Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,565
- 7,984
Dhana nzima ya mtu na akili zake "kuibiwa" ni tete, lakini kisheria Josephine hadi leo hii ni mke wa mtu mwengine, hilo lipo wazi
Sasa mwalimu, nataka tuzungumze hapa bila ushabiki ili kuelimishana na kusaidiana kwakuwa mambo haya yanatokea kila siku.
Ikiwa Josephine anatambua kwamba aliwahi kuolewa na mwanaume mwingine lakini kutokana na sababu ambazo sisi hatuzijui tukaja kumkuta anaishi na Dr. Slaa, kwanini lawama anabebeshwa mtu mmoja tu hapa? mbona hatujipi jukumu la kutaka kujua kilichomtoa kwa mahimbo ili tuwe fair kwa watu wote watatu?