FAHAMU HAKI YAKO PALE
UNAPOKAMATWA NA POLISI
Raia ana haki ya kumwomba askari
ajitambulishe kwako.
Mwulize jina lake
Mwulize namba yake ya uaskari
Raia ana haki ya kujulishwa kwanini
anatiliwa mashaka ama kukamatwa.
Raia ana haki ya kuwajulisha ndugu,
jamaa ama sehemu anakofanyia
kazi kwamba ama amekamatwa na
polisi ama Taasisi ya Kuzuia
Rushwa.
Raia ana haki ya kuomba na
kupewa dhamana wakati akiwa
kituo cha polisi ama Taasisi ya
kuzuia rushwa.
Hutakiwi kutoa fedha kama
dhamana uwapo kituo cha polisi
ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa,
isipokuwa maelezo utakayoandika.
Raia ana haki ya kuwaeleza polisi
ama Maafisa wa Kuzuia Rushwa
kwamba lolote atakalosema
linaweza kutumiwa kama ushahidi
mahakamani, na asiburuzwe
kuandika tu.
Raia ana haki ya kuomba Wakili
wake awepo kituo cha polisi ama
Taasisi ya Kuzuia Rushwa wakati
anatoa maelezo yake.
Raia ana haki ya kuyasoma kabla ya
kutia sahihi yake.
Raia ana haki ya kudai risiti ya
orodha ya vitu vyake/fedha zake
alizozitoa ama kukabidhi kituo cha
polisi ama Taasisi ya Kuzuia
Rushwa.
Raia kama ni mwanamke ana haki
ya kupekuliwa na polisi wa kike, na
iwapo hakuna polisi mwanamke,
basi mwanamke yeyote na vile vile
kwa mwanamume.
Raia ana haki ya kufikishwa
mahakamani katika muda usiozidi
saa 24 tangu alipokamatwa na
kufikishwa kituo cha polisi.
[Share na mwenzako kama
umeipenda, toa maoni yako kisha
like]