Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante kwa elimu hii mh. Lakini kwa upande wangu bado sijaelewa vizuri kuhusiana na muda wa Askari kwenda kumkamata au kumpekuwa mtuhumiwa nyumbani kwake. Kwani nimewahi kusikia Polisi wakiwavizia baadhi ya watuhumiwa usiku au alfajiri na mapema majumbani mwao. Na kama hatua hii ni uvunjifu wa sheria, sasa Polisi watawezaje kuwakamata majambazi wanaoingia makwao usiku na kuondoka kabla hakujachwa?
Raia ana haki ya kumwomba askari
ajitambulishe kwako.
o Mwulize jina lake
o Mwulize namba yake ya uaskari Raia ana haki ya kujulishwa kwanini
anatiliwa mashaka ama kukamatwa.
Raia ana haki ya kuwajulisha ndugu,
jamaa ama sehemu anakofanyia kazi
kwamba ama amekamatwa na polisi ama
Taasisi ya Kuzuia Rushwa. Raia ana haki ya kuomba na kupewa
dhamana wakati akiwa kituo cha polisi
ama Taasisi ya kuzuia rushwa.
o Hutakiwi kutoa fedha kama dhamana
uwapo kituo cha polisi ama Taasisi ya
Kuzuia Rushwa, isipokuwa maelezo utakayoandika.
Raia ana haki ya kuwaeleza polisi ama
Maafisa wa Kuzuia Rushwa kwamba lolote
atakalosema linaweza kutumiwa kama
ushahidi mahakamani, na asiburuzwe
kuandika tu. Raia ana haki ya kuomba Wakili wake
awepo kituo cha polisi ama Taasisi ya
Kuzuia Rushwa wakati anatoa maelezo
yake.
Raia ana haki ya kuyasoma kabla ya
kutia sahihi yake. Raia ana haki ya kudai risiti ya orodha ya
vitu vyake/fedha zake alizozitoa ama
kukabidhi kituo cha polisi ama Taasisi ya
Kuzuia Rushwa.
Raia kama ni mwanamke ana haki ya
kupekuliwa na polisi wa kike, na iwapo hakuna polisi mwanamke, basi
mwanamke yeyote na vile vile kwa
mwanamume.
Raia ana haki ya kufikishwa
mahakamani katika muda usiozidi saa 24
tangu alipokamatwa na kufikishwa kituo cha polisi.
Iwapo askari polisi ataamua kumpekua
mtuhumiwa, mtuhumiwa ana haki ya
kumpekua askari polisi KABLA ya
kupekuliwa yeye mwenyewe.
Pia, askari polisi hawana haki ya kuingia kwenye gari, nyumba au ofisi ya mtu
wanayemtuhumu, kwa madhumuni ya
kufanya upekuzi, pasi na kuwapo kwa (a)
hati ya upekuzi ambayo hutolewa
mahakamani,
(b) mashahidi wanaotambulika rasmi kisheria, kama vile, mwenyekiti/mjumbe
wa serikali ya mtaa au mwenyekiti wa
nyumba kumi kumi (iwapo mfumo huo
unatumika), au
(c) jirani wa mtu anayetuhumiwa.
Aidha, mtuhumiwa hatakamatwa au kupekuliwa na askari polisi baada ya saa
12.30 jioni au kabla ya saa 12.30 alfajiri,
kwa mujibu wa Mwenendo wa Makosa ya
Jinai (Penal Code Act), isipokuwa tu, kama
kutakuwa na ushahidi wa kutosha
kwamba, kumpekua mtuhumiwa kabla ya saa 12.30 alfajiri au baada ya saa 12.30
jioni kunaweza kuleta madhara kwa
askari polisi, mashahidi au watu wengine
wowote wale.
Safi, tusaidie pia haki za dereva ukishikwa na traffic police. Maana nao ni keeero tupu barabarani
- Raia ana haki ya kumwomba askari ajitambulishe kwako.
- Mwulize jina lake
- Mwulize namba yake ya uaskari
- Raia ana haki ya kujulishwa kwanini anatiliwa mashaka ama kukamatwa.
- Raia ana haki ya kuwajulisha ndugu, jamaa ama sehemu anakofanyia kazi kwamba ama amekamatwa na polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
- Raia ana haki ya kuomba na kupewa dhamana wakati akiwa kituo cha polisi ama Taasisi ya kuzuia rushwa.
- Hutakiwi kutoa fedha kama dhamana uwapo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa, isipokuwa maelezo utakayoandika.
- Raia ana haki ya kuwaeleza polisi ama Maafisa wa Kuzuia Rushwa kwamba lolote atakalosema linaweza kutumiwa kama ushahidi mahakamani, na asiburuzwe kuandika tu.
- Raia ana haki ya kuomba Wakili wake awepo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa wakati anatoa maelezo yake.
- Raia ana haki ya kuyasoma kabla ya kutia sahihi yake.
- Raia ana haki ya kudai risiti ya orodha ya vitu vyake/fedha zake alizozitoa ama kukabidhi kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
- Raia kama ni mwanamke ana haki ya kupekuliwa na polisi wa kike, na iwapo hakuna polisi mwanamke, basi mwanamke yeyote na vile vile kwa mwanamume.
- Raia ana haki ya kufikishwa mahakamani katika muda usiozidi saa 24 tangu alipokamatwa na kufikishwa kituo cha polisi.
Umesahau hizi:
Nikikumbuka mengine nitawapa mkanda.
- Iwapo askari polisi ataamua kumpekua mtuhumiwa, mtuhumiwa ana haki ya kumpekua askari polisi KABLA ya kupekuliwa yeye mwenyewe
- Pia, askari polisi hawana haki ya kuingia kwenye gari, nyumba au ofisi ya mtu wanayemtuhumu, kwa madhumuni ya kufanya upekuzi, pasi na kuwapo kwa (a) hati ya upekuzi ambayo hutolewa mahakamani, (b) mashahidi wanaotambulika rasmi kisheria, kama vile, mwenyekiti/mjumbe wa serikali ya mtaa au mwenyekiti wa nyumba kumi kumi (iwapo mfumo huo unatumika), au (c) jirani wa myu anayetuhumiwa
- Aidha, mtuhumiwa hatakamatwa au kupekuliwa na askari polisi baada ya saa 12.30 jioni au kabla ya saa 12.30 alfajiri, kwa mujibu wa Mwendendo wa Makosa ya Jinai (Penal Code Act), isipokuwa tu, kama kutakuwa na ushahidi wa kutosha kwamba, kumpekua mtuhumiwa kabla ya saa 12.30 alfajiri au baada ya saa 12.30 jioni kunaweza kuleta madhara kwa askari polisi, mashahidi au watu wengine wowote wale
./Mwana wa Haki
Mh kazi hiyoUmenena kweli...,..
Kwa bongo hapa hayawezekani kiuwalisia, usisababishe tukayatumia then ikawa ndo kiama chako bure