JUBILEE protests IEBC's move on spoilt votes

JUBILEE protests IEBC's move on spoilt votes

Kama wanaiita rejected vote halafu wanaijumlisha sasa hapo hiyo vote imekuwa rejected vipi?

Rejected vote in my view maana yake ni karatasi ambayo imekutwa kwenye ballot box inayofanana na karatasi za kupiga kura lakini haijakidhi vigezo vya kuwa kura halali na hivyo basi haipaswi kuingia kwenye mahesabu yoyote yanayoweza kuamua mshindi wa uchaguzi.

Unaporuhusu rejected votes ziamue kama uchaguzi urudiwe au la unaondoa maana ya msingi ya kura.
 
Hawa jamaa wananikumbusha wahindi wa Mwanza na viwanda vyao vya samaki, unaweza kupeleka lori lako limejaa samaki kama tani saba halafu ukajikuta zaidi ya nusu ni reject na kwa maana hiyo hawakulipi lakini cha ajabu hawakuachii samaki uondoke nao au kuona wakiwatupa.
 
Kama hii hapa chini ndiyo provision ya katiba yao namna ya kumpata mshindi wa kiti cha uraisi hapo IEBC hawastahili lawama hata kidogo bali kwakuwa kila mmoja angependa kupata ushindi wa moja kwa moja raundi hii ya kwanza ndio sababu wanalalamika, wala hili halihitji intervention ya foreign missions kama Ruto anavyolalamika, ni suala tu la tafsiri ya katiba na sheria. Hapo kwenye red colour hapo ndipo tafsiri sahihi ya kikatiba ilipo na kama wanadhani ama na wewe Butola unadhani kujumuisha kura zilizoharibika ni makosa basi inabidi uwashauri wakenya wairekebishe katiba yao isomeke kwamba mshindi atapatikana kwa asilimia 50 + ya kura halali.

Mkuu nikitumbukiza karatasi yangu ya kura ndani ya ballot box bila kuweka alama yoyote sehemu yoyote utaiita a casted vote?
 
226451_10200730299200318_1537057947_n.jpg

Mmh wakuu mbona hii form ya results declaration inanipa wasiwasi.
Ukiiangalia vizuri hiyo karatasi kuna maeneo mawili yamenipa mashaka na usahihi wa hizi kura.

Kwanza, Total number of registered voters for the polling station-726
Pili, Total number of votes cast-769

Swali langu hapa imekuwaje kura zilizopigwa (769) zimezidi idadi ya watu waliojiandikisha (726) katika kituo hicho?
Je kuna uwezekano kwamba kuna mchezo mchafu umechezeka hapa???
 
...Nakubali kuwa imeandikwa hivyo, ndio maana nadhani kama IEBC wataidefine hivyo, ni vyema iende mahakamani ili mahakama nayo ipate nafasi ya kutoa definition ya suala hili...

...kwa sababu kama definition ndio hiyo, hilo hitaji la kipengere hicho litakuwa ni la kijinga kwa sababu "halijaangalia ni kwa namna gani tutaumaliza uchaguzi kama ata kwenye uchaguzi wa marudio pia hakutakuwa na mgombea atakayepata zaidi ya 50%+1?hii ndio hofu yangu hapa, watarudia uchaguzi mara ngapi ndio waseme sasa basi?...
 
Mkuu hiyo ndio demokrasia sasa, kwa kizungu changu cha kuunga unga wanasema Democracy is the dictatorship of the majority to the minority, as long as below 50% is regarded as a minority then they should agree with the majority which is above 50%.

Kwa wenzetu ni sawa!

Ila kwa nchi zetu za kiafrika, ambapo kila mpiga kura ana ineterest zake (dini,kabila,rangi,rafiki........) majority inabidi ielezewe vizuri, kwa sababu 50%+1, and 49.9% is almost the same, hapo nani atamuelimisha mwenzake na ukitokea ogomvi ujue lazima mass murder itokee!

Tuache kuiga wazungu kwa kila kitu, we unadhani tungekuwa tunaangalia sera kungekuwa na 50.0001% win and 49.99999% lose?
 
Kama wanaiita rejected vote halafu wanaijumlisha sasa hapo hiyo vote imekuwa rejected vipi?

Rejected vote in my view maana yake ni karatasi ambayo imekutwa kwenye ballot box inayofanana na karatasi za kupiga kura lakini haijakidhi vigezo vya kuwa kura halali na hivyo basi haipaswi kuingia kwenye mahesabu yoyote yanayoweza kuamua mshindi wa uchaguzi.

Unaporuhusu rejected votes ziamue kama uchaguzi urudiwe au la unaondoa maana ya msingi ya kura.

...Aksante sana hapo...
 
Mmh wakuu mbona hii form ya results declaration inanipa wasiwasi.
Ukiiangalia vizuri hiyo karatasi kuna maeneo mawili yamenipa mashaka na usahihi wa hizi kura.

Kwanza, Total number of registered voters for the polling station-726
Pili, Total number of votes cast-769

Swali langu hapa imekuwaje kura zilizopigwa (769) zimezidi idadi ya watu waliojiandikisha (726) katika kituo hicho?
Je kuna uwezekano kwamba kuna mchezo mchafu umechezeka hapa???

Inawezekana sheria zinaruhusu wasimamizi, polisi na kadhalika kupiga kura sehemu walipo hata kama hawajajiandikisha hapo!!
 
Labda ili tuelewane vizuri inabidi tuanze na definition ya kupiga kura.

Kupiga kura maana yake siyo tu kuidumbukiza karatasi ya kura kwenye sanduku la kura.

Ili mtu aitwe kuwa amepiga kura ni LAZIMA vigezo vifuatavyo vitimie.
1. Kuwa na sifa za kikatiba za kupiga kura
2. Kufika kwenye kituo cha kura kwa muda uliopangwa
3. kuweka alama inayoashiria kumchagua mmoja wapo wa wagombea/chama
4. Kuidumbukiza karatasi/kura kwenye sanduku la kura au sehemu nyingine iliandaliwa maalum kwa shughuli hiyo.

Iwapo chochote kati ya hivi vinne hakijakamilika basi karatasi/taarifa inayokutwa kwenye kisanduku cha kura inapoteza sifa ya kuitwa kura. Hii inamaanisha inatoka kwenye mahesabu yote yaliyodhamiriwa kwa ajili ya uchaguzi.

Kutokana na hatua ya kutokutekeleza masuala hayo manne, kunatakiwa kuwe na sheria inayoelezea hatua gani zinapaswa kuchukuliwa kwa maana ya adhabu kwa kukiukwa kwa kanuni/sheria.
Kwa mfano katika hatua namba 1 akitokea mtu ambaye hana sifa akaruhusiwa kufanya hatua 2,3 na 4 basi mtu huyo pamoja na wote waliohusika kumruhusu wanatakiwa kupewa adhabu kisheria, vile vile kwenye hatua namba 2 iwapo mtu ameruhusiwa kupiga kura mapema kabla ya muda rasmi wa kufungua kituo. Kwa misingi hiyohiyo katika hatua namba 4 iwapo karatasi iliyochagua mgombea ikikutwa nje ya kisanduku cha kura waliohusika kusababisha hilo wanapaswa kuadhibiwa kisheria.

Kwa sababu kura hupigwa kwa siri, mtego uko kwenye hatua namba 3 ambapo kwanza haiwezekani kumtambua ni nani aliyechora karatasi kinyume na utaratibu na pili ni vigumu kuthibitisha kuwa mtu huyo alikuwa na elimu ya kutosha kumuwezesha kujua jukumu lake kama mpiga kura. Kwahiyo hapa HAIWEZEKANI kutoa adhabu kwa aliyeharibu karatasi ya kura ila tu karatasi hiyo inakuwa haijakidhi sifa za kuitwa kura na haitakiwi kuingizwa kwenye mahesabu kama jinsi zile karatasi nyingine zilizokosewa katika hatua 1,2 na 4.
 
Mkuu nikitumbukiza karatasi yangu ya kura ndani ya ballot box bila kuweka alama yoyote sehemu yoyote utaiita a casted vote?
Wewe si utahesabika "umeshapiga kura" (huwezi kuruhusiwa kurudia)?
 
swali la kizushi:
Tuseme zimepigwa 100,kura 20 zikaenda kwa Raila,kura 25 zikaenda kwa Uhuru na kura 55 zikaharibika,hivi Uhuru atatangazwa kuwa ni Rais wa Kenya?

We do round three UHURU vs Kura za Kuharibika.

Kura za kuharibika zikimzidi UHURU it means wananchi hawataki yeyote kati ya waliojitokeza....Vyama vilete wagombea wapya...kwenye multiple choice tunaita "NONE of the ABOVE"

masematiki kiboko usipokomaa unaishia kuchora Zombie.....lol
 
Lakini hajawataja Jubilee! Au unaunganisha dots?

...Si unajua Kibaki hagombei katika uchaguzi huu?...

Hizi ndizo mbinu zilizotumika 2007 kumrudisha Kibaki Ikulu. Naona jamaa hawakupata funzo na wanarudia
tena. Thats the only explanation to it...jamaa wanachakachua hizi kura.
 
...Sina tatizo na hilo, tatizo langu ni uwezekano wa mgombea yeyote kutopata 50%+1 ata kwenye uchaguzi wa marudio, sasa je uchaguzi utarudiwa mara ngapi?

...hapa ndipo ilipo hekima ya kuchukua tu "Jumla ya Idadi ya Kura Halali", ukizichukua tu "kura halali" basi ni lazima round ya pili itatoa mshindi, lakini bila hivyo, mtarudia uchaguzi mara ngapi?hapa ndipo palipo na tatizo...

Kiongozi....Suppose wananchi walio wengi 75% (20% kura opponent na 55% za NONE) hawajaridhika na yeyote katika wagombea unawalazimisha watawaliwe na aliyepata 25%??
 
Kiongozi....Suppose wananchi walio wengi 75% (20% kura opponent na 55% za NONE) hawajaridhika na yeyote katika wagombea unawalazimisha watawaliwe na aliyepata 25%??

...kama wanazihitaji sana hizi "kura zilizoharibika", nadhani it makes sense kuweka utaratibu kuwa kama hizi kura zitawanyima ushindi wagombea kwenye duru ya pili, basi itamkwe kuwa "wagombea hao wote" wataondolewa na process ya uchaguzi kuanza tena upya kabisa, lakini vip kama ata hao wengine watazuiwa na "kura zilizoharibika" kupata 50%+1?je uchaguzi utarudiwa mara ngapi?na je nchi kweli haitafilisika kwa kufanya chaguzi?...
 
Ninakupata uzuri sana kwenye hii point and am in full agreement...ila nadhani watunga katiba hili hawakulitarajia ndiposa hawakuweka provision on how to go about...

Ukiacha tu mambo yaende in the name of democracy hata kile kidogo mlichonacho kinatafunwa na uchaguzi...Run off Kenya itagharimu kiasi cha Ksh 6billion, pesa ndefu sana hiyo.
 
Hapa kuna kitu,haiwezekani kura karibia laki tano ziharibika,alafu kuna tetesi nimezisoma sehemu fulani kwamba mtandao wa IEBC umekuwa hucked,inasemekana,kuna expart wa mambo ya mtandao alikodiwa na chama fulani ili kufanya haya mambo,na inasemekana huyo jamaa ashakamatwa.

Jamani hata mimi hili jambo la jirani zetu la uchaguzi kura zilizoharibika laki 5?. Ni nyingi sana.

Jamani kweli huu ni makakati wa kimipango ambao umekodiwa na chama fulani ili kukiangusha kingine
Hata hivyo jamani kama kweli amekamatwa mtu aliyechezea mfumo wa kuhesabu kura tume inabidi imtangaze na kwa vile computer au software ina record mtu akliingia na kutoka na mpaka muda mathalani kwenye computer software inaonyesha ninani ila kama ni mtaalamu wa computer basi sijui atatumia mbinu gani asionekane basi tumwachie Mungu.

Kweli majirani zetu ni watu wa ajabu ni washindaniwa ukabila sana sana kuliko sisi hapa bongo

sisi tunao wezi wetu wa kila siku chama tawala nasi lakini KATIBA mpya itaondoa mambo yote. Tuombe Mungu nasi hapo mwakani itoke katiba mpya ila mizengwe kwa majirani zetu jamani wametuzidi. Mungu awasidie majirani zetu wanashida kubwa na waondoe ukabila ili taifa lao liwe salama. Amina
 
Butola kupata uharibu wa kura kwa kiwango cha 3% nako kunatia mashaka na hii ilitokea Zanzibar na ilisemekana na kura za Maalimu Seif zilikuwa zinaharibiwa ili kumpitisha Dr Shein. Nahisi hata huko Kenya kuna matatizo si bure

pendekeza: na hapa zinaharibiwa za nani ili ashinde nani?, na ni nani anayeziharibu?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom