni la hawa watu wanaojisifia mitandao vitu vya kijinga na sio vya msingi.
Kama huyo aliyefiwa juzi kuna interview yake niliiyona anaeleza vitu alivyotupia wigi la milioni na zaidi,cheni milioni 2na zaid,nguo za milioni na zaidi,handbag mbili milioni na viatu, sijui saa hereni alikuwa anajisifia amevaa vitu vya zaidi ya milioni 8.
Ukiangalia kwa makini unakuta sio kweli,sasa mtu kama huyo akipata matatizo watu wanakumbuka kauli zao kama hizo na kuanza kuwazodoa
Mtu mmoja anavaa vitu vya M?
Niko na mchina hapa sait kwangu. Ndio fundi wangu mkuu.
Jumapili unamkuta kavaa
Yeboyebo za buku tatu
Jeans ya elfu kumi na Saba
T shirt ya buku tano.
Halafu namlipa kwa dola mshahara wa expertriate
 
Mkuu kuna kupambana tujikwamue kwenye nafasi ya chini tuliyokuwepo kwenda nafasi nzuri.
Tatizo ni la hawa watu wanaojisifia mitandao vitu vya kijinga na sio vya msingi.
Kama huyo aliyefiwa juzi kuna interview yake niliiyona anaeleza vitu alivyotupia wigi la milioni na zaidi,cheni milioni 2na zaid,nguo za milioni na zaidi,handbag mbili milioni na viatu, sijui saa hereni alikuwa anajisifia amevaa vitu vya zaidi ya milioni 8.
Ukiangalia kwa makini unakuta sio kweli,sasa mtu kama huyo akipata matatizo watu wanakumbuka kauli zao kama hizo na kuanza kuwazodoa

shida ya hawa mabinti wengi wamekuja mjini wanatumika na watu kwa ajili ya biashara zao..masikini na wao kutojua wanaingi kwenye mkumbo wa kimjini kwa ajili ya maslahi ya watu.

Matajiri wao aka mamentor wao wa mjini ndio huwajaza ujinga kwa kuwafundisha namna ya kuishi kwa lugha ya "kuishi star" kwa namna hii wengi hulazimika kufake wakiamini wanajibrand na kuwa na thamani lakini ukweli behind the scene wananufaisha watu fulani na wao kuishia kukwadiwa kwa masponsor na kuishi kupewa material thing kwa ajili ya kuishi mjini....

Kiukweli kwa hiyo tafsiri kama kweli..alivaa vitu vya gharama hizo anastahili kupewa lawama....maana angeweza hata kuikarabati the same house, hata kwa kupiga cement lipu, madirisha ya kisasa, tiles chini...kufanyia usafi area around ikiwa sambasamba na kupanda miti ambayo haina gharama, kuweka gardeni, miti miti ya matunda area around...viti ya miti area around na kwa tafsiri ya usanini wake Nyumba na eneo kuzunguka ingekuwa kama culture fulani..
 
Vijana tunabebeshwa mzigo mkubwa sana Yani ukipata kazi unatakiwa uishi kwanza maisha ya wazazi wako kabla ya kuanza kuishi maisha yako, uwajengee wazaz na ww uje kujijengea tena na kwako kwakweli ni mzigo mzito kwa sisi wenye vipato vya kawaida.
Mm nitaishi kama waarabu na wahindi najenga nyumba moja kubwa familia yangu yote ikae hapo na hata watoto wangu badae hiyo hela ya kujenga ni Bora waanzishe biashara ili tujikwamue kwanza kiuchumi
 
Inategemea na uwezo wangu sina najengaje?ukoo mzima wameshindwa jenga nijenge mie maisha yangu yenyewe ya kusua sua

hahahaha, eti ukoo mzima umeshindwa kujenga halafu ndio ujenge wewe.....
 
Anaandika Mbunge mstaafu wa Jimbo la Rombo

Eti kuna wanaomlaumu kwa kuwa hakujenga kwao.
Kwao ni wapi? kwa baba yake ni kwao? Kwa wajomba ni kwao? Yaani awajengee kaka/ wifi zake? Mimi naona sio sawa.
Lakini kuna anayejua maisha ya kwao? Kula kwao, elimu, matibabu nk?
Kwani haiwezekani huyu binti LULU DIVA nisiyemjua lakini namsoma tu kwenye vyombo vya habari ndiye pekee Mungu aliyempa kakipato kanakotegemewa na familia yote?
Kipato cha familia nyingi maeneo hayo zinajulikana. Minazi michache inayowawezesha kuuza madafu machache, miti kadhaa ya machungwa tunda la msimu, miti michache ya mifenesi nk
Nampongeza mtoto huyu wa kike ambae ktk familia alijitokeza kwa kipaji chake na kulea wenzake.
Kumuuguza mzazi aliyelala kitandani miaka nane(
😎
sio mchezo pamoja na huduma myingine nyingi za familia.
Nani asiyejua kipato cha wasanii? Nadhani wanaomdharau hasa wanaume tujitafakari sana. Huyu alitetea kwanza uhai wa mamake kwa kila njia halali na labda haramu.
Baadala ya kumdharau, kumkashifu, na kumbeza yafaa kumpa pole kwa msiba na kumpongeza.
Kitu alichohitaji mama yake kwa miaka nane haikuwa nyumba bali dawa.
Pole binti na
hongera

sana kwa kutimiza wajibu wako.
Nawajua wanaume waliokamatwa na wake zao na kuwasusa wazazi na ndugu zao kiasi cha kushindwa hata kupata mlo wa siku na wakafariki bila hata panadol.
Tujitafakari sana kabla ya kuelekeza mashambulizi yasiyo na maana kwa mtu yeyote.
Mbaya Zaidi walao mlaumu wengine bado wanaishi kwao.
 
Back
Top Bottom