Makala Jr
JF-Expert Member
- Aug 25, 2011
- 3,395
- 1,112
Alipozungumza na Zembwela wa East Africa Radio katika kipindi cha Super Mix, Mwanadada na mwanaharakati wa haki za wanawake anayetumia kipindi cha runinga almaarufu WANAWAKE LIVE,
Bi.Joyce Kiria ametambulisha ujio mpya wa kipindi chake kwa kuwagusa wanawake vijijini. Bi.Joyce Kiria amesema, "kuna matatizo mengi yanayowakumba wanawake vijijini kama kupigwa,kunyanyaswa kijinsia,kunyimwa haki ya kumiliki mali pamoja na ukatili.Mfano Dodoma, siwataji vibaya wagogo, lakini ukiukwaji wa haki za wanawake umekuwa mkubwa kiasi kwamba kuna Mwanamke amekatwa mkono na Mumewe kisa wivu eti Mume aliikuta alama ya mguu wa mtu aliyepita nje kwake,(Zembwela alidakia) kwani lazima mtu akipita kwako amtake mkeo?"
Kwa upande mwingine Bi.Joyce Kiria amesema anasikitishwa na namna Mhe.Rais Jakaya Kikwete alivyokusahau kijijini kwao haswa kwa kutokuimarisha huduma muhimu kama maji.Nje ya hayo ni mtoto wa umri wa miaka 8 kuozeshwa Bagamoyo...Zaidi fuatilia kipindi leo saa 21:00 EATV! kufuatilia visa hivi na mijadala isiyopewa nafasi