Ab-Titchaz , baada ya kusoma hizo extracts ulioweka hapo juu, kwa namna fulani nakubaliana na mawazo ya
ZeMarcopolo hapo juu na pengine naiona hoja ya Jubilee.
Najaribu kujiuliza, what is a vote? and what is a ballot paper? Kwa kiswahili nadhani "vote" ni kura (ni dhana inayoonesha uamuzi wa mtu/mpiga kura), wakati 'ballot paper' ni 'karatasi ya kupigia kura' (ie. karatasi ambayo mpiga kura anaonesha uchaguzi/uamuzi wake). Sasa kama 'ballot paper' imejazwa katika njia ambayo maafisa hawawezi ku determine kwa usahihi "uamuzi" (vote") wa mpiga kura, then kimsingi huyo mpiga kura atahesabika kama "hajafanya uamuzi wowote" (has not cast/'casted' his "vote"), ingawa alifika kituoni na kujaza "ballot paper".
Katiba, inazungumzia "...votes cast in the election" ( na sio "ballot papers" zilizojazwa katika uchaguzi).