Jua chanzo cha neno banana republic lilipotokea

Jua chanzo cha neno banana republic lilipotokea

Dennis Robert Shughuru

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2024
Posts
5,559
Reaction score
8,747
Ndizi mbivu kila mtu anazijua ziko za aina nyingi sana huko sokoni

Miaka 400+ ukoloni ulianza kukua na wakoloni walizunguka dunian kwa nia ya kuijua dunia, wareno moja ya wakoloni walipita afrika wakaja East afrika na waliacha ngome yao Fort Jesus na hawakuishia East afrika bali walienda mbali zaidi mpaka Asia ya kusini na kule walichukua bidhaa nyingi mojawapo ni ndizi

Wareno walichukua ndizi na kuipeleka Americas na moja ya eneo walipopeleka ni Jamaica, kule Jamaica ndizi ilikubali sana kuna mvuvi wa marekani aliitwa lorenzo Dow Baker alienda Jamaica na alivyoona ndizi ya kuiva akaona fedha na utajiri akaanza kuichukua ndizi mbivu Jamaica na kwenda kuiza marekani na biashara ikawa inaenda vizuri

Mwisho mwa miaka 1890's kulikuwa na trade fair kulikuwa bidhaa nyingi na mojawapo ni ndizi mbivu na huko kwenye trade fair ndizi mbivu ilipendwa sana na ikawa maarufu na tokea pale ndizi mbivu ikawa maarufu sana

Biashara ya ndizi ilishamiri sana mpaka new York City kukaanzishwa banana Dock na kila kona ya jiji kulikuwa na maganda ya ndizi watu wametupa juu ya paving watu wakawa wanaanguka wakikanyaga na ikapelekea mkuu wa polisi wa new York City Theodore Roosevelt ambaye baadae atakuwa Rais kuanzisha faini na hata kifungo kwa atakayetupa maganda ya ndizi mbivu hovyo

BANANA REPUBLIC ILIPOANZIA
Wafanyabiashara wa ndizi wa-kimarekani walitaka kucontrol supply chain yote ya banana na eneo ambalo walilichagua ni central America kuanzia Colombia mpaka hondurus sababu lina climate kama ya equator na walianzisha kampui iliyoitwa United fruit company
Kucontrol supply chain walimaanisha
Kumanage watu
Kumiliko reli na barabara za kutoka kwenye mashamba
Kumanage bandari na waterways
Kumanage maduka ya watu wanaonunulia vitu
Kutokulipa kodi yeyote ile baada ya uwekezaji

Walianza na Guatemala wakajikuta wanamiliki mashamba, miundombinu na baadae mpaka shirika la posta, na baadae wakaamia kwenye nchi nyingine kama Honduras na Colombia walikuwa hawalipi wafanyakazi mishahara bali vocha ambazo wanaenda kwenye maduka ya united fruit company walioanzisha na yalikuwa na mahitaji mbalimbali

United fruit company ikawa ni kama serikali ndani ya serikali wakawa na nguvu sana kwenye nchi za Central america

Mwaka 1911 Honduras walipata Rais na akawaambia United fruit company tumechoka na inatosha tuachieni nchi yetu na ardhi hii ya kilimo cha ndizi watapewa watu wa hali ya chini, United fruit company hawakupenda wakaenda kulalamika kwa serikali ya marekani na serikali ya marekani ikawapa support na wakaenda muondoa rais wa Honduras na kumuweka kibaraka wao atakayelinda maslai yao tunaona sasa marekani inaanza-behave kama empire

Mwaka 1920 wafanyakazi wa United fruit company wa nchini Colombia waliandamana hawakutaka kulipwa kwa vocha, na walitaka siku za kazi ziwe sita na sio saba na kutaka mazingira ya kazi yawe mazuri- kama kawaida United fruit company walienda kulalamika kwenye serikali ya marekani na serikali ya marekani wakapeleka wanajeshi kwenye ufukwe wa Colombia, na baadae serikali ya Colombia kwa kuogopa serikali ya marekani iliwavamia wale waandamanaji waliokuwa wanataka mabadiliko baadhi iliwaumiza, wengine kuuwawa, na wengine walifungwa kwa kudai haki yao

Mwaka 1950 serikali ya Honduras walipinga manyanyaso ya United fruit company na kuwataka waondoke kama kawaida yao United fruit company walitunga uongo kupitia magazeti waliyokuwa wanayamiliki Honduras na kwenda kulalamika na kusema kiongozi wa Honduras anataka kuleta ujamaa kama kawaida kupitia CIA wakawapa support waasi wakamwondoa Rais wa Honduras

Matendo ya United fruit company ni sababu kuu ya nchi kama Honduras, Guatemala, na Colombia kuwa kwenye dimbwi la umaskini mkubwa sana mpaka leo

maana fupi ya banana Republic kwa tafsiri ya kile ni nchi ambayo inatoa rasilimali zake na kuwapa makampun ya kigeni kwa kupenda au kutokupenda na baada ya mda ya hali ya wananchi inabaki vile-vile huku hayo makampuni yakidanganya yanapata hasara ilihali yanapata faida na atakayetokea anahoji hayo makampuni sababu yana-nguvu sana yanamshughulikia huyo mtu anaweza akawa kiongozi au mwanaharakati
 
"Mwaka 1911 Honduras walipata rais na akawaambia United Fruit Company tumechoka na tuachieni nchi yetu..."

Nadhani kuna kitu unataka kusema Mheshimiwa, urais utapata na tunatarajia uwaambie tumechoka...
 
"Mwaka 1911 Honduras walipata rais na akawaambia United Fruit Company tumechoka na tuachieni nchi yetu..."

Nadhani kuna kitu unataka kusema Mheshimiwa, urais utapata na tunatarajia uwaambie tumechoka...
History has tendency to repeat itself
 
Back
Top Bottom