Juice na unga wa ngano kutoka viwanda vya Kenya vitaingia Tanzania bila vikwazo na sementi kutoka viwanda vya Tanzania vitaingia Kenya bila vikwazo

Azam na mo mbona wana viwanda kenya
 
Aue tu. Miaka yangu hii 65 sina la kupoteza
 
Umesemaje paragraph ya mwisho?
 
Kenya hakuna kiwanda cha ngano kikubwa kama AZAM. Na ubora wa bidhaa za AZAM ni wa kimataifa,kwa hiyo AZAM wamepata fursa ya kuuza bidhaa zao Kenya.
 
hivi sasa wajameni tutakaa hivi mpaka lini?!? maana miaka nenda miaka rudi kauli ni ileile tunalinda viwanda vyetu wakati huohuo tunasaini mikataba ya kimataifa (kama huu wa Afrika Mashariki). tunaogopa kushindana!?! yaani hapa tulipofikia hatuna maarifa tene ya kuboresha bidhaa zetu za viwanda kuhimili vishindo vya ushindani?!? hivi makampuni yetu hayawezi kwenda kuuza bidhaa kenya?!?,Burundi, Congo DRC, Chad au Mali!?! hebu wajuzi sanakabisa wa uchumi wa viwanda mtufundishe hapa
 
Huyo ndio SSH, yeye mwenyewe anakuambia anatumia akili, sijui hizi ndio akili zenyewe?
We kenge tuliza mshono. Sisi wenye akili tunaona mambo makubwa anayofanya mama.

We kenge kwa akili yako ndogo huwezi kuona. Kila siku,kazi yako ni kumponda mama..why?
 
Kenya hakuna kiwanda cha ngano kikubwa kama AZAM. Na ubora wa bidhaa za AZAM ni wa kimataifa,kwa hiyo AZAM wamepata fursa ya kuuza bidhaa zao Kenya.
ni kweli sidhani kama AZAM anatetemeshwa na hilo, kuanzia afrika mashariki hii yote mpaka kusini mwa Afrika AZAM yupo hivyo sidhani kama ana hofu yoyote
 
Nonsense!

You are just making noise.
 
We mataga tulia. Acha kutupigia kelele.

Wakati dikteta wenu mwendazake alipokuwa anatuharibia nchi mbona mlikaa kimyaa? Tulieni mama ajenge nchi.
 
Hiyo historia uliyotoa wapi jomba? Huyo aliyekusimulia alikulisha matango pori kabisa. Kwa mfano,Tanzania,Kenya na Uganda hazijawahi kutumia sarafu moja katika historia!
 
Mbona sijasema najua kila kitu. Nilimaanisha kama wameweza kupata masoko huku watashindwaje kupata soko hapo jirani hadi tuwe na woga wote huo?
Kuhusu ingredients "zote" kuwa artificial kama lina ukweli maana wapo watu wengi wanaowauzia azam maembe na machungwa, sasa huwa wanayapeleka wapi? Kweli kuna juice zao ambazo ni ingredients zote ni artificial na wala hawajawahi ficha na mtu yeyote anaweza jua.
Then kuna ambazo wanatumua juice pulp au concentrate, hizi ni natural ingredients ambazo wanaimport. Concentrate ni juice ya kawaida ila imetolewa maji ili iwe rahisi kusafirishwa na kuhifadhi.
Halafu juu ya yote hayo tujue kila mzalishaji ana target market yake. Kuna watu wanotaka juice isiyo na sukari/preservatives iliyoongezwa na kuna wengine hawajali sana kuhusu hilo. Huyo anayetumia all natural ingredients wateja wake watanunua kwa bei ya juu kidogo kwa hiyo market yake sio sawa na anayetumia additives.
 
Yaani mimi ninachoshwa sana na hii mentality. Sijui watu wanaogopa nini kwa wakenya na wageni wengine. Mbona ni watu wa kawaida tu na tunashindana nao mara kibao tunawachakaza vibaya mno. Dunia ya sasa hivi sio ya kuogopana, vitu kama hivi ni fursa ya watu kujitanua.
 
Yaani tutafaidi uhondo huo! Na kuna Zesta Jam, Blue Band na Omo! Tutaachana na hiyo mi Redgold Jam na misabuni ya Doffi etc.

Kenya hakuna kiwanda cha ngano kikubwa kama AZAM. Na ubora wa bidhaa za AZAM ni wa kimataifa,kwa hiyo AZAM wamepata fursa ya kuuza bidhaa zao Kenya.
Makubaliano ni ngano ya Kenya kuuzwa Tanzania and not vice versa. Sisi tunaruhusiwa kuuza Kenya sementi na gesi tu, siyo ngano.
 
Hiyo historia uliyotoa wapi jomba? Huyo aliyekusimulia alikulisha matango pori kabisa. Kwa mfano,Tanzania,Kenya na Uganda hazijawahi kutumia sarafu moja katika historia!
Mimi nilikuwapo, si kwamba nimeisoma wapi. Tulikuwa na sarafu moja ya EA. Senti moja na senti 5 zilikuwa na tobo katikati la kuzibeba kama mshikaki. Ndiyo mambo yalikuwa hivyo mtukuu wangu. Senti moja unanunua kilo ya nyama ya ng'ombe ya kwenye ubao! Tumetoka mbali mtukuu wangu. Shillingi 5 unapata dume la makisai.
 
Hawawezi kufurukuta kwa AZAM. Bidhaa za AZAM zina viwango vya kimataifa halafu bei mteremko!
Mkuu tembea uone !
Azam ni chemicals , tupu , nenda kiwandani kwake pale mwandege , uone kama kuna mapera yanatumika inapotengenezwa guava juice , syrups , ingredients , preservatives na sukari .
 
Hawawezi kufurukuta kwa AZAM. Bidhaa za AZAM zina viwango vya kimataifa halafu bei mteremko!
Bei na viwango directly proportional😎 Bei mteremko viwango mashaka, bei juu viwango juu.
 
Huu ndio uoga wa kijinga uliomcost Nyerere alidhani akizuia bidhaa za nje viwanda vyetu vitapata solo la ndani huku akisahau kwamba sio kila malighafi atanunua kutoka ndani ya nchi hivyo angehitaji kupata soko la nje ili kupata fedha za kigeni.

Pia alisahau kwamba soko la ndani halijitoshelezi sababu consumer power ilikuwa ndogo kama sasa ilivyo.

Angalia sasa watu waliishia kununua mahitaji ya muhimu hata soda ilionekana ni anasa na hata maji ya chips ikifika wakati wenye familia kubwa walirudi kwenye kuchemsha maji ya kunywa.

Hii yote Ina maanisha kwamba, tunahitaji kutafuta masoko zaidi. Jambo la muhimu ni kutengeneza bidhaa katika ubora wenye kushindana na bidhaa zao hatushindwi tatizo tumezoea kulipua ili tuuze ndani ya nchi yetu tu.

Let's go for international markets.
 
Mkuu tembea uone !
Azam ni chemicals , tupu , nenda kiwandani kwake pale mwandege , uone kama kuna mapera yanatumika inapotengenezwa guava juice , syrups , ingredients , preservatives na sukari .
Asome tu Ile packet ataelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…