JOSEPH SELASINI:MAISHA YANA SIRI KUBWA,TUSIMDHARAU TUMPE POLE

JOSEPH SELASINI:MAISHA YANA SIRI KUBWA,TUSIMDHARAU TUMPE POLE

Inategemea na uwezo wangu sina najengaje?ukoo mzima wameshindwa jenga nijenge mie maisha yangu yenyewe ya kusua sua

Hapo utaeleweka,tatizo linaanza pale unapojikweza mitandaoni umevaa kuanzia juu hadi chini ni 8million.
Ukipata janga kama la huyo lulu lazima watu wakunange.
Watu watafikiria ile milioni 8 si angejenga hata kaslope ka matofali ya kuchoma huko kijijini kwa mama yake ingekuwa maana kuliopo mazingira yale yalivyokuwa hovyo kwa mtu anayevaa nguo za milioni 8 na kutembelea gari ya mil 40
 
Vijana tunabebeshwa mzigo mkubwa sana Yani ukipata kazi unatakiwa uishi kwanza maisha ya wazazi wako kabla ya kuanza kuishi maisha yako, uwajengee wazaz na ww uje kujijengea tena na kwako kwakweli ni mzigo mzito kwa sisi wenye vipato vya kawaida.
Mm nitaishi kama waarabu na wahindi najenga nyumba moja kubwa familia yangu yote ikae hapo na hata watoto wangu badae hiyo hela ya kujenga ni Bora waanzishe biashara ili tujikwamue kwanza kiuchumi

yah, hili ni tatizo la Africa....ni wakati wa kizazi kipya kubadili huu mfumo kwa kuamua kuishi tofauti na kujenga familia ambazo hazihitaji kutegemeana....

Huo mfumo wa kujenga lijumba mooja likubwa na kuweka familia yote hapo ni nzuri sana..angalau unaweza kuwa free... ukianza kuwaza kujengea wazazi na wewe ujenge sijui kule kijijini nitakapozikwa....unaweza kujikuta unazeeka hujafanya kitu zaidi ya kujenga..
 
hahahaha, eti ukoo mzima umeshindwa kujenga halafu ndio ujenge wewe.....
Ambae najihangaikia napuyanga niache kujenga kwanza kwangu nikajenge kwa ndugu zangu ,hivi unajua ndugu wewe tunakuwaga hata hatupendani kwanza ukiwa we na mama yako ni maskin ndio mnadharaurika haswa
 
Anaandika Mbunge mstaafu wa Jimbo la Rombo

Eti kuna wanaomlaumu kwa kuwa hakujenga kwao.
Kwao ni wapi? kwa baba yake ni kwao? Kwa wajomba ni kwao? Yaani awajengee kaka/ wifi zake? Mimi naona sio sawa.
Lakini kuna anayejua maisha ya kwao? Kula kwao, elimu, matibabu nk?
Kwani haiwezekani huyu binti LULU DIVA nisiyemjua lakini namsoma tu kwenye vyombo vya habari ndiye pekee Mungu aliyempa kakipato kanakotegemewa na familia yote?
Kipato cha familia nyingi maeneo hayo zinajulikana. Minazi michache inayowawezesha kuuza madafu machache, miti kadhaa ya machungwa tunda la msimu, miti michache ya mifenesi nk
Nampongeza mtoto huyu wa kike ambae ktk familia alijitokeza kwa kipaji chake na kulea wenzake.
Kumuuguza mzazi aliyelala kitandani miaka nane(
😎
sio mchezo pamoja na huduma myingine nyingi za familia.
Nani asiyejua kipato cha wasanii? Nadhani wanaomdharau hasa wanaume tujitafakari sana. Huyu alitetea kwanza uhai wa mamake kwa kila njia halali na labda haramu.
Baadala ya kumdharau, kumkashifu, na kumbeza yafaa kumpa pole kwa msiba na kumpongeza.
Kitu alichohitaji mama yake kwa miaka nane haikuwa nyumba bali dawa.
Pole binti na
hongera

sana kwa kutimiza wajibu wako.
Nawajua wanaume waliokamatwa na wake zao na kuwasusa wazazi na ndugu zao kiasi cha kushindwa hata kupata mlo wa siku na wakafariki bila hata panadol.
Tujitafakari sana kabla ya kuelekeza mashambulizi yasiyo na maana kwa mtu yeyote.
KINACHO WASHANGAZA WATU, NI AINA YA MAISHA YA MTU ANAVYO ISHI, ILE LIFESTYLE YA KUJIONA UNAZO ZA KUTOSHA.YAFAA NINI SASA KUIGIZA KAMA ZIPO WAKATI HAZIPO?
 
Vijana tunabebeshwa mzigo mkubwa sana Yani ukipata kazi unatakiwa uishi kwanza maisha ya wazazi wako kabla ya kuanza kuishi maisha yako, uwajengee wazaz na ww uje kujijengea tena na kwako kwakweli ni mzigo mzito kwa sisi wenye vipato vya kawaida.
Mm nitaishi kama waarabu na wahindi najenga nyumba moja kubwa familia yangu yote ikae hapo na hata watoto wangu badae hiyo hela ya kujenga ni Bora waanzishe biashara ili tujikwamue kwanza kiuchumi
Nop tatizo Baadhi ya vijana akipata kazi anaanza kujipa mizigo ya ajabu yeye mwenyewe,
Kufake life iG kwamba keshatoka kimaisha, wapuudhi wengine wanapiga picha hotelini anakwambia amechili home.
Vijana acheni kujipa mizigo ya kufake life kwa kupost mapost ya uongo mitandaoni mnajitesa sana
 
shida ya hawa mabinti wengi wamekuja mjini wanatumika na watu kwa ajili ya biashara zao..masikini na wao kutojua wanaingi kwenye mkumbo wa kimjini kwa ajili ya maslahi ya watu.

Matajiri wao aka mamentor wao wa mjini ndio huwajaza ujinga kwa kuwafundisha namna ya kuishi kwa lugha ya "kuishi star" kwa namna hii wengi hulazimika kufake wakiamini wanajibrand na kuwa na thamani lakini ukweli behind the scene wananufaisha watu fulani na wao kuishia kukwadiwa kwa masponsor na kuishi kupewa material thing kwa ajili ya kuishi mjini....

Kiukweli kwa hiyo tafsiri kama kweli..alivaa vitu vya gharama hizo anastahili kupewa lawama....maana angeweza hata kuikarabati the same house, hata kwa kupiga cement lipu, madirisha ya kisasa, tiles chini...kufanyia usafi area around ikiwa sambasamba na kupanda miti ambayo haina gharama, kuweka gardeni, miti miti ya matunda area around...viti ya miti area around na kwa tafsiri ya usanini wake Nyumba na eneo kuzunguka ingekuwa kama culture fulani..
Jamen lulu pale ni kwa wajomba zake wajomba zake wapo wajengee lulu anatakiwa ajenge kwake
 
Nop tatizo Baadhi ya vijana akipata kazi anaanza kujipa mizigo ya ajabu yeye mwenyewe,
Kufake life iG kwamba keshatoka kimaisha, wapuudhi wengine wanapiga picha hotelini anakwambia amechili home.
Vijana acheni kujipa mizigo ya kufake life kwa kupost mapost ya uongo mitandaoni mnajitesa sana
Ndo maana watu wanasema mitandao ya kijamii imefanya tuwaonee wivu watu ambao tulistahili kuwahurumia , wasanii wengi/vijana wengi huwa tunapenda kufake maisha, na kushindana na watu muda mwngne mtu unashindana starehe na mtu ambae kwao katokea familia Bora na wakat wewe kwenu wazaz wako nyumba inataka kuwaangukia, ni bora uwe humble tu ukijikweza sana lazima ulaumiwe maana kila mtu atakuona mjinga kwa kushindwa kusaidia wazaz wako
 
Nadhani utamaduni wa kuwajengea nyumba nzuri wazazi umeanzia kwetu vijana wa kileo...sidhani kama wazazi wetu waliwajengea nyumba nzuri wazazi wao..au nasema uongo ndugu zangu??......
 
Inategemea na uwezo wangu sina najengaje?ukoo mzima wameshindwa jenga nijenge mie maisha yangu yenyewe ya kusua sua
Huku mjini full bata unabadili magari na party kila siku pumbavy
 
Ile nyumba si mbaya milioni mbili tu ingetosha kuipiga plasta na kuipaka rangi dah mbavu za mbwa mie
 
Tatizo Hawa wanaojiita wasanii huwa na mbwembwe sana na ndio maana wanasakamwa, utasikia nimenunua cheni ya milioni Mia mbili, sasa inategemea watu wakusemaje? Mbona Kuna watu kwao kwa kawaida na watu hawawasemi sababu they humble themselves????

Mtu mwenyewe muuza K Ila kila wakati mbwembwe kibao, ndio waache kujitamba.
 
kibongo bongo wanajua ukiwa superstar ni lazima uwe tajiri sana kumbe....
 
Tatizo sio kujenga kwao tatizo ni maisha wanayotuaminisha wanayoishi mitandaoni, tunahisi kwao mambo safi maana kila siku yuko airport na kwenye mahoteli ya 5 star kumbe kwao kuko vile mi namlaumu kwa hilo wanajisahau sana.
 
Mtu mmoja anavaa vitu vya M?
Niko na mchina hapa sait kwangu. Ndio fundi wangu mkuu.
Jumapili unamkuta kavaa
Yeboyebo za buku tatu
Jeans ya elfu kumi na Saba
T shirt ya buku tano.
Halafu namlipa kwa dola mshahara wa expertriate
Huyo mchina watoto wake wanavaa vya milion kwa siku
 
Nop tatizo Baadhi ya vijana akipata kazi anaanza kujipa mizigo ya ajabu yeye mwenyewe,
Kufake life iG kwamba keshatoka kimaisha, wapuudhi wengine wanapiga picha hotelini anakwambia amechili home.
Vijana acheni kujipa mizigo ya kufake life kwa kupost mapost ya uongo mitandaoni mnajitesa sana
Instagram hakuna masikini wote tunazo
 
Back
Top Bottom