evangelical
JF-Expert Member
- Nov 21, 2011
- 5,989
- 9,948
Inategemea na uwezo wangu sina najengaje?ukoo mzima wameshindwa jenga nijenge mie maisha yangu yenyewe ya kusua sua
Vijana tunabebeshwa mzigo mkubwa sana Yani ukipata kazi unatakiwa uishi kwanza maisha ya wazazi wako kabla ya kuanza kuishi maisha yako, uwajengee wazaz na ww uje kujijengea tena na kwako kwakweli ni mzigo mzito kwa sisi wenye vipato vya kawaida.
Mm nitaishi kama waarabu na wahindi najenga nyumba moja kubwa familia yangu yote ikae hapo na hata watoto wangu badae hiyo hela ya kujenga ni Bora waanzishe biashara ili tujikwamue kwanza kiuchumi
Ambae najihangaikia napuyanga niache kujenga kwanza kwangu nikajenge kwa ndugu zangu ,hivi unajua ndugu wewe tunakuwaga hata hatupendani kwanza ukiwa we na mama yako ni maskin ndio mnadharaurika haswahahahaha, eti ukoo mzima umeshindwa kujenga halafu ndio ujenge wewe.....
KINACHO WASHANGAZA WATU, NI AINA YA MAISHA YA MTU ANAVYO ISHI, ILE LIFESTYLE YA KUJIONA UNAZO ZA KUTOSHA.YAFAA NINI SASA KUIGIZA KAMA ZIPO WAKATI HAZIPO?Anaandika Mbunge mstaafu wa Jimbo la Rombo
Eti kuna wanaomlaumu kwa kuwa hakujenga kwao.
Kwao ni wapi? kwa baba yake ni kwao? Kwa wajomba ni kwao? Yaani awajengee kaka/ wifi zake? Mimi naona sio sawa.
Lakini kuna anayejua maisha ya kwao? Kula kwao, elimu, matibabu nk?
Kwani haiwezekani huyu binti LULU DIVA nisiyemjua lakini namsoma tu kwenye vyombo vya habari ndiye pekee Mungu aliyempa kakipato kanakotegemewa na familia yote?
Kipato cha familia nyingi maeneo hayo zinajulikana. Minazi michache inayowawezesha kuuza madafu machache, miti kadhaa ya machungwa tunda la msimu, miti michache ya mifenesi nk
Nampongeza mtoto huyu wa kike ambae ktk familia alijitokeza kwa kipaji chake na kulea wenzake.
Kumuuguza mzazi aliyelala kitandani miaka nane(sio mchezo pamoja na huduma myingine nyingi za familia.
Nani asiyejua kipato cha wasanii? Nadhani wanaomdharau hasa wanaume tujitafakari sana. Huyu alitetea kwanza uhai wa mamake kwa kila njia halali na labda haramu.
Baadala ya kumdharau, kumkashifu, na kumbeza yafaa kumpa pole kwa msiba na kumpongeza.
Kitu alichohitaji mama yake kwa miaka nane haikuwa nyumba bali dawa.
Pole binti na
hongera
sana kwa kutimiza wajibu wako.
Nawajua wanaume waliokamatwa na wake zao na kuwasusa wazazi na ndugu zao kiasi cha kushindwa hata kupata mlo wa siku na wakafariki bila hata panadol.
Tujitafakari sana kabla ya kuelekeza mashambulizi yasiyo na maana kwa mtu yeyote.
Nop tatizo Baadhi ya vijana akipata kazi anaanza kujipa mizigo ya ajabu yeye mwenyewe,Vijana tunabebeshwa mzigo mkubwa sana Yani ukipata kazi unatakiwa uishi kwanza maisha ya wazazi wako kabla ya kuanza kuishi maisha yako, uwajengee wazaz na ww uje kujijengea tena na kwako kwakweli ni mzigo mzito kwa sisi wenye vipato vya kawaida.
Mm nitaishi kama waarabu na wahindi najenga nyumba moja kubwa familia yangu yote ikae hapo na hata watoto wangu badae hiyo hela ya kujenga ni Bora waanzishe biashara ili tujikwamue kwanza kiuchumi
Tunasubiria kwao mwakinyo
Jamen lulu pale ni kwa wajomba zake wajomba zake wapo wajengee lulu anatakiwa ajenge kwakeshida ya hawa mabinti wengi wamekuja mjini wanatumika na watu kwa ajili ya biashara zao..masikini na wao kutojua wanaingi kwenye mkumbo wa kimjini kwa ajili ya maslahi ya watu.
Matajiri wao aka mamentor wao wa mjini ndio huwajaza ujinga kwa kuwafundisha namna ya kuishi kwa lugha ya "kuishi star" kwa namna hii wengi hulazimika kufake wakiamini wanajibrand na kuwa na thamani lakini ukweli behind the scene wananufaisha watu fulani na wao kuishia kukwadiwa kwa masponsor na kuishi kupewa material thing kwa ajili ya kuishi mjini....
Kiukweli kwa hiyo tafsiri kama kweli..alivaa vitu vya gharama hizo anastahili kupewa lawama....maana angeweza hata kuikarabati the same house, hata kwa kupiga cement lipu, madirisha ya kisasa, tiles chini...kufanyia usafi area around ikiwa sambasamba na kupanda miti ambayo haina gharama, kuweka gardeni, miti miti ya matunda area around...viti ya miti area around na kwa tafsiri ya usanini wake Nyumba na eneo kuzunguka ingekuwa kama culture fulani..
Wabongo tunavyoongea weeeHahahaaaaa uzuri wa huyu mwamba hanaga mashow off ya kijinga mitandaoni
Ndo maana watu wanasema mitandao ya kijamii imefanya tuwaonee wivu watu ambao tulistahili kuwahurumia , wasanii wengi/vijana wengi huwa tunapenda kufake maisha, na kushindana na watu muda mwngne mtu unashindana starehe na mtu ambae kwao katokea familia Bora na wakat wewe kwenu wazaz wako nyumba inataka kuwaangukia, ni bora uwe humble tu ukijikweza sana lazima ulaumiwe maana kila mtu atakuona mjinga kwa kushindwa kusaidia wazaz wakoNop tatizo Baadhi ya vijana akipata kazi anaanza kujipa mizigo ya ajabu yeye mwenyewe,
Kufake life iG kwamba keshatoka kimaisha, wapuudhi wengine wanapiga picha hotelini anakwambia amechili home.
Vijana acheni kujipa mizigo ya kufake life kwa kupost mapost ya uongo mitandaoni mnajitesa sana
Ndo tunge paona hapo kwake ata Chumba na sebuleJamen lulu pale ni kwa wajomba zake wajomba zake wapo wajengee lulu anatakiwa ajenge kwake
Huku mjini full bata unabadili magari na party kila siku pumbavyInategemea na uwezo wangu sina najengaje?ukoo mzima wameshindwa jenga nijenge mie maisha yangu yenyewe ya kusua sua
Huyo mchina watoto wake wanavaa vya milion kwa sikuMtu mmoja anavaa vitu vya M?
Niko na mchina hapa sait kwangu. Ndio fundi wangu mkuu.
Jumapili unamkuta kavaa
Yeboyebo za buku tatu
Jeans ya elfu kumi na Saba
T shirt ya buku tano.
Halafu namlipa kwa dola mshahara wa expertriate
Instagram hakuna masikini wote tunazoNop tatizo Baadhi ya vijana akipata kazi anaanza kujipa mizigo ya ajabu yeye mwenyewe,
Kufake life iG kwamba keshatoka kimaisha, wapuudhi wengine wanapiga picha hotelini anakwambia amechili home.
Vijana acheni kujipa mizigo ya kufake life kwa kupost mapost ya uongo mitandaoni mnajitesa sana