Judith Kapinga amegawa mitungi ya gasi 1500 kwa wakazi wa Kijiji cha Msomela Wilayani Handeni mkoani Tanga

Judith Kapinga amegawa mitungi ya gasi 1500 kwa wakazi wa Kijiji cha Msomela Wilayani Handeni mkoani Tanga

Blasio Kachuchu

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
366
Reaction score
243
Na Mwandishi Wetu, Tanga.

NAIBU Waziri wa Nishati Judith Kapinga amegawa mituni ya gasi 1500 kwa wakazi wa Kijiji cha Msomela Handeni Wilayani Handeni mkoani Tanga iliyotolewa na Kampuni ya Taifa Gas.

Kutolewa kwa mitungi hiyo kwa wakazi hayo inalenga kuunga mkono kampeni ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk, Samia Suluhu Hassani ya kumtua mzigo wa kuni Mama kwa kutumia nishati ya Taifa Gas na kuhifadhi Mazingira.
Akishukuru msaada huo Naibu Waziri wa Nishati Kapinga amesema Taifa Gas walichokifanya Msomela ni kupanda mbegu ya Mabalozi wa kudumu ambao watakuwa na wataendelea kuwa wateja wenu daima.

"Imarisheni huduma hii hapa Msomela na jirani kuzunguka Msomela ili wananchi hawa gesiikiisha wasipate tabu mahala pa kwenda kubadilisha."

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Taifa Gas, Davis Deogratius amesema timu yake tayari imeshafanya mchakato wa kuwa na mawakala hapo Msomela tena wazawa, hivyo wasiwe na wasiwasi kwani gesi ikiwaishia wataipata Msomela na wale ambao hawajabahatika kupata mitungi ya Taifa Gas tayari ipo itakuwa inauzwa kwa bei nafuu.

Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Wakili Albart Msando amewashukuru Taifa Gas kwa msaada mkubwa kwa Wananchi wake wa Msomela na aliendelea kuwaomba kuwa wananchi wake ni wengi hapa watapata nusu yao tu na nusu bado hivyo wakipata nafasi tena wasiwasahau Wananchi wa Msomela waliokosa.





















 
Ikiisha inajijaza ? Kuna mdau wangu mmoja aliniambia there is no such thing as bad publicity.., hapo mwenye Taifa gesi kajipatia promo na kutangazwa as well as kutafutiwa soko la gesi ikiisha kujazwa tena..., Nadhani sisi kama wadau na Serikali tungejikita kwanza kweli swali kama Hii Gesi is the way to go in the first place....

Ukizingatia kuna mapesa yanakuja mengi ya Nishati Safi..., Sasa tusije kutajirishana wenyewe kwa wenyewe kwa hasara ya kumuondolea mama mzigo wa kuni na kumpatia mzigo wa gharama za pesa...

Nishati Safi ya Kupikia, Mwarobaini tunao na ni Bora kuliko Gesi

 
Viongozi wetu wapuuzi kweli.badala ya kupunguza bei ya gesi wao wanawagawia gesi ambayo ikiisha wananchi hawataweza kujaza tena.upuuzi kabisa.wanachofanya hapo ni kutangaza kampuni ya taifa gesi na kuiongezea wateja.kama mnalengo la kuwasaidia Kwa Nini gesi ikiisha hamuwapi hela ya kwenda kujaza nyingine?
 
A good business and marketing strategy for some tycoons.
Umewaza Kama Mimi Ila issue itakuja kwenye ku refill maana icho kipato Cha MTU wa Chini kabisa anae ishi Chini ya dola moja sizani Kama ATAWEZA ku accommodate 24,000/= kila gesi iki isha
 
Back
Top Bottom