stigajemwa
JF-Expert Member
- Nov 12, 2016
- 449
- 430
Wanabodi,
Kutokana na vitendo vinavyofanywa na viongozi wa serikali na vyombo vya dola kuna kila dalili kuwa upinzani hauhitajiki tena nchini na kwamba mfumo wa chama kimoja ndio unaohitajika kwa sasa.
Mfano mzuri ni huu wa kuzuia wabunge wa upinzani kufanya mikutano kwa Uhuru na wapiga kura wao. Hii imetokea Mara kwa Mara kwa wabunge kama Msigwa,Mbowe,Mnyika na wengine wengi.
Mfano mwingine ni huu wa viongozi waandamizi wa serikali kutokuwapa ushirikiano wabunge wa upinzani. Hii imejidhihirisha pale wanapowaambia wananchi kuwa hawatapewa maendeleo sababu walichagua upinzani,huku pia wakiwaandalia mazingira ya kuonekana ni wezi wanaokula pesa za ruzuku ya jimbo na sitting allowance bila kuwajali wala kuwasemea wananchi waliowachagua.
Mfano mwingine ni huu wa kuwabambikia kesi za jinai na kuzuia mikutano ya hadhara kwa viongozi wa vyama vya upinzani nchini.
Matukio yote hayo yanaashiria shughuli za vyama vya upinzani hazihitajiki tena nchini na kwamba wabunge wa upinzani hawapaswi kurudi bungeni 2020.
Swali ni je, kuondoa wabunge wote wa upinzani bungeni na kuua vyama vya upinzani ni kwa maslahi mapana ya nani? Je,Watanzania wote?aAu kikundi? Au mtu fulani?
Nawasilisha.