Juhudi za udhibiti wa kichocho za China zawaokoa maisha Visiwani Zanzibar

Juhudi za udhibiti wa kichocho za China zawaokoa maisha Visiwani Zanzibar

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,310
Reaction score
1,265
4QGhJwB8u4InIgC1.jpg

China ni nchi kubwa inayoendelea, ambayo imekuwa mstari wa mbele katika kuzisaidia nchi nyingine zinazoendelea duniani zikiwemo za Afrika, kujipatia maendeleo kwa njia na mazingira yanayoendana na nchi husika. Kwa kupitia njia mbalimbali, China imekuwa ikitoa misaada kwa nchi hizo katika sekta tofauti ikiwemo afya, kilimo, uchumi na biashara, na ujenzi wa miundombinu.

Katika sekta ya kilimo, China imekuwa ikihamisha teknolojia zake za kisasa za kilimo kwa nchi za Afrika, na hivyo kuzisaidia kuongeza mavuno na kupata usalama wa chakula. Mbegu bora, zana za kilimo, na utaalamu wa China uliohamishiwa kwa nchi za Afrika, zimesaidia sana katika kuboresha kilimo na hivyo kuinua hali ya maisha ya wakulima.

Kwa upande wa sekta ya afya, China imekuwa na desturi ya kupeleka timu za wataalamu wa afya katika nchi za Afrika ambao wamekuwa wakishirikiana na madaktari wazawa kutoa tiba kwa wagonjwa wa huko. Timu hizo zimepongezwa sana na watu katika nchi husika, kwani pamoja na changamoto ya lugha, wataalamu hao wamekuwa wakitoa tiba sahihi na za uhakika.

Visiwani Zanzibar, Tanzania, kichocho ni ugonjwa ambao uliwasumbua watu wa huko kwa muda mrefu, hususan katika maeneo ya vijijini, ambako wakazi walitegemea maji ya mito na visima visivyo salama, na hivyo kupata maambukizi ya ugonjwa huo. Lakini sasa, wakazi wa Chaani, kisiwani Unguja, wanafurahia maisha yao baada ya kuondokana na ugonjwa huo, na hii ni kutokana na mradi wa maji safi uliowezeshwa na China, kama moja ya njia za kukabiliana na ugonjwa wa kichocho. Hivi sasa, maji safi na salama yanapatikana kwenye mabomba katika kijiji hicho, kitu ambacho wanakijiji wa hapo hawakuwahi kutarajia kuwa kitatokea.

Kwa miongo mingi, kijiji cha Chaani kilichoko kisiwani Unguja, Zanzibar, kilikuwa na tatizo la vyanzo visivyo salama vya maji, lakini hali hiyo ilianza kubadilika mwaka 2025. Mkazi wa eneo hilo, Haji Makame Omar anasema, kwa miaka mingi maji lilikuwa ni tatizo kubwa sana kwao, na waliteka maji kutoka kwenye mito, na hapo ndipo walipata maambukizi ya kichocho. Lakini sasa, kutokana na upatikanaji wa maji safi ya bomba, hawana tena haja ya kwenda mtoni kuteka maji, na hivyo wako salama. Makame ameusifu mradi wa kudhibiti kichocho unaoungwa mkono na China na kutekelezwa kwa pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO) na serikali ya Zanzibar. Kwa kuunganisha mifumo ya upatikanaji wa maji safi na tiba ya ugonjwa huo, udhibiti wa konokono na elimu ya afya, mradi huo umepunguza kidhahiri kiwango cha maambukizi huku ukiboresha maisha ya watu.

Kwa wanawake, ambao walibeba mzigo mkubwa wa kuchota maji na kuhudumia watoto, mabadiliko hayo yamekuwa dhahiri. Mwanaisha Abdallah, mkazi wa kijiji cha Chaani, anasema zamani walikuwa wanasumbuka sana, lakini sasa, anatembea mwendo mfupi na kupata maji, pia anaweza kulima bustani ya mbogamboga na kufua nguo kwa urahisi.

Katika kijiji hiki cha Chaani, mafanikio ya mradi huu yanaonekana kidhahiri. Bustani za mbogamboga zinaonekana katika nyumba za watu, na hii inatokana na maji kuwa karibu na makazi. Uwanja mdogo ambapo bomba la maji lipo, umegeuka kuwa sehemu yenye shughuli nyingi sana katika kijiji hicho.

Lakini nyuma ya mabadiliko yanayoonekana wazi, kuna juhudi za ushirikiano zilizodumu kwa miongo kadhaa. Kwa mujibu wa Wang Wei, kiongozi wa timu ya watu watano ya kundi la wataalamu wa China, na profesa kutoka Taasisi ya Magonjwa ya Vimelea ya Jiangsu, China, ushirikiano huu ulianza baada ya Zanzibar kutafuta msaada wa kimataifa mwaka 2014, wakati ugonjwa wa kichocho uliendelea kuwepo licha ya juhudi za kuudhibiti. Anasema uzoefu wa China katika kudhibiti kichocho ulionyesha mafanikio makubwa na ya kiwango kikubwa, na kutokana na ahadi ya pamoja, China, WHO na serikali ya Zanzibar zilisaini makubaliano ya awali, na mradi huo ukazinduliwa rasmi mwaka 2016.

Kwa mujibu wa takwimu za mradi huo, awamu ya kwanza ya mradi, utekelezwaji katika kisiwa cha Pemba kuanzia mwaka 2017 hadi 2020, ulipunguza kiwango cha maambukizi katika maeneo hatari kutoka asilimia 8.92 hadi asilimia 0.64, na kukidhi vigezo vya WHO vya kutokomeza kichocho kama tatizo la afya ya umma. Awamu ya pili ya mradi huo, iliyozinduliwa mwaka 2023, imeongeza wigo wake mpaka kisiwa cha Unguja.

Licha ya miundombinu, mradi huo pia umejikita katika uendelevu. Hospitali za umma na watu wa kujitolea walipata mafunzo, elimu ya msingi ya afya na shule za mfano zilianzishwa, na usimamizi ulijumuishwa hatua kwa hatua katika mifumo ya taarifa za afya ya Zanzibar.
 
Back
Top Bottom