Joti, "Awawezi kutushusha labda watoke na roho zetu mimi na Diamond "

Joti, "Awawezi kutushusha labda watoke na roho zetu mimi na Diamond "

Heheheeheh
View attachment 725986

Akiunga mkono kauli aliyotoa Diamond wakati anahojiwa na TimesFm.... Joti nae ameunga mkono msimamo wa Diamond wa kutokubali kubuluzwa na media.

Diamond kwa kujiamini alisema wakati wa kuwa watumwa wa media umepitwa na wakati na haitokaa itokee apotezwe na media.

Kwa taarifa tu ni kwamba media zilizofungia content za Diamond ndio pia zimefungia content za Joti kwa muda mrefu.
hehehhehe Jot mchekeshaji kama ujamuelewa ningumu.. Ongezea team Paka
 
Sasa kwa akili yako ni sawa kuangalia video ya yule binti aliye uchi? Suppose uko na wazazi wako, unaweza kuangalia hiyo video? Vitu vingine si vya kuiga jamani, tulinde tamaduni zetu.

Tulianza taratibu kuzoea kuwaona wanawake wakiwa wanacheza na vichupi tupu mbele ya wazazi wetu, na hawahawa BASATA walikuwepo na waliachia tu tuharibike.
Kama hatukuyaona haya katika nyimbo za watanzania, basi tuliyashuhudia katika nyimbo za nje ya Tanzania ambazo zilirushwa katika vituo vyetu Tanzania na BASATA wakiwa wasimamizi ila hawakuona.
Hawawezi kutukunja sasa hivi tukiwa tumeshakauka, watuache tu, mila zetu zimetushinda wacha ziende tu.
 
Hivi Joti ana content gani zaidi ya matangazo anayofanya? Hivi Clouds media na Ipp media wamefungia contents gani za Joti maana kwenye hili kwangu kama jipya vile
 
Sasa jiulize, kwa akili yako unafikiri Diamond yuko sawa? Nyimbo zake zimefungiwa kwa sababu hazing maadili, hata huko Marekani HAKUNA wimbo usio na maadili unapigwa redioni bila kuwa edited, yeye Diamond nani mpaka asifungiwe? Akiona vipi ahame tu nchi, tunataka wanamuziki wa kweli si wababaishaji.
Daah Ulivyokurupuka ka unajisaidia kichakani....relax
 
Hivi wewe ukiwa na wazazi wako hua unaangalia miziki ya kisasa mkuu?

Kwa hiyo miziki ya kisasa ni ya kukaa uchi? Msipende kuiga kila kitu, vingine si vya kuiga hata kidogo. Tamaduni yetu Afrika ni tofauti kabisa na Marekani au Ulaya.
 
Ninatumai unaweza kujicheka baada ya kurudia kusoma ulichoandika.!
yamkini Diamond hanisaidii mimi binafsi lakini ninapokuwa Nje ya Nchi hii huwa najisikia fahari sana Kusikia Nyimbo zake zikichezwa kwenye redio kadhaa za huko kila ukitune unasikia

" this is Diamond a musician from Tanzania"

huwa ninatembea kifua mbele na kuona fahari mimi kuwa mtanzania na hata kurudia kupiga mziki wake kwa sauti ya juu ndani ya gari niwapo Nje ya Nchi..hii ni zaidi ya zawadi kwangu ambayo yamkini hata mama yako mzazi asingeweza kufikiria kunizawadia.!

Diamond amewakilisha mziki wa Taifa hili mara nyingi wala sihitaji kukwambia mara ngapi lakini wajuzi walio humu waweza kukupa jibu likutoshalo
wala sihitaji kukueleza habari za kombe la dunia huko Russia.!

Je wewe na familia yako nzima mmeliwakilisha Taifa hili kwa jambo lipi?
by the way kilema mwenzangu wa fikra..
Diamond hanifahamu wala sidhani kama ana sabbu yoyote ya yeye kunifahamu lakini alifanyalo ana sapoti yangu ya kutosha.

Nakuuliza kwa mara ya pili, ni lini Diamond aliwakilisha taifa hili kimuziki? Sina sababu ya kuandika mapovu yasiyo na msingi kama wewe kwani unaonyesha ni mtu wa namna gani na siku zote mtu asiyejitambua anakuwa mgumu kuelewa hata a simple question because akili yake imeganda kwa kitu akiaminiacho hata kama si cha uhakika/ukweli. Lini Diamond aliwakilisha hili taifa kimuziki nje?
 
Tulianza taratibu kuzoea kuwaona wanawake wakiwa wanacheza na vichupi tupu mbele ya wazazi wetu, na hawahawa BASATA walikuwepo na waliachia tu tuharibike.
Kama hatukuyaona haya katika nyimbo za watanzania, basi tuliyashuhudia katika nyimbo za nje ya Tanzania ambazo zilirushwa katika vituo vyetu Tanzania na BASATA wakiwa wasimamizi ila hawakuona.
Hawawezi kutukunja sasa hivi tukiwa tumeshakauka, watuache tu, mila zetu zimetushinda wacha ziende tu.

Haya yalizoeleka toka kwa tawala zilizopita za Marais fake kina Mkapa na Kikwete....wale hawakupaswa kuwa Marais hata kidogo kwani walifanya yale kimakusudi tu. Walitaka wananchi wajikite kwenye ujinga huku wao na familia zao wakijinufaisha na rasilimali za nchi yetu na kusingizia kuwa nchi ni ya kimasikini. Tactics hizi alikuwa anatumia sana Mobutu kule Zaire enzi zile, akihisi wananchi wana huzuni anawajengea kumbi mpya za starehe ili wasahau naye akiwahibia na kujitajirisha kinoma.
 
Nakuuliza kwa mara ya pili, ni lini Diamond aliwakilisha taifa hili kimuziki? Sina sababu ya kuandika mapovu yasiyo na msingi kama wewe kwani unaonyesha ni mtu wa namna gani na siku zote mtu asiyejitambua anakuwa mgumu kuelewa hata a simple question because akili yake imeganda kwa kitu akiaminiacho hata kama si cha uhakika/ukweli. Lini Diamond aliwakilisha hili taifa kimuziki nje?

Naomba kuuliza hapa mkuu kama hutajali!
Kama msanii/mwanamuziki akiitwa ama niseme akienda kutumbuiza kwenye michuano ya kombe la mataifa huru ya Afrika, hapa anaenda yeye kama yeye ama itaandikwa mwanamuziki fulani kutoka nchi fulani?
Maana kama itaandikwa ni msanii fulani kutoka nchi fulani hapo ni wazi kabisa kawawakilisha wanamuziki wengine kutoka hiyo nchi fulani. Na kama anaenda yeye kama yeye, huu utaratibu wa mwanamuziki husika kukabidhiwa bendera ya nchi yake husika unatoka wapi?
Samahani nimekukoti.
 
Kwa hiyo miziki ya kisasa ni ya kukaa uchi? Msipende kuiga kila kitu, vingine si vya kuiga hata kidogo. Tamaduni yetu Afrika ni tofauti kabisa na Marekani au Ulaya.
Ushawahi kuona ngoma za asili jinsi zilivyo mkuu?
 
Sasa jiulize, kwa akili yako unafikiri Diamond yuko sawa? Nyimbo zake zimefungiwa kwa sababu hazing maadili, hata huko Marekani HAKUNA wimbo usio na maadili unapigwa redioni bila kuwa edited, yeye Diamond nani mpaka asifungiwe? Akiona vipi ahame tu nchi, tunataka wanamuziki wa kweli si wababaishaji.
Mkuu sory naomba mfano wa nyimbo iliyofungiwa marekan _?..
 
Maadili ya mtanzania ni yapi ?
 
Kingereza hiki!!!!!
Mbona Mimi nakiona kipo sawa kabisa mkuu ,,,

Au macho yangu na obulongata yangu ya ile shule ambayo inayotumia rim la gari kam kengele ndo walinifunza vibaya nn?
 
Mkuu sory naomba mfano wa nyimbo iliyofungiwa marekan _?..

Hivi unaelewa unaandika nini au ni katika ile hali ya ubishi usio na tija? Sijakuambia ama kuandika popote pale kuwa wimbo wa msanii fulani umefungiwa Marekani, nilichosema ni kwamba nyimbo za matusi za wasanii wa Marekani hazipigwi redioni huko Marekani bila kuwa edited ila hapa Bongo zinapigwa hivyo hivyo huku dj na mtangazaji wanachekelea. Kumbuka kuwa wasanii wa Marekani wanapotoa wimbo ama nyimbo katika CD zao kuna zile radio version ambazo zimechujwa kuendana na maadili na Club version za matusi ambazo hazipigwi redioni ila hapa Bongo tunazipiga wakati wamarekani wenyewe hawazipigi, sasa kama huu si ujinga ni nini?
 
Back
Top Bottom