Jua haki yako unapokamatwa na Polisi

Jua haki yako unapokamatwa na Polisi

jamani mtu atujuze makosa ya barabarani kwani trafick wanatamka mengine ya kutilia shaka
 
Asante mkuu kwa kutujuza ila kwetu hapa ukianza kudai hayo unachezea kichapo kwa kisingizio kwamba unajifanya unajua,

jaribu kufuata haki za raia pindi ukikamatwa na askari wa barabarani uone,japokuwa wengine wanafuata sheria wengine hata sheria za kazi yao hawajui wanachojua ni kutumia nguvu tu.
 
Kwa nini ukikutwa na kosa usilipe hiyo faini tuu? Ili iishe au ipungue tulipe faini tuu, wao hawataomba rushwa, sisi wenyewe ndio tunawashawishi kuwapa kitu kidogo. Halafu kitu kingine watu hata kama hawana kosa kutojiamini kwao ndio askari kisaikolojia tuu anakugandamiza, tuwe ngangari tusionewe
Mkuu uyasemayo ni kweli lkn fikiri,unakamatwa na gari yako unaandikiwa makosa matatu kila moja 30000/=
afande ukimpa buku 10 mmemalizana,unabaki na balansi ya kuanzia kesho.ukikomaa ukalipa zote tisini unapewa makaratasi lkn hayana ushahidi kwamba zinaingia serikalini au nazo zinaliwa na wenye meno.hilo linachangia sana kuwapa maafande maji ya kunywa badala ya kuchangia wanaolia vivulini wakati wenzao wanashinda juani.
 
shida kubwa tanzania hata wanajua sheria na waliopewa dhamana ya kuzisimamia ndio wavunjaji wakubwa.
 
Nlikamatagwa nikivuta ganja Zenji pale beach Gofu. Acha wanirukishe kichura! Manina zao. Hapo nipo bwax kinoma.
 
Hili la mtuhumiwa kukaa lumande kwa muda usiozidi masaa 24 halizingatiwi hasa maeneo ya vijijini
 
Hebu naomba kuuliza kama mtu alikuwa anakudai halafu anapeleka pilice case ya jinai, hii inakuwaje?
 
ukamataji wa polisi lazima uzingatie utu wa binadamu kama katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania inavyotamka ibada ya 12 (2) na kwenye CPA kifungu 11 how arrest made then 0757001400 kwa ushauri wa kisheria wasiliana nami kukujuza mengi
 
wewe jidanganye tu tena kipindi hiki walivyouwawa kama kuku yaani watakuburuza .kumbuka kila haki ina wajibu pia kila sheria inazo isipokuwa zake .akili za kuambiwa changanya na zako.
 
Back
Top Bottom