Naanza kwa kuwashukuru wote,naheshimu mawazo na mchango wa kila mmoja kwani kila mtu ananena kilichomo ndani ya moyo wake.Jambo moja tu naloweza kusema sikumpata mtoto kwa bahati mbaya wala kumbahatisha,nilimtamani na kumuhitaji hivyo namshukuru Mungu ameniwezesha,kwangu mimi ni mtoto wa thamani sana Namtukuza Mungu wakati wote.
kwenu ninyi mnaomtamkia maneno yafedheha nayarudisha kwenu na familia zenu,Mungu aliyeniumba hajanihesabia dhambi iweje ninyi?
Hatutayumbishwa na maneno ya watu tutamuangalia Mungu aliyetuumba kwani yeye ndiye taa na nuru yetu wakati wote,anayajua mapito yetu lakini pia anaijua kesho yetu.Yeye ndiye aliyetuwezesha kama angetuhukumu kama baadhi yenu hapa basi alikuwa na uwezo wakuzuia kila kitu kisiwezekane.Najua jambo moja tu Njia zake siyo kama za mwanadamu.Mungu awabariki.