JUBILEE protests IEBC's move on spoilt votes

Mkuu nikitumbukiza karatasi yangu ya kura ndani ya ballot box bila kuweka alama yoyote sehemu yoyote utaiita a casted vote?

Mkuu Kunta Kinte ukishatumbukiza maguu kwenye chumba cha kufanyia mtihani na wewe ni mtahiniwa lakini ukaamua kutoandika chochote hautaitwa absentee (mtoro) bali wewe unaandikiwa fails. Kama wale vijana walioishia kumchora Zombie na Messi wameishia kulambishwa zero na hawakuandikiwa absentees.!!!
 
Last edited by a moderator:
...According to IEBC, as of now, "All Votes Cast" means "Total Number of Valid Votes Cast"....
Butola Labda hiyo definition walikosea. Unajua batola unachoshindania hapa ni sasa na kutaka kusema wale wadogo zetu 240,000 waliopata Division Zero wasihesabiwe kwenye wahitimu wa Form bali wale waliopata Division IV mpaka I ndio wataumbulike. Kunta Kinte hoja yangu ni kuwa kila mkenya aliyetoka nyumbani kwake na kwenda kuunga mstari; kadi yake ikahakikiwa na kuchukua karatasi za kupiga kura huyo kapiga kura na lazima kura yake ihesabiwe na ijumlishwe kwenye jumla ya idadi ya wakenya waliojitokeza kupiga kura
 
Last edited by a moderator:
Butola kupata uharibu wa kura kwa kiwango cha 3% nako kunatia mashaka na hii ilitokea Zanzibar na ilisemekana na kura za Maalimu Seif zilikuwa zinaharibiwa ili kumpitisha Dr Shein. Nahisi hata huko Kenya kuna matatizo si bure

Mkuu Ndachuwa kwa mujibu wa IEBC kura nyingi "zilizoharibika" ni zile ambazo ziliingizwa kwenye masanduku tofauti.. Yaani kura ya raisi ikaingizwa kwenye box la gavana.. ya gavana ikaingizwa kwa seneta & etc..
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Ndachuwa kwa mujibu wa IEBC kura nyingi "zilizoharibika" ni zile ambazo ziliingizwa kwenye masanduku tofauti.. Yaani kura ya raisi ikaingizwa kwenye box la gavana.. ya gavana ikaingizwa kwa seneta & etc..

Sasa hapo zimeharibikaje??? si hizo zingekuwa kura zenye utata ambazo baada ya kujiridhisha idadi ya waliopiga kura na kulinganisha na idadi ya kura zilizopigwa wangeweza kuzihamishia katika masanduku husika na mambo yakaenda vizuri.
 
Last edited by a moderator:
Sasa hapo zimeharibikaje??? si hizo zingekuwa kura zenye utata ambazo baada ya kujiridhisha idadi ya waliopiga kura na kulinganisha na idadi ya kura zilizopigwa wangeweza kuzihamishia katika masanduku husika na mambo yakaenda vizuri.

Na hilo ndilo linaleta kautata fulani hivi Mwita Maranya.. Maana baadhi yao wanataka hizo zirudishwe kwenye masanduku yanayostahili lakini wengine wanapinga.. Na kila upande una sababu..
 
Last edited by a moderator:
Walioandika katiba hapo wamechemsha.

Kadri katiba ilivyo cast votes ni pamoja na zilizoharibika. Hilo Jubilee hata wakienda mahakamani watashindwa maana katiba iko clear.

ILA pia kwa kutumia neno cast votes ina maana kwenye round ya pili kuna uwezekano hata upige kura mara 100 mshinde asipatikane maana hiyo 50% plus one haiwezi kupatikana kama unajumlisha na kura zilizoharibika. Hasa pale wagombea wawili wakikaribiana sana.

Hapo dawa tu ni kubadili hiyo section ili kwenye mahesabu ziingie vald votes tu. Hilo nafikiri ni kwa baadaye maana kwasasa bunge halipo.

Kuandika katiba inayokidhi vigezo vyote sio kazi rahisi maana scenarios zingine huwezi kuzijua mpaka kutokee tatizo.
 
Mtanzania kwenye raundi ya pili sanduku la kutumbukiza kura litakuwa moja hivyo hakutakuwa na mkanganyiko kama alivyoeleza sosoliso
 
Last edited by a moderator:
Butola hao 377000 walikuwa wapiga kura? Kama jibu ni ndiyo kama hawakuona mgombea anayefaa unataka kura yake isihesabiwe?

nani aliyekufundisha kuwa kura zilizoharibika zinamaanisha mpiga kura aliyeharibu kura hakuona mgombea anayefaa?

anyway,kwani katiba yao na sheria na kanuni za uchaguzi wao zinasemaje kuhusu kipengele hicho?ama hakuna hicho kipengele mpaka jambo limetokea ndio wanatafuta namna ya kushughulikia jambo hilo?

ugumu mmojawapo wa sheria,sheria hutungwa baada ya matukio kutokea,huenda kipengele hicho hakuna hata ktk sheria zao!mfano wa jambo ambalo pengine sheria haijatamka chochote..mimi nikaenda kupiga kura nikataka kupiga kura ya mbunge tu sitaki ya diwani wala rais sheria inasemaje kuhusu mtu kama mimi?no surprise huenda hakuna kipengele
 
Sasa hapo zimeharibikaje??? si hizo zingekuwa kura zenye utata ambazo baada ya kujiridhisha idadi ya waliopiga kura na kulinganisha na idadi ya kura zilizopigwa wangeweza kuzihamishia katika masanduku husika na mambo yakaenda vizuri.

tunatakiwa tupata tafsiri sahihi ya kura iliyoharibika maana yake ni nini....kwa maoni yangu kusema kura iliyo sahihi ni ile iliyofuata taratibu husika inaweza kuwa too general,msingi wa kupiga kura ni mtu kutoa maoni yake anadhani nani anapaswa kuwa kiongozi wake...hivyo tafsiri sahihi ya kura iliyoharibika ni ile ambayo kwa namna yeyote ile HATUWEZI KUTAMBUA MAONI YAKE KWA NAMNA ILIVYOPIGWA!sasa kama mtu kampigia kabisa fulani na maoni yake tunaweza kuyatambua lakini kakosea kuweka ktk box kusema imeharibika ni kumnyima haki yake ya kidemokrasia
 

Kura nyingi 'zilizoharibika' inasemekana ni kura ambazo hazikuwekwa kwenye kisanduku husika, yaani mpiga kura ametia alama sawa sawa na maelekezo, lakini kwa kudumbukiza kwenye pipa, akajisahau akaweka kura ya Senator kwenye pipa la Rais, au ya mbunge kwenye pipa la Governor. Watu wengine ni colour-blind hasa ukizingatia waliopiga kura kwenye mwanga wa gas lamp au fluorescent tube.
 
Butola,

Pamoja na ZeMarcopolo, Kunta Kinte, SMU, mfianchi, Mwanakijiji, Ngongo, na wengine wote wanaosoma.

Heshima mbele wakuu. Nataka niseme hivi:

Tukumbuke kua Kenya na Tanzania ni vitu viwili tofauti wakati huu na kwa hapa namaanisha kikatiba. Ishu za ushabiki na maswala yoyote yale hii leo yanawsilishwa mahakamani ambapo Katiba mpya inazidi kila mtu kete.

Kwa hivyo tujiulize Katiba ya Kenya inasema nini kuhusu hili swala? Kwa haraka, hawa IEBC wako sahihi kujumlisha kura zilizopigwa maana that's what the Kenyan Constitution says.

Sasa hii hapa katiba mpya ya Kenya:

Section 109 (1) (p) of the Elections Act 2011 states that the IEBC may:

"prescribe the procedure to be followed in the counting of votes and the circumstances in which votes may be rejected by a returning officers as being invalid"


Regulation 77 (1) of the Elections General Regulations 2012, sets out the conditions under which a ballot paper may be rejected and states that:

"Any ballot paper-

(a) which does not bear the security features determined by the Commission;

(b) on which votes are marked, or appears to be marked against the names of, more than one candidate;

(c) on which anything is written or so marked as to be uncertain for whom the vote has been cast;

(d) which bears a serial number different from the serial number of the respective polling station and which cannot be verified from the counterfoil of ballot papers used at that polling station; or

(e) is unmarked,

shall,
subject to subregulation (2), be void and shall not be counted."

Sub-regulation 2, for the avoidance of doubt, states that the presiding officer may uphold a ballot paper if the intention of the voter can be clearly discerned.



Concerning the constitutional provision being relied on to count "all the votes" cast
,

Article 138 (4) (a) states:

"A candidate shall be declared elected as President if the candidate receives more than half of
all the votes cast in the election."



Tuzidi kuelimishana.
 

Mkuu hapo bado kuna mkanganyiko. Kama katiba inasma vote shall not be counted then watajuaje idadi yake?

Jinsi nilivyoelewa ni kwamba hiyo vote haitaingia kwenye mahesabu ndio maana haitakiwi hata kuhesabiwa.

That means kwamba kabla ya kuhesabu kura hatua ya kwanza inatakiwa kuwa kuverify kama kura zote zimekidhi vigezo vilivyotajwa. Zile zote ambazo hazijakidhi ziwekwe pembeni bile kuhesabiwa (shall not be counted) halafu sasa zile zilizokidhi vigezo kuanza kuhesabiwa na majibu yake kutengeneza asilimia.
 
Reactions: SMU
mkuu @Ab-Tichatz hii katiba iko ambiguous na inavyoonekana italeta matatizo makubwa, tuombe wapite salama ili waifanyie marekebisho. Naamini na Warioba na wenzake nao wanafuatilia haya ili waepuke shida hizi kwenye katiba waitengenezayo
 
Ab-Titchaz , baada ya kusoma hizo extracts ulioweka hapo juu, kwa namna fulani nakubaliana na mawazo ya ZeMarcopolo hapo juu na pengine naiona hoja ya Jubilee.

Najaribu kujiuliza, what is a vote? and what is a ballot paper? Kwa kiswahili nadhani "vote" ni kura (ni dhana inayoonesha uamuzi wa mtu/mpiga kura), wakati 'ballot paper' ni 'karatasi ya kupigia kura' (ie. karatasi ambayo mpiga kura anaonesha uchaguzi/uamuzi wake). Sasa kama 'ballot paper' imejazwa katika njia ambayo maafisa hawawezi ku determine kwa usahihi "uamuzi" (vote") wa mpiga kura, then kimsingi huyo mpiga kura atahesabika kama "hajafanya uamuzi wowote" (has not cast/'casted' his "vote"), ingawa alifika kituoni na kujaza "ballot paper".

Katiba, inazungumzia "...votes cast in the election" ( na sio "ballot papers" zilizojazwa katika uchaguzi).
 
Kwani hayo makubaliano ya awali kabla ya kupigwa kura kuna any documentation na kila chama ilipewa copy yake?

Asanteni Ze Marcopolo na butola kwa kuchambua angle ambayo naona wakenya wasipoangalia, wanaweza kufanya elections mwaka mzima wa kupata rais bila kufikia muafaka, kwa kung'ang'ania "all votes cast" badala ya "valid votes cast".

Na kwenye hili ndio kuna potential ya that dreaful small spark itakayoweza kuleta a loud explosion.

Nilichogundua kuna watu wengi sana waliaminishwa na akina SYNOVATE na other opinion poll mongers kwamba RAILA ndiye chaguo la wakenya. Sasa wanapoona kile kinacho unfold ni kinyume, hata ile center ya LOGIC kwenye brains zetu nayo inakufa. Wanabaki kuwa kama makasuku wa maandiko, kiasi cha kuipa tafsiri ya kimahakama kifungu tajwa.

I can see a long battle ya kuhakikisha Kenyatta haingii Ikulu, ila it will come at a price.

Best Wishes to our neighbours, i hope sane minds and sound judgements will prevail.
 
kwa sasa sio wakati wa kutunga sheria tena, sheria ishasema wazi kuwa kura za maruhani zinahesabiwa, kama ni hivyo basi mambo yaende hivyohivyo uchaguzi hata ukirudiwa mara 7, kazi iwe kuelimisha kura za kuharibika zisitokee. ila baada ya uchaguzi huu tu katiba ndipo inabidi irekebishwe
 
Soma katikati ya mistari:

The Constitution sets the threshold for victory at 50 per cent plus one vote for “all votes cast”.


ALL votes cast ina maana Kura zote zilizopigwa zikiwamo zilizoharibika. unless kwa tafsiri yako kura zilizoharibika hazikupigwa! na kama hazikupigwa zimeharibika vipi??!!
 

All votes cast? Including those that ideally do not belong to the presidential ballot box?
 
Napata shida sana kuelewa definition ya rejected votes. Hapa namnukuu Isaack Hassan "For any rejected vote for any candidate, they were being multiplied by eight," said the IEBC chairman.

Rejected vote inaweza vipi kuwa for a certain candidate?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…