Uchaguzi 2020 JPM kwenye mabango, Tundu Lissu kwenye mioyo ya watu

Uchaguzi 2020 JPM kwenye mabango, Tundu Lissu kwenye mioyo ya watu

TWisheshagi

Member
Joined
May 2, 2020
Posts
14
Reaction score
209
MAKALA hii nimeanza kuandika jana, nikiwa kwenye jukwaa la CCM, mjini Musoma.

Mengi nimeyashuhudia kwa macho yangu, lakini kwa nafasi yangu hususan kwenye timu ya kampeni ya mgombea wetu nitajadili machache:

Nimeshuhudia baadhi ya watu muhimu kwenye timu yetu wakifuatilia hotuba za Lissu kwa siri katikati ya Hotuba ya mgombea wetu!

Yaani, hatumsikilizi mgombea wetu, tuna msikiliza Lissu! Mgombea wetu amebakia kwenye mabago nchi nzima huku Lissu akitawala kwenye MIOYO ya watu!

Aliposimama "Mama wa TAIFA" Mama Maria Nyerere, kuongea ndani ya dakika moja, tayari alianza kuumbua watu kabla ya kumaliza hotuba yake fupi yenye masimango ndani yake!

Hotuba fupi ya Mama Nyerere, ili beba ujumbe mzito na muhimu kuliko hotuba za makada wengi wa CCM walio panda jukwani kuzungumza!

Wengi tulibaki vichwa chini baada ya Mama Maria Nyerere, kuzungumza!

Mama huyu amebakia na chembe chembe za ukweli kutoka kwa Marehemu Mume wake! Huwezi kupanga naye jambo la uongo, anaweza kukubalia mwanzoni na kisha kukana baadaye kwa staili ya aina yake! Hicho ndicho kilichotokea jana.

Kupanga jambo na watu wenye umri mkubwa unapaswa kuwa mwangalifu! Ukizoea ghiriba uwe makini, ukipenda uongo uwe mwangalifu!

Lipo jambo jingine linalojitokeza kwenye kampeni zetu! Mgombea wetu, pamoja na kupendelewa na vyombo vya habari vyote muhimu, bado hotuba zeke zinafuatiliwa na watu wachache sana, ukilinganisha na wale wanavyofuatilia hotuba za Lisu kwenye mtandao ya kijamii! Ipo haja ya kujipanga upya!

Jambo jingine tumeanza kujibu Lissu, badala ya kueleza sera zetu, na mambo mengi mazuri tuliyofanya! Tumesahau sisi ndiyo wenye serikali. Tuliaminiwa kukusanya kodi za Watanzania kwa miaka mitano. Wajibu wetu ni kueleza utekelezaji zaidi kuliko kuahidi jambo jingine jipya wakati kuna mengi hatujatimiza!

Tunasikiliza Lisu, kasema kitu gani ili kesho yake tujibu! tena kwa vijembe!

Tumekosa kumbukumbu kabisa! tulichokesema jana tunakikataa leo, na tunachosema leo tunakipinga kesho asubuhi!

Ushauri wangu: Naomba kutoa ushauri ambao hauwezi kukubalika! Tunahitaji kuongezewa nguvu ya timu ya kampeni. Tupunguze watu wenye blabla tuite watu wenye uwezo wa kumsaidia mgombea wetu!

Wasanii wanapoteza muda mwingi, tunashindwa hata kuwanadi wagombea ubunge na udiwani vizuri. Jana tumeacha malalamiko mengi Musoma.

Kuna baadhi ya wagombea ubunge hata sisi wenyewe tulioko kwenye timu ya kampeni hatuwajui!

Pili, tumuombe Mzee Kinana ATUSAIDIE! Mipango mingi ya Dkt. BASHIRU imefeli kabla ya utekelezaji. Ni yeye aliyetutangazia kuwa hakutakuwa na wasanii badala yake bendi ya Chama itatumika kutumbuiza. Hilo limeshindikana kabla halijaanza kutekelezwa!

Mzee Kikwete, toka kwenye mashamba ya mananasi Msoga, njoo kwenye kampeni ili ukoe jahazi! Ushawishi wako kwa umma ni muhimu sana kuliko porojo na kelele za Humphrey Polepole!

Ndimi mkulima wa bamia, bonde la mto Simiyu Magu-MWanza. Safarini CCM KIRUMBA
 
MAKALA hii nimeanza kuandika jana, nikiwa kwenye jukwaa la CCM, mjini Musoma.

Mengi nimeyashuhudia kwa macho yangu, lakini kwa nafasi yangu hususan kwenye timu ya kampeni ya mgombea wetu nitajadili machache:..
Magufuli , Polepole na Bashiru Sio wanasiasa. Waombe masada kwa Nape, Kinana, Mzee Makamba na JK haraka, hawa ndio wanasiasa wabobezi.
 
CCM inapaswa kujitafakari zaidi. Wanatumia mda mwingi kuuza sera za Chadema kwa vijembe visivokuwa na msingi huku wakisahau kunadi ilani yao

Kosa jingine kubwa walilolifanya ni kuamini kwa 100% kuwa kufikia mwaka huu upinzani ungekufa kwa sababu hawakupata platform ya kuzungumza kwa miaka mitano. Mapokezi ya watanzania kwa CDM yamewachanganya na ndo maana wamebakia kujibu hoja za Lisu.

Mwisho; Bashiru abadili strategy za kampeni kabla Jua halijazama.
 
Magufuli , pole pole na bashiru Sio wanasiasa. Waombe masada kwa nape,kinana,mzee Makamba na JK haraka,Hawa ndio wanasiasa wabobezi.

Umesahau Yale Mambo yaliyodukuliwa na wengine kuomba msamaha?

Wengi Kama Kinana wakiingia ulingoni hapo wapinzani wataanza kufukua makaburi ya mmoja hd mwingine.. matokeo yake sera ya ufisadi itatamalaki...
 
MAKALA hii nimeanza kuandika jana, nikiwa kwenye jukwaa la CCM, mjini Musoma.

Mengi nimeyashuhudia kwa macho yangu, lakini kwa nafasi yangu hususan kwenye timu ya kampeni ya mgombea wetu nitajadili machache:..
Kupanga jambo na watu wenye umri mkubwa unapaswa kuwa mwangalifu! Ukizoea ghiriba uwe makini, ukipenda uongo uwe mwangalifu
 
Mmekula ruzuku hadi mmeshindwa kuweka mabango
Kuna bango moja la mgombea wa kiti cha Urais, Mh. Magufuli linasema eti Magufuli ni mnyenyekevu!

Nilipoliona bango hili, nikashtuka sana. Nikajiuliza maswali mengi:

1) Ni Magufuli mwenyewe amehiari kuwepo kwa bango la namna hiyo?

2) Kuna watu fulani wameamua kutengeneza bango hilo, labda kwa kumdhihaki Magufuli?

3) Au Magufuli amewaeleza kuwa endapo akichaguliwa safari hii anataka awe mnyenyekevu?

Kuwa 'mnyenyekevu' au kwa kiingereza kuwa 'humble', tafsi yake:

Unyekenyekevu hutokana na neno kunyenyekea. Anayenyenyekea huitwa mnyenyekevu. Kama Magufuli ni mnyenyekevu, ni lazima tujiulize, huwa anamnyenyekea nani?

Kunyenyekea ni kujishusha. Kunyenyekea ni kuamini wewe si kitu mbele ya yule unayemnyenyekea. Kunyenyekea ni kuonesha kuwa ama wewe ni duni mbele ya yule unayemnyenyekea au zaidi ni kuwa upo sawa na yule unayemnyenyekea.

Kunyenyekea maana yake ni kuwa msikivu. Kunyenyekea ni kuwa tayari kupokea ushauri, maelekezo na matakwa ya unaowanyenyekea.

Sasa tujiulize, hivi kweli Rais Magufuli anazo hizi sifa? Bila ya kutafuta majibu toka kwa watu wengine, nina hakika Magufuli hatakuwa amependezwa na bango linalosema yeye ni mnyenyekevu maana mara kadhaa kwa kauli yake na kwa matendo yake amekataa kabisa kuitwa "mnyenyekevu".

Rais Magufuli amewahi kutamka yafuatayo:

1) Mimi sibadilishwi na yeyote, mimi jiwe. Maana yake yeye hapokei ushauri wala maelekezo kutoka kwa yeyote

2) Mimi ukinishauri, ndiyo umeharibu kabisa, maana sitafanya unachonishauri

3) Wewe Mpina ni kichaa mwenzangu, endelea hivyo hivyo

Mtu mnyenyekevu, ni mtu mwenye huruma, kwa sababu anaamini kuwa wale anaowanyenyekea wanastahili kuthaminiwa na kuheshimiwa utu wao.
Mara kadhaa Rais Magufuli amefisha utu wa watu wengine na kuwaonesha kuwa ni takataka mbele yake. Baadhi ya kauli na matendo yake:

1) Huyu Kabudi na Mpango, hawawaambii tu, nilikwishawaambia ni mapumbavu mara nyingi tu

2) Huko Marekani ulikokuwa ulikiwa unafanya upumbavu huu (aliambiwa mkurugenzi wa halmashauri ya Tunduru)

3) Kuna watu walikuwa wanaishi kama malaika, nitahakikisha wataishi kama mashetani (anapenda watu wateseke. Wala hakusema kuwa kuna watu wanaishi kama mashetani, nataka nao waishi kama malaika. Yeye anapenda watu wapate taabu)

4) Kwenye utawala wangu, tajiri anaweza kufanywa chochote wakati wowote (maana yake anaweza kumwonea mtu kwa sababu tu ni tajiri. Yaani kuonesha kuwa yeye ni bora kuliko watu wote kiasi cha kuweza kumfanya mtu chochote bila ya kujali mtu huyo ana kosa au hana kosa)

5) Wa Mwanza msiwabomolee nyumba zao kwa sababu walinipa kura nyingi (kama hukumpa kura, ina maana ni halali kubomolewa nyumba yako. Haamini kuwa kuna mtu mwingine yeyote mwenye haki sawa na ya kwake ya kuweza kupigiwa kura)

6) Kamdai maji mbunge wako uliyemchagua au mume wako (alitamka Tunduma dhidi ya mama aliyemwambia wana tatizo la maji)

7) Ninyi mlichagua mbunge mpinzani ndiyo maana siwezi kuleta maendeleo (aliwaambia wananchi wa kule Lindi)

8) Tetemeko halikuletwa na Serikali wala CCM. Hakuna serikali inayowajengea nyumba wahanga wa matetemeko (aliwaambia wahanga wa tetemeko la ardhi)

9) Serikali haina shamba (aliwaambia wananchi waliomba chakula baada ya mazao yao kufa kwa ukame)

Magufuli anaamini kuwa wananchi wengine ni duni kuliko yeye, hawastahili kuwa viongozi, bali yeye na wale tu ambao yeye anawataka.

Ukimtazama Magufuli, matendo yake na kauli zake, bila ya ushabiki, ungeweza kumtafsiri kwa majumuisho yafuatayo:

1) Ni kiongozi mbabe
2) Ni kiongozi mwenye majivuno
3) Ni kiongozi mbaguzi
4) Ni kiongozi anayejiamini kupita kiasi
5) Ni kiongozi mwenye dharau
6) Ni kiongozi asiyependa kusikiliza, kuelekezwa wala kushauriwa
7) Ni kiongozi asiye na huruma
8) Ni kiongozi asiyejali

Na kila moja katika hizi sifa 7, kuna au kauli au matendo yanayotoa uthibitisho. Anaweza kuwa na tabia nyingine pia lakini kunaweza kusiwepo na uthibitisho wa moja kwa moja.

Swali langu, hivi kusema Rais Magufuli ni "mnyenyekevu", walioandaa bango hili, wanamdhihaki, wanawadanganya wananchi, au limewekwa kwa lengo gani? Maana Rais Magufuli, kwa hakika ni kinyume kabisa cha Unyenyekevu, na wala hata yeye haipendi hiyo tabia ya unyenyekevu. Watanzania tuache unafiki, tumwelezee mtu katika uhalisia wake.
[9/6, 09:25] Kurwa: SISI SIO WAJINGA
Ulipochukua tu madaraka ukaanza na kubomoa nyumba zetu katika bonde la Msimbazi. Bila huruma ukatuacha tumelala nje na watoto wetu. Ulidhani tutahama mjini lakini sisi bado tupo.

SISI SIO WAJINGA
Ulipokuwa unapanua barabara ya Ubungo - Kibaha ukabomoa nyumba zetu. Mbunge wetu Mnyika aliomba utulipe fidia ukampinga mbele yetu. Lengo lako tufe masikini lakini kwetu sisi maisha yanaendelea.

SISI SIO WAJINGA
Hukutaka tuwaone wawakirishi wetu, wakiwakirisha matatizo yetu Bungeni. Ulisema gharama za kurusha matangazo Live ni kubwa. Lakini leo hii unatuomba tufungue TBC tukuangalie ukikata mitaa kuomba kura.

SISI SIO WAJINGA
Baada ya kuwa tumefanya kazi kwa miaka 40 na tumebakiza miezi 3 tustaafu ukatufukuza kazi kwa kisingizio cha vyeti feki. Ulidhani tutakufa kwa njaa lakini Mungu anatupigani bado tunaishi.

SISI SIO WAJINGA
Tulipopata tetemeko la ardhi Watanzania wenzetu walituchangia pesa nyingi lakini wajanja wakatafuna. Ulipokuja Bukoba tulidhani utatutetea wanyonge badala yake ukatusimanga na kutukumbusha majanga ya Ukimwi, MV Bukoba kwamba yote yanatupiga sisi. Sasa nasikia unakuja kuomba kura kwetu! Je, ni kweli wewe utakanyaga Bukoba?

SISI SIO WAJINGA
Tulipokuwa tuna njaa. Njaa iliyotokana na ukame. Tukakuomba msahada wa chakula. Hii sio kwako tu, hata Serikali zilizopita zilitusaidia tulipokumbwa na ukame. Lakini ulitujibu kwa kejeli na kiburi cha hali ya juu. Eti tusikuombe chakula, Serikali haina shamba. Leo hii unakuja tena kuomba kura?

SISI SIO WAJINGA
Tukaenda Mtwara kulima korosho. Ukatuma askari wako wakatunyang'anya korosho halafu wakadai tuwaonyeshe mashamba yetu. Mbona wanaolima Mahindi, Pamba, Mpunga, n.k. hamuwaulizi mashamba yao? Ukasema hao askari watabangua korosho kwa meno ili kila Mtanzania atapata kilo 2, lakini hatujapata mgao. Sasa nasikia unakuja kuomba kura! Labda uishie Nangurukuru kwa sababu.

SISI SIO WAJINGA
Tumeitumikia nchi yetu kwa bidii kubwa. Tumefanya kazi kwa uzalendo mkubwa, huku tukipokea mishahara kidogo. Leo hii tumestaafu, tupo nyumbani miaka ikikatika. Lakini hutaki kutulipa mafao yetu. Bila aibu unakuja kutuomba kura tena?

#SISI_SIO_WAJINGA.
 
1599374922913.png
 
MAKALA hii nimeanza kuandika jana, nikiwa kwenye jukwaa la CCM, mjini Musoma.

Mengi nimeyashuhudia kwa macho yangu, lakini kwa nafasi yangu hususan kwenye timu ya kampeni ya mgombea wetu nitajadili machache:...
Tindu Lissu ni Rais wa mitandao. Magufuli ni Rais wa Watanzania.
 
MAKALA hii nimeanza kuandika jana, nikiwa kwenye jukwaa la CCM, mjini Musoma.

Mengi nimeyashuhudia kwa macho yangu, lakini kwa nafasi yangu hususan kwenye timu ya kampeni ya mgombea wetu nitajadili machache:..
Upo kwenye timu ya kampeni kama unavyodai, kwa nini usiwaambie huko sasa unatueleza sisi wa nje ili tukusaidie nini?

Kama vp hamia kwa lissu ili usiteseke
 
Tundu Lissu yupo kwenye mioyo ya wajinga wasiolithamini taifa lao.
 
MAKALA hii nimeanza kuandika jana, nikiwa kwenye jukwaa la CCM, mjini Musoma...

Wasanii wanapoteza muda mwingi, tunashindwa hata kuwanadi wagombea ubunge na udiwani vizuri. Jana tumeacha malalamiko mengi Musoma...

Hii ingeandikwa na vijana wa ACT ingeonekana propaganda... Ukweli ndio huo.

Safi Sana mtoa mada... Kichwa Cha habari Ni fikirishi Sana...
 
Nimeshangaa sana kusikia eti Bashiru Alli alikua mwalimu wa siasa UDSM
Ndio ilivyo, huyu aliingia UD Mwaka 2008, Mlugaluga na mapekosi yake!

Wakati huo kulikuwa na jotojoto la Siasa, jamaa akawa mchanguaji/mwanaharakati akijiita RAIS WA OFFCAMPUS!
Kumbe........!
 
Magufuli , Polepole na Bashiru Sio wanasiasa. Waombe masada kwa Nape, Kinana, Mzee Makamba na JK haraka, hawa ndio wanasiasa wabobezi.
nakubali sana vichwa hivi sana , katika mashambulizi , ila wajipange , maana mambo yamearibika sana na mbaya zaidi pale mgombea wao anapobaki na misimamo yake ile ile , anazidi kujibomolea nyumba yake mwenyewe, watanzania sio wajinga
 
Upo kwenye timu ya kampeni kama unavyodai, kwa nini usiwaambie huko sasa unatueleza sisi wa nje ili tukusaidie nini?

Kama vp hamia kwa lissu ili usiteseke

Ukweli mchungu... Rudia Kusoma Tena labda haujaelewa..
 
Back
Top Bottom