Juice na unga wa ngano kutoka viwanda vya Kenya vitaingia Tanzania bila vikwazo na sementi kutoka viwanda vya Tanzania vitaingia Kenya bila vikwazo

Juice na unga wa ngano kutoka viwanda vya Kenya vitaingia Tanzania bila vikwazo na sementi kutoka viwanda vya Tanzania vitaingia Kenya bila vikwazo

Umechelewa, tumeshaweka kidole (saini) tayari!
Bidhaa za Tanzania zinazalishwa zikiwa zimebebeshwa kodi kibao , ndo maana zinakuwa ghali, Cement ya dangote haiwezi kwemda kenya , maana ni cement ghali.sana sana cement ya kenya ndo itaingia Tanzania .

Ni funzo kwa tax systems zetu maana seriously viwanda vyetu havitaweza kushindanna na products za kenya , unless kufanyike amendments kadhaa kwenye kodi zetu.
 
Kwa nini tumekuwa waoga miaka yote hivi?ndio maana hata kwenye michezo tunafungwa Sana!?
Soma historia kama wewe ni kijana. Viwanda vyote vilivyoko Kenya vilikuwa vyetu kwa pamoja na Uganda kupitia EAC ya zamani iliyoundwa baada tu ya nchi hizi kupata uhuru. Hata hiyo currency ya shillingi ilikuwa moja. Iddi Amini Dada alipoichukua Uganda na sisi kutopenda tukawa buisy kuzozana na huyo Amini. Kenya ikachukua advantage ya mzozano huo na kujimilikisha mali zote za EAC ikiwemo hivyo viwanda na kuvunja EAC. Baada ya kumaliza mzozano huo na Iddi Amini, Tanzania (chini ya JK Nyerere) na Uganda (chini ya Kabuta Mseveni) zilijikuta hazina viwanda, usafiri wa treni wala wa ndege na wala sarafu (currency). Zilirudi back to square one hadi sindano, viberiti, sabuni, dawa ya mswaki etc ilibidi ivinunue kutoka Kenya. Sasa tulikuwa tumeanza ku pick up, hili Kenya hawapendi wanataka tubaki vile vile.
 
Azam juice amesha kamata soko labda ajichanganye tu

Sent from my TECNO CA6 using JamiiForums mobile app
Amekamata soko la Rwanda na Burundi tu, hilo la Kenya hawezi kuthubutu hata kidogo. Na hata hilo la Burundi na la Rwanda atanyang'anywa, rais wa Burundi sasa hivi yuko Kenya na yeye keshaweka dole!. Kenyatta safi!
 
Mi nasubiri maziwa ya brookside

20210602_010817.jpg
 
Cement ya dangote haiwezi kwemda kenya , maana ni cement ghali.sana sana cement ya kenya ndo itaingia Tanzania .
Kasome hayo makubaliano. Kenya wanataka hiyo sementi ya Dangote kwani grade yake ndiyo inafaa kwa ujenzi wa madaraja na maghorofa marefu. Sisi tunaweza kuletewa ile ya daraja hafifu inayozalishwa na viwanda vingi vya Kenya.
 
Yaani tutafaidi uhondo huo! Na kuna Zesta Jam, Blue Band na Omo! Tutaachana na hiyo mi Redgold Jam na misabuni ya Doffi etc. Ninakahurumia sana hako karembo ka kwenye tangazo la Doffi.

..niliwahi kumsikia waziri kabudi akisema wamalawi wanapenda sana bidhaa za tanzania, na bidhaa mojawapo aliyoitaja ni sabuni ya unga foma.

..nadhani Tz bado tunaweza kuuza bidhaa kwa majirani wetu wengine kama malawi, zambia, drc congo,..

..lingine ni kujitahidi ili gharama za uzalishaji ktk viwanda vya Tz ziwe chini kuliko majirani zetu wote. Na zaidi tujitahidi ktk kuzalisha bidhaa zenye viwango.
 
Una endorse mkataba wa EPA na EU, sisi tunapeleka nini EU hadi uruhusu bidhaa zote za EU ziingie Tz duty free ? Huyu ndio Rais atakayeua kabisa manufacturing industry ambayo ndio kwanza ilikuwa jnaanza kukomaa baada ya kazi ya muda mrefu ya Mkapa, JK na JPM.
Watamtuliza wahusika wakiona anazingua mwenzie si katulia tayari
 
Wataweza? Viwanda vya Kenya na vya European Union vina uzoefu wa miaka mingi. Nishati ya umeme kwao ni senti 0.004 ya dola kwa unit wakati sisi ni senti 20 ya dola kwa unit (= TZS 500). Sasa tunatarajia kujenga bomba la kupeleka gesi yetu kutoka Mtwara hadi Kenya kwa bei nafuu ili viwanda vyao vipate nishati ya bei nafuu zaidi ili juices zao watuuzie kwa bei nafuu zaidi.
Kama huu sio ujinga tuuite kitu gani?

Kenya atatoa wapi umeme wa senti 0.004?

Makala yenyewe ya hiyo Business Daily ni upotoshaji moja kwa moja kama ilivyo kawaida ya waandishi wa habari wa Kenya, halafu mtu analeta habari hiyo hapa kwa furaka kabisa!
 
Back
Top Bottom