Joyce Kiria: Ni aibu kubwa, kijijini alikozaliwa Kikwete aolewa mtoto mwenye miaka 8!

Joyce Kiria: Ni aibu kubwa, kijijini alikozaliwa Kikwete aolewa mtoto mwenye miaka 8!

Makala Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2011
Posts
3,395
Reaction score
1,112
Alipozungumza na Zembwela wa East Africa Radio katika kipindi cha Super Mix, Mwanadada na mwanaharakati wa haki za wanawake anayetumia kipindi cha runinga almaarufu WANAWAKE LIVE,

Bi.Joyce Kiria ametambulisha ujio mpya wa kipindi chake kwa kuwagusa wanawake vijijini. Bi.Joyce Kiria amesema, "kuna matatizo mengi yanayowakumba wanawake vijijini kama kupigwa,kunyanyaswa kijinsia,kunyimwa haki ya kumiliki mali pamoja na ukatili.Mfano Dodoma, siwataji vibaya wagogo, lakini ukiukwaji wa haki za wanawake umekuwa mkubwa kiasi kwamba kuna Mwanamke amekatwa mkono na Mumewe kisa wivu eti Mume aliikuta alama ya mguu wa mtu aliyepita nje kwake,(Zembwela alidakia) kwani lazima mtu akipita kwako amtake mkeo?"

Kwa upande mwingine Bi.Joyce Kiria amesema anasikitishwa na namna Mhe.Rais Jakaya Kikwete alivyokusahau kijijini kwao haswa kwa kutokuimarisha huduma muhimu kama maji.Nje ya hayo ni mtoto wa umri wa miaka 8 kuozeshwa Bagamoyo...Zaidi fuatilia kipindi leo saa 21:00 EATV! kufuatilia visa hivi na mijadala isiyopewa nafasi
 
Mambo mengine jamani yananichanganya kidogo,

kwani ameambiwa kuwa jakaya ndiye aliyemwoa huyo mtoto;

na kwa nini aanze na jakaya wakati wapo watendaji wa chini ambao
wako karibu sana na wananchi kuliko jakaya ambaye
ni mtumishi wa watanzania wote;
chama nisaidie hapa
 
Last edited by a moderator:
Alipozungumza na Zembwela wa East Africa Radio katika kipindi cha Super Mix, Mwanadada na mwanaharakati wa haki za wanawake anayetumia kipindi cha runinga almaarufu WANAWAKE LIVE, Bi.Joyce Kiria ametambulisha ujio mpya wa kipindi chake kwa kuwagusa wanawake vijijini. Bi.Joyce Kiria amesema, "kuna matatizo mengi yanayowakumba wanawake vijijini kama kupigwa,kunyanyaswa kijinsia,kunyimwa haki ya kumiliki mali pamoja na ukatili.Mfano Dodoma, siwataji vibaya wagogo, lakini ukiukwaji wa haki za wanawake umekuwa mkubwa kiasi kwamba kuna Mwanamke amekatwa mkono na Mumewe kisa wivu eti Mume aliikuta alama ya mguu wa mtu aliyepita nje kwake,(Zembwela alidakia) kwani lazima mtu akipita kwako amtake mkeo?" Kwa upande mwingine Bi.Joyce Kiria amesema anasikitishwa na namna Mhe.Rais Jakaya Kikwete alivyokusahau kijijini kwao haswa kwa kutokuimarisha huduma muhimu kama maji.Nje ya hayo ni mtoto wa umri wa miaka 8 kuozeshwa Bagamoyo...Zaidi fuatilia kipindi leo saa 21:00 EATV! kufuatilia visa hivi na mijadala isiyopewa nafasi

Tunakisubiri kipindi kwa hamu sana, Tunajua shemeji yetu hatatuangusha kwa kuonyesha uhalisia wa maisha wanayopitia wanawake watz. Namkubali sana Joyce ni mwanamke aliyeonyesha ujasiri wa hali ya juu mumewe alipopatwa na matatizo na akafanya jambo ambalo wanawake wengi wa wanaharakati duniani hawajawahi kulifanya zaidi ya kusifiwa kuwa wa jasiri na wavumilivu, Kitendo cha joyce kuandamana na wanawe na kutokujifungia ndani kulia ule ulikuwa ujumbe tosha jinsi familia hii ilivyojengwa kwa uimara. Joyce ipo siku ataingia kwenye vitabu vitakavyo mtambulisha duniani kote bila hata yeye mwenyewe kujua alichokifanya kilikuwa kitu kikubwa sana, Ile aangalie Watu wasije anzakuanza kumtumia vibaya kwa kutaka kumdhoofisha mumewe maana watawala wabovu duniani hufanya hivyo.. Joyce kama ni mwanachama wetu wa Jf endelea kuwa imara na usiwe na hofu kama ambavyo hukuionyesha hofu mumeo alivyokuwa amekamatwa.
 
Mambo mengine jamani yananichanganya kidogo,

kwani ameambiwa kuwa jakaya ndiye aliyemwoa huyo mtoto;

na kwa nini aanze na jakaya wakati wapo watendaji wa chini ambao
wako karibu sana na wananchi kuliko jakaya ambaye
ni mtumishi wa watanzania wote;
chama nisaidie hapa

Kumbuka lile jimbo Rais wenu ameshawahi kuwa mbunge wa pale akiwa waziri wa mambo ya nje.. wewe haraka yako ni ya nini? subiri uone hali halisi.
 
Mamndenyi; Kijiji alichozaliwa Rais kinatakiwa kutunzwa ili kuvipa msukumo wa ustawi vijiji vingine.Mama Salma Kikwete anayo NGO inayoshughulikia namna ya kumkomboa Mwanamke hivyo, "CHARITY BEGINS AT HOME". Anakumbushwa kwa lengo zuri na hili halishangazi.Hata Kenya, kijiji alichozaliwa Obama kimepewa hadhi yake.Pia ni aibu kwa wananchi wa Msoga kunywa maji machafu yanayopatikana kwa shida wakati mabomba yanatandazwa kupita Bagamoyo kuelekea Dar es salaam.
 
Last edited by a moderator:
sipendi kabisa mwanamke aolewe na mtu anayemwagia watu tindikali halafu hasemi ili huyo mtu achukiliwe hatua
 
nalaani sana wanawake wanaficha taarifa za waovu wanaomwagia watu tindikali
 
Nyanidume; Mbona mnakurupuka wakati masuala haya lengo lake ni zuri tu.Kwani ukienda kijijini Msoga kuna maji safi? Mbona kijiji alichozaliwa Mhe.Mkapa almaarufu Lupaso hakuna ndoa za utotoni kwa kiwango kikubwa kama Bagamoyo? Sasa wewe unachokipinga ni kipi kisicho cha kweli?
 
Last edited by a moderator:
habariyamujini; Rudi kwenye mada wewe, kitendo cha Mwenyekiti wa CCM kushindwa kukifanya mfano wa kuigwa kijiji/jimbo lake ni aibu kubwa!
 
Last edited by a moderator:
kipindi kinaitwa Wanawake live, mimi ni mwanaume, hakinihusu
 
Back
Top Bottom