Jua haki yako unapokamatwa na Polisi

Jua haki yako unapokamatwa na Polisi

Hiyo shule ni muhimu sana, ngoja niwape kisa hiki
Kuna wakati nilikamatwa usiku karibu na mtaani nikaambiwa mie ni mzururaji kwa kuwa sikuwa na ID Nikaambiwa niongozane nao kituoni.
Nikabisha nikawaambia kwanza, hakuna amri iliyotolewa ya watu kutembea na vitambulisho. Pili hakuna amri ya kumzuia mtu kutembea usiku. kwa hiyo sina kosa lolote. wakaniachia.

hivyo kujua haki zako ni suala la msingi sana
 
FAHAMU HAKI YAKO PALE
UNAPOKAMATWA NA POLISI
Raia ana haki ya kumwomba askari
ajitambulishe kwako.
Mwulize jina lake
Mwulize namba yake ya uaskari
Raia ana haki ya kujulishwa kwanini
anatiliwa mashaka ama kukamatwa.
Raia ana haki ya kuwajulisha ndugu,
jamaa ama sehemu anakofanyia
kazi kwamba ama amekamatwa na
polisi ama Taasisi ya Kuzuia
Rushwa.
Raia ana haki ya kuomba na
kupewa dhamana wakati akiwa
kituo cha polisi ama Taasisi ya
kuzuia rushwa.
Hutakiwi kutoa fedha kama
dhamana uwapo kituo cha polisi
ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa,
isipokuwa maelezo utakayoandika.
Raia ana haki ya kuwaeleza polisi
ama Maafisa wa Kuzuia Rushwa
kwamba lolote atakalosema
linaweza kutumiwa kama ushahidi
mahakamani, na asiburuzwe
kuandika tu.
Raia ana haki ya kuomba Wakili
wake awepo kituo cha polisi ama
Taasisi ya Kuzuia Rushwa wakati
anatoa maelezo yake.
Raia ana haki ya kuyasoma kabla ya
kutia sahihi yake.
Raia ana haki ya kudai risiti ya
orodha ya vitu vyake/fedha zake
alizozitoa ama kukabidhi kituo cha
polisi ama Taasisi ya Kuzuia
Rushwa.
Raia kama ni mwanamke ana haki
ya kupekuliwa na polisi wa kike, na
iwapo hakuna polisi mwanamke,
basi mwanamke yeyote na vile vile
kwa mwanamume.
Raia ana haki ya kufikishwa
mahakamani katika muda usiozidi
saa 24 tangu alipokamatwa na
kufikishwa kituo cha polisi.
[Share na mwenzako kama
umeipenda, toa maoni yako kisha
like]
 
Kwa hiyo jizi likivamia usiku wa manane inabidi kisheria tusubiri kuche ndio tiulikimbize kulikamata na kulisachi?

Kuna exceptional...ndio maana kuna makosa ambayo hayahitaj search warrant....kama inaaminika mtuhumiwa hawez kukamatwa mchana...au n jambaz LA maana atakamatwa ucku
 
  • Raia ana haki ya kumwomba askari ajitambulishe kwako.
    • Mwulize jina lake
    • Mwulize namba yake ya uaskari
  • Raia ana haki ya kujulishwa kwanini anatiliwa mashaka ama kukamatwa.
  • Raia ana haki ya kuwajulisha ndugu, jamaa ama sehemu anakofanyia kazi kwamba ama amekamatwa na polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
  • Raia ana haki ya kuomba na kupewa dhamana wakati akiwa kituo cha polisi ama Taasisi ya kuzuia rushwa.
    • Hutakiwi kutoa fedha kama dhamana uwapo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa, isipokuwa maelezo utakayoandika.
  • Raia ana haki ya kuwaeleza polisi ama Maafisa wa Kuzuia Rushwa kwamba lolote atakalosema linaweza kutumiwa kama ushahidi mahakamani, na asiburuzwe kuandika tu.
  • Raia ana haki ya kuomba Wakili wake awepo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa wakati anatoa maelezo yake.
  • Raia ana haki ya kuyasoma kabla ya kutia sahihi yake.
  • Raia ana haki ya kudai risiti ya orodha ya vitu vyake/fedha zake alizozitoa ama kukabidhi kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
  • Raia kama ni mwanamke ana haki ya kupekuliwa na polisi wa kike, na iwapo hakuna polisi mwanamke, basi mwanamke yeyote na vile vile kwa mwanamume.
  • Raia ana haki ya kufikishwa mahakamani katika muda usiozidi saa 24 tangu alipokamatwa na kufikishwa kituo cha polisi.

Mmesahau haki ya kikatiba...ibara ya 16(b)..marufuku kumtende mshitakiwa was kosa LA jinai kama MTU mwenye kosa mpaka ithibitishwe na mahakama
 
Sio PENAL CODE ACT Ni THE CRIMINAL PROCEDURE ACT CHAPTER 20 OF THE LAWS R.E 2002 hii kiswahili tunaita SHERIA YA MWENENDO WA MAKOSA YA JINAI, ni sheria inayoongoza ni jinsi gani mashauri ya jinai yaendeshwe
 
Also Section 23 of the criminal procudure act 23(1) Aperson who arrests another person shall ,at the time of the arrest,inform that other person of the offence for which he is arrested (2) A person who arrests amther person of the substance of the offence for which he is arrested, and it is not necessary for him to do so in a language of a precise or technical nature .
 
Hukukwe2 haki imepotea kabisaaa kwani wanaokamata mapikipik na magal ni askal magereza wenyewe wanajiita voda fasta .Hakika kama nitaeleza kaz za hawa jamaa jf watastaajabu xana
matokeo yanaonekana kwn wanamilik mijengo
noa,na miboxer
kwamuda mfup2
 
Mi kuna swala linanitatiza kuhuxu haki ya kumpeleka askari kituoni kabla hsjakupeleka inakuaje? Ufumbuzi tafazali.
 
Inamaana hizo haki za Raia hao askari polisi hawazijui? Huwa naona watu wakikamatwa huwa hawapewi muda wakujitetea..! Inakuwaje hapo.?
 
Naombeni msaada wa 'law' ya ardhi, nimetaifishwa shamba na gov, bila notice, shamba hilo nime miliki tangu 1970,
 
jamani vip kwa sisi tunaoendesha bodaboda maana trafik anakusimamisha na kuchomoa fungua ya pikipiki hii imekaaje
 
Kaka ameelezea vizuri sana.. Mtuhumiwa hatakamatwa na kupekuliwa na askari polisi... Je... Wewe Ni polisi? Pia uelewe maana ya neno (Isipokuwa) .. In Law every General rule has its Exception..
 
Pole sana... Kitendo cha kutaifishwa tu Ilo shamba lako bila ya kupewa notice ni kosa kisheria.. Pia je kuna Malipo yoyote ambayo walikupatia? Kama watakuwa hawajakupatia malipo yoyote watakuwa wameenda kinyume na katiba ya jamhuri ya muungano ya Tanzania ya mwaka 1977.. Ibara ya 24.. uisome wewe mwenyewe..
 
Je kwa mashahidi wana HAKI gani baada ya kuitwa na mahakama kutoa ushahidi Kenya makos a ya jinai. Je ni lazima wahudhurie?
 
Back
Top Bottom