Joseph Selasini: Mwaka 2020 Mbatia alitupeleka na Anthony Komu kwa Dkt. Bashiru Ally kufanya makubaliano na CCM

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1653575227810.png

Picha: Joseph Selasini

Joseph Selasini: Kuna barua inaonekana kusambaa katika mitandao ya kijamii ikidaiwa kusaini wa na katiba kata wa Makiidi nyumbani kwetu, ikinihusisha mimi na uanachama wa CHADEMA. Niliondoka CHADEMA mwezi Juni 2020, na tangu nilipoondoka CHADEMA sikurejea tena"
Joseph Selasini: Mimi ni mwanachama wa NCCR, barua inayoendelea hivi sasa mitandaoni, imewekwa na watu wenye nia ovu, kama ningeomba kurejea CHADEMA na ningeandika barua, basi ingewekwa barua ya mimi kuomba kurejea CHADEMA na si barua ile"
Joseph Selasini: Sheria ya vyama vya siasa inaitaka kila chama Kuwasilisha kwa msajili wa vyama vya siasa nchini majina ya wanachama wote ambao ni wajumbe wa Kamati Kuu, Halmashauri Kuu, Baraza Kuu na Kamati kuu, hivyo wanaotaka kuthibitisha uanachama wangu, wakatafute hapo"

Joseph Selasini: Tangu ulipofanyika mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM, maneno mengi yamesemwa kwamba kilikuwa na mapinduzi, naomba niseme kwamba hapakuwa na mapinduzi bali kulikuwa na kikao halali cha Halmshauri Kuu kilichotimiza akidi"
Joseph Selasini: Maneno ya kwamba Joseph Selasini amempindua Mbatia ni maneno ya kejeli, uchochezi, uzushi na uongo. Ni maneno yanayojaribu kujenga dhana ya kwamba, wenyeviti wa vyama vya siasa ni wakubwa kuliko katiba ya vyama vyao na hawawezi kujadiliwa"

Joseph Selasini: Halmashauri Kuu ya NCCR Mageuzi na ya chama chochote cha siasa, haina mamlaka ya kikatiba ya kumfukuza Mwenyekiti wa chama, mamlaka ya Halmshauri Kuu ni kumsimamisha mwenyekiti, ni kama mfanyakazi anaposimamishwa kupisha uchunguzi"

Joseph Selasini: Sidhani kama Mwenyekiti aliyeongoza chama kwa miaka 23 anaweza kuogopa mkutano mkuu, au afanye vikao nje ya ya katiba ha utaratibu ili ajenge hofu ili watu wakuunge mkono"

Joseph Selasini: Moja ya jambo ambalo Mwenyekiti wetu (James Mbatia) ambalo anatuhumiwa nalo kwa muda mrefu ni uhusiano wake na Chama cha Mapinduzi (CCM), hata baadhi ya vyama vingine vya siasa vimekuwa vikisema kuwa hatumwelewi Mbatia ana uhusiano gani na CCM"

Joseph Selasini: Mimi na Anthony Komu tuliporudi NCCR Mageuzi mwaka 2020 Mbatia alitupeleka hadi kwa Dkt.Bashiru Ally kwa lengo la kufanya makubaliano ya kuisaidia CCM kwenye uchaguzi,tulipotoka kwenye kikao hicho tulikubaliana mimi na Komu kutoshiriki uharamu huo".
1653576084368.png

Barua inayodaiwa kuwa ya CHADEMA inayomtaja Selasini kuwa aliomba kadi yao

Chanzo: Dar Mpya Blog
 
"Mimi na Anthony Komu tuliporudi NCCR Mageuzi mwaka 2020 Mbatia alitupeleka hadi kwa Dkt.Bashiru Ally kwa lengo la kufanya makubaliano ya kuisaidia CCM kwenye uchaguzi,tulipotoka kwenye kikao hicho tulikubaliana mimi na Komu kutoshiriki uharamu huo"

Aisee kumbe. Kujifanya NCCR Mageuzi kuwa chama kikuu Cha upinzani, lakini mwishoni wakatoswa.
 
Hapo ndio ugomvi unapoanzia, Mbatia akapewa shs. 500 miliion kuisaidia ccm kwenye uchaguzi 2020; Selasini na Komu hawakuambulia kitu!!! Lakini kwenye sakata hili Komu yuko na Mbatia!! Hawa wachaga wanachezea saccos yao!!!
 
Kwanini hawakusema wakati ule ule kama ni kweli yeye na Komu waliamuwa “kutokushiriki haramu hiyo”?

Na kwasasa hivi nani anawasaidia ccm kama siyo yeye akishirikiana na msajili wa vyama?

Akili za kuambiwa…
 
Hapo ndio ugomvi unapoanzia, Mbatia akapewa shs. 500 miliion kuisaidia ccm kwenye uchaguzi 2020; Selasini na Komu hawakuambulia kitu!!! Lakini kwenye sakata hili Komu yuko na Mbatia!! Hawa emek
 
View attachment 2239563
Picha: Joseph Selasini

Joseph Selasini: Kuna barua inaonekana kusambaa katika mitandao ya kijamii ikidaiwa kusaini wa na katiba kata wa Makiidi nyumbani kwetu, ikinihusisha mimi na uanachama wa CHADEMA. Niliondoka CHADEMA mwezi Juni 2020, na tangu nilipoondoka CHADEMA sikurejea tena"
Joseph Selasini: Mimi ni mwanachama wa NCCR, barua inayoendelea hivi sasa mitandaoni, imewekwa na watu wenye nia ovu, kama ningeomba kurejea CHADEMA na ningeandika barua, basi ingewekwa barua ya mimi kuomba kurejea CHADEMA na si barua ile"
Joseph Selasini: Sheria ya vyama vya siasa inaitaka kila chama Kuwasilisha kwa msajili wa vyama vya siasa nchini majina ya wanachama wote ambao ni wajumbe wa Kamati Kuu, Halmashauri Kuu, Baraza Kuu na Kamati kuu, hivyo wanaotaka kuthibitisha uanachama wangu, wakatafute hapo"

Joseph Selasini: Tangu ulipofanyika mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM, maneno mengi yamesemwa kwamba kilikuwa na mapinduzi, naomba niseme kwamba hapakuwa na mapinduzi bali kulikuwa na kikao halali cha Halmshauri Kuu kilichotimiza akidi"
Joseph Selasini: Maneno ya kwamba Joseph Selasini amempindua Mbatia ni maneno ya kejeli, uchochezi, uzushi na uongo. Ni maneno yanayojaribu kujenga dhana ya kwamba, wenyeviti wa vyama vya siasa ni wakubwa kuliko katiba ya vyama vyao na hawawezi kujadiliwa"

Joseph Selasini: Halmashauri Kuu ya NCCR Mageuzi na ya chama chochote cha siasa, haina mamlaka ya kikatiba ya kumfukuza Mwenyekiti wa chama, mamlaka ya Halmshauri Kuu ni kumsimamisha mwenyekiti, ni kama mfanyakazi anaposimamishwa kupisha uchunguzi"

Joseph Selasini: Sidhani kama Mwenyekiti aliyeongoza chama kwa miaka 23 anaweza kuogopa mkutano mkuu, au afanye vikao nje ya ya katiba ha utaratibu ili ajenge hofu ili watu wakuunge mkono"

Joseph Selasini: Moja ya jambo ambalo Mwenyekiti wetu (James Mbatia) ambalo anatuhumiwa nalo kwa muda mrefu ni uhusiano wake na Chama cha Mapinduzi (CCM), hata baadhi ya vyama vingine vya siasa vimekuwa vikisema kuwa hatumwelewi Mbatia ana uhusiano gani na CCM"

Joseph Selasini: Mimi na Anthony Komu tuliporudi NCCR Mageuzi mwaka 2020 Mbatia alitupeleka hadi kwa Dkt.Bashiru Ally kwa lengo la kufanya makubaliano ya kuisaidia CCM kwenye uchaguzi,tulipotoka kwenye kikao hicho tulikubaliana mimi na Komu kutoshiriki uharamu huo".

Chanzo: Dar Mpya Blog
Mbona hakusema kuhusu vile vitita walivyolipwa ?
 
Mbatia ni afisa kipenyo wa mda mrefu sana
Mbatia ni mchumia tumbo tu. Hana uafisa wowote. Uchaguzi wa mwaka 2020 walipoitwa na Magufuli, waliahidiwa vyeo na fedha za kusaidia kampeni zao na wao wapewe baadhi ya nafasi za ubunge na kuwa chama cha upinzani kitiifu kwa mwendazake. Hali ilikuja kubadilika baada ya Chadema kumsimamisha Lissu na kuvutia umati mkubwa wa watu.

Magufuli alipoona hali ni mbaya kwake akaamua kutumia dola kupora uchaguzi na akawatupilia mbali hawa wachumia tumbo kwani aliona hawana uwezo wa kupambana na Chadema.
 
"Mimi na Anthony Komu tuliporudi NCCR Mageuzi mwaka 2020 Mbatia alitupeleka hadi kwa Dkt.Bashiru Ally kwa lengo la kufanya makubaliano ya kuisaidia CCM kwenye uchaguzi,tulipotoka kwenye kikao hicho tulikubaliana mimi na Komu kutoshiriki uharamu huo"
Kwanini hawakusema wakati ule ule kama ni kweli yeye na Komu waliamuwa “kutokushiriki haramu hiyo”?

Na kwasasa hivi nani anawasaidia ccm kama siyo yeye akishirikiana na msajili wa vyama?

Akili za kuambiwa…
Hawa wafanya biashara wamegundua kuwa fursa ziko kwenye Siasa hivyo wanacheza humo humo!!!
 
Back
Top Bottom