Joto kali duniani linathibitisha kuwa ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika kwenye mambo ya tabia nchi ni sahihi

Joto kali duniani linathibitisha kuwa ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika kwenye mambo ya tabia nchi ni sahihi

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG111446670119.jpg


Mwezi Julai mwaka huu unatajwa na wanasayansi kwa tabia nchi kuwa ni kipindi ambacho dunia imeshuhudia viwango vikubwa sana vya joto katika historia. Hali hii imefanya baadhi ya wanasayansi waliokuwa wanasita kukiri kwa uwepo wa mabadiliko ya tabia nchi duniani warudi nyuma, na wale waliokuwa wanafanya mzaha kwenye suala hili kuanza kuchukua hatua za kujiangalia na kubadilisha mwenendo wao.



Marekani ni moja ya nchi ambazo zina wanasayansi wengi wanaopinga suala la mabadiliko ya tabia nchi duniani. Baadhi ya wanasiasa wa nchi hiyo wamewahi hata kufikia hatua ya kuitoa Marekani kwenye mkataba wa Paris kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, wakidai kuwa suala hilo halina ukweli wowote na ni mbinu ya wanasiasa wa mrengo wa kushoto kukwamisha maendeleo ya sekta ya nishati ya visukuku.



Lakini joto kali la hivi karibuni limeifanya serikali ya Marekani kushtuka, na sehemu ya kwanza ilipokimbilia kutafuta jibu la kukabiliana na changamoto hii ni Beijing. Serikali ya Marekani ilimtuma mjumbe wake Bw. John Kerry kuja kufanya mazungumzo na serikali ya China kuhusu suala la mabadiliko ya tabia nchi. Hii ni hatua nzuri inayoonesha kuwa Marekani imeamua kurudisha busara zake.



Hata hivyo kuna kitu ambacho Bw. Kerry na wenzake wanasahau, nacho ni kuwa China imekuwa inafanya juhudi endelevu kwenye suala la mabadiliko ya tabia nchi, na imekuwa ikifanya juhudi hizi ndani na nje ya China. Kwa wanaofuatilia mchango wa China kwenye suala la mabadiliko ya tabia nchi, watakuwa wanajua kuwa China imefanya juhudi za miongo kadhaa kuongeza eneo lake la misitu, imejenga ukanda mkubwa sana wa kuzuia kuenea kwa jangwa, na hata kurudisha ardhi iliyokuwa jangwa kwa matumizi ya kilimo.


Katika siku za hivi karibuni China imekuwa mstari wa mbele katika kubadilisha muundo wake wa matumizi ya nishati, na sasa matumizi ya nishati jadidifu nchini China yanakaribia kuwa sawa na ya nishati ya visukuku. Kwa sasa ni jambo la kawaida kuona matumizi ya magari yanayotumia betri, au kutumia umeme unaozalishwa kwa nishati ya maji, upepo, jua na joto la ardhini nchini China.



Lakini juhudi za China hazijaishia ndani ya China. Kwa sasa ushirikiano kati ya China na nchi mbalimbali duniani, na hasa za Afrika kwenye sekta ya nishati safi umekuwa ukiimarika. Miradi ya kuzalisha umeme kwa nishati endelevu barani Afrika kama vile jua, maji na upepo imekuwa ikijengwa na makampuni ya China. Kumekuwa na dalili ya kuanza kwa matumizi ya magari yanayotumia nishati mpya kutokana na teknolojia zinazoingizwa kutoka China.



Mbali na hayo, kumekuwa na miradi mbalimbali inayohusu sekta zinazohusiana na mabadiliko ya tabia nchi. Kwa mfano wanasayansi wa Kenya, Ethiopia na Nigeria wamekuwa wakishirikiana na wenzao wa China kujifunza mafanikio ya China katika kupambana na Jangwa la Taklimakan mkoani Xinjiang, eneo kubwa zaidi la ukame nchini China. Wanatumia uzoefu wa China kukabiliana na jangwa katika nchi zao. Kumekuwa na Kituo cha Utafiti wa Pamoja cha Sino-Afrika (SAJOREC) katika Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta kinachofadhiliwa na China, ambacho imefanya programu 45 za utafiti wa pamoja hasa zinazolenga kukabiliana na ukame.



Pamoja na kuwa ni jambo zuri kwa Marekani kuanza kukubali ukweli, na ziara ya Bw. Kerry nchini China ni jambo la kukaribishwa, ni bora kama Marekani itafuata mtindo wa China wa kuwa juhudi endelevu zenye ufanisi za ndani ya nchi na nje ya nchi, na sio kuwa kigeugeu kutegemea nani yuko madarakani.
 
Back
Top Bottom