Jukwaa la habari msitafute mchawi, Chanzo kikubwa cha vyombo vya habari kufa ni kukosekana "Habari za kiuchunguzi"

Jukwaa la habari msitafute mchawi, Chanzo kikubwa cha vyombo vya habari kufa ni kukosekana "Habari za kiuchunguzi"

Hayo ndio malipo na mshahara wa dhambi zao unafiki unalipwa sawia na karma mnaandika vichwa vya habari vya kipuuzi miaka 5 yote vichwa ni

Jpm gangwe
Jpm hakamatiki
Miradi kabambe ya jpm yaitisha dunia
Dunia yamkubali jpm
Marekani yamgwaya jpm
Jpm aipiga korona
Korona yamkimbia jpm
Jpm mwana wa Mungu
Jpm Kama Mungu

Hivyo ndio vichwa vya habari vya magazeti yenu Sasa kufeni kabisa wajinga nyie cc tutabaki na jamiiforums yetu.
 
Jukwaa la habari na wachambuzi mbalimbali wanadai kukosekana kwa wateja kwenye vyombo vya habari kumeletwa na teknolojia ya mitandao!

Wanadai kwamba Siku hizi watu wengi wanapata taarifa mitandaoni hivyo ndiyo maana hawanunui magazeti au kuangalia TV.

Madai kama haya hayaakisi ukweli halisi wa tatizo!

Chanzo kikuu cha kufa kwa vyombo vya habari ni ukosefu wa habari za kiuchunguzi (investigation)

Kwasababu watu wanahitaji habari halisi ili wavutiwe kutizama au kusoma magazeti!

Vyombo vya habari karibu vyote siku hizi vimekosa Investigation Journalism.

Ni kama kusifu na kupamba rangi ya nyumba pasipo kujadili nyufa nyumba!
Vyombo vingi vya habari vitapotea kama hawatajipambanua kutoa habari TECHNICAL!

Vyombo vya habari vinahoji watu walewale kama chanzo cha taarifa pasipo kujikita katika uchunguzi wa tatizo lenyewe!
Mm nitachangia kwa case ya Tv tu.
Hapa Tz tv stations nyingi ni utopolo mtupu waandishi wa habari hawa discuss issues zilizopo nchini wao kila siku ukiamka na kulala ni kumsifia kiongozi mkuu, mfano mdogo kwa jirani zetu Uganda yaan tv stations zao wana discuss issues daily yaan ukiangalia tv station kuanzia asubuh wana discuss issuea ndan ya nchi yao.
Watazungumzia mambo gender mara oil and gas, debates za issues za sanitation and hygine ktk mashule, yaan vipindi vyao vipo full package of issues jioni entertainment unapata muvies za maana sio takataka

Ila hapa tz hali ni tafauti
 
Media zinakufa sababu ya technology

Mtasingizia kila kitu
Uchawi ni internet tu
Kama kufa vingekufa vipindi vya michezo vya Radio...ambako huko ndo internet zipo na mechi zinaangaliwa...lakini kwa sasa vipindi hivyo ndo vinatusua.
Ukweli ni kwamba Habari za upande mmoja zinawafelisha Internet kisingizio tu....
 
Unaongea na still hujui unachoongea
Washington post iliuzwa Kwa kushindwa
Kupata faida ina survive now Kwa kuwa alienunua ndo mtu tajiri kuliko wote duniani
Haimpi shida kumiliki gazeti linalopata hasara

Hayo magazeti yote uliyotaja yote Yana struggle..
Mengine yana online contents na matangazo ya online
Mengine yanamilikiwa na big media houses zenye online branch na TV na kadhalika
Hakuna newspaper inayopata faida these days...
Hakuna mtu kichaa anaweza fanya biashara ambayo haina faida,come on fella,that aint gonna happen. Pamoja na kuwa yanamilikiwa na giant media groups, lakini haijawahi kuwa projected the way unavotaka kupotray hapa jamvini. Hatukatai kuwa biashara sio ya faida kila mara,lakini hayo magazeti hayajwahi kutangaza kufunga biashara zao mpaka yananunuliwa. Problem iliyopo bongo media groups zimejikita kutangaza non sense muda wote take it from me. Angalia tu kipindi cha compaign, coverage yote ilijikita kwa CCM utacikiri majority ya Watanzania wote ni CCM. Hawajui kufanya coverage, hata kama chama tawala kinaminya uhuru wa habari lakini mnakuwa wajanja kwenye kucover habari. Sometimes aweza kuta hii ni migomo tu,wengi hatuwezi jua.
 
Ingekuwa ni hivo The Telegraph, mirror washington post, Newyork post zingekuwa zimekufa, make huko ndo technology imeanzia. Watu hawajui watu wanapenda habari gani. Watu tunapenda kusoma investigative news and politics, hizi ishu za miundombinu kila mtu anajua ipo na inajengwa tena kwa kodi zetu. Sasa media zikijikita kuandika hizo habari watu wanawaona kama bunch of lunatics wanatafuta kick za uteuzi
Kweli watu wanataka habari za gizani...maendeleo yanaonekana tu..ukipita Ubungo utaona barabara juu au kama upo mkoani utaona kwenye tv.
Watu wanataka za ndani kama sakata la Trilion 1.5 na mambo kama hayo.
 
Sakata la kina halima mdee; hakuna gazeti hata moja liliaandaa Makala ya uchambuzi wa kanuni na katiba kuhusu ukweli halisi!
Wao wapo busy kusema "NDUGAI ASEMA"
Wapuuzi sana. Na watafunga wote......unaamka asubuhi unakuta gazeti kubwa la kuaminiwa (kwa jina) lina heading "19 NI WABUNGE HALALI" -NDUGAI
Hawajifunzi kitu, mbona watu tunasubiri kwa hamu kubwa kutazama Dira ya Dunia BBC?
Wafunge tu wote, praise and worship team za jiwe hizo.
 
Mimi kuna Dr mmoja nilimwambia jana, magazeti yamepoteza uhalisia wa Journalism akabisha eti oh mitandao,sikutaka kubishana nae. Huko Marekani na Western Europe watu wanasoma magazeti kwani hakuna mitandao. Ishu hapa ni hii miaka waandishi wamepoteza mwelekeo. Kila mwandishi anaangalia kama anaweza pata teuzi toka kwa kiongozi mtarajiwa wa malaika atakapokuwa huko walipo.
Imepitishwa sheria ya uandishi wa habari ambapo waandishi wengi wenye vyeti hawana uwezo wa kufanya uandishi makini.

Habari za kiuchunguzi na chambuzi zilizomakinika ni vigumu kupata kwenye media zetu ambazo zimekaa kimrengo wa vyama...
 
Wenyewe wanasema, "News is when a man bites a dog, not a dog bites a man" na Kubenea akaongeza "Rais kufungua Daraja sio habari".

Sasa kama wamekazana kuandika irrelevant issues, nani anunue?
 
Magazeti na TV Tanzania navifananisha na uharo uliooza
 
Jukwaa la habari na wachambuzi mbalimbali wanadai kukosekana kwa wateja kwenye vyombo vya habari kumeletwa na teknolojia ya mitandao!

Wanadai kwamba Siku hizi watu wengi wanapata taarifa mitandaoni hivyo ndiyo maana hawanunui magazeti au kuangalia TV.

Madai kama haya hayaakisi ukweli halisi wa tatizo!

Chanzo kikuu cha kufa kwa vyombo vya habari ni ukosefu wa habari za kiuchunguzi (investigation)

Kwasababu watu wanahitaji habari halisi ili wavutiwe kutizama au kusoma magazeti!

Vyombo vya habari karibu vyote siku hizi vimekosa Investigation Journalism.

Ni kama kusifu na kupamba rangi ya nyumba pasipo kujadili nyufa nyumba!
Vyombo vingi vya habari vitapotea kama hawatajipambanua kutoa habari TECHNICAL!

Vyombo vya habari vinahoji watu walewale kama chanzo cha taarifa pasipo kujikita katika uchunguzi wa tatizo lenyewe!
Umeongea ukweli waandishi wetu wamejikita kuwa maripota wanaandika kile wanachoambia swala la kina Mdee kama tungekuwa na waandishi mahiri tusingeishia kuwasikili Chadema, Mdee na Ndugai wangeingia ndani zaidi ya hapo.
Ukiangalia vilevile wanaotoa maoni ni walewale hawabadiliki.
Wanapenda habari za udaku wasipobadilika magazeti mengi yatakufa hata habari za michezo zinaripotiwa kutokana na mapenzi ya mwandishi au mtangazaji.
 
Umeongea ukweli wa asilimia 100. Tatzo wanaandika taarifa ambazo hata kama sijasoma gazeti nishaijua kiundani au nishahisi wanaongelea nn kwa undani. Mfano Chadema waliwavua uanachama kina mdee na wenzake taarifa ambayo nishaijua leo afu kesho unanijia na maelezo yaleyale alyoongea mbowe wakati wanavua uanachama, Sasa hapo naaja gani ya kununua gazeti. Wao ilibidi wande ndani zaidi kuchunguza sakata lenyewe na sheria zikoje na waseme ukweli sio kwa kuangalia upande mmoja afu mwingine wanaufumbia macho.
 
Habari za ziara za viongozi Singida zinamsaidia nini msomaji wa Tandahimba? Wanaacha kuandika mambo ya kulisaidia Taifa wanakalia kusifu na kuabudu mtu. Ndo wqjue waliokuwa wananunua magazeti yao siyo praise team, ni watu wenye uelelwa wanaotaka kujua kinachoendelea kiuahalisia. Na kilichowaua zaidi ni taarifa mbovu kuhusu uchaguzi.
 
Hakika
 
Jukwaa la habari na wachambuzi mbalimbali wanadai kukosekana kwa wateja kwenye vyombo vya habari kumeletwa na teknolojia ya mitandao!

Wanadai kwamba Siku hizi watu wengi wanapata taarifa mitandaoni hivyo ndiyo maana hawanunui magazeti au kuangalia TV.

Madai kama haya hayaakisi ukweli halisi wa tatizo!

Chanzo kikuu cha kufa kwa vyombo vya habari ni ukosefu wa habari za kiuchunguzi (investigation)

Kwasababu watu wanahitaji habari halisi ili wavutiwe kutizama au kusoma magazeti!

Vyombo vya habari karibu vyote siku hizi vimekosa Investigation Journalism.

Ni kama kusifu na kupamba rangi ya nyumba pasipo kujadili nyufa nyumba!
Vyombo vingi vya habari vitapotea kama hawatajipambanua kutoa habari TECHNICAL!

Vyombo vya habari vinahoji watu walewale kama chanzo cha taarifa pasipo kujikita katika uchunguzi wa tatizo lenyewe!

Msaki Habari leo imemfia mkononi. Madoido yote yale, no innovation
 
Chanzo cha vyombo vya habari kufa ni hiki hapa.Unalijua hilo,nalijua hilo na wanalijua hilo.Achana na simulizi za Alfu Lela U Lela!
0659010.jpg
 
Jukwaa la habari na wachambuzi mbalimbali wanadai kukosekana kwa wateja kwenye vyombo vya habari kumeletwa na teknolojia ya mitandao!

Wanadai kwamba Siku hizi watu wengi wanapata taarifa mitandaoni hivyo ndiyo maana hawanunui magazeti au kuangalia TV.

Madai kama haya hayaakisi ukweli halisi wa tatizo!

Chanzo kikuu cha kufa kwa vyombo vya habari ni ukosefu wa habari za kiuchunguzi (investigation)

Kwasababu watu wanahitaji habari halisi ili wavutiwe kutizama au kusoma magazeti!

Vyombo vya habari karibu vyote siku hizi vimekosa Investigation Journalism.

Ni kama kusifu na kupamba rangi ya nyumba pasipo kujadili nyufa nyumba!
Vyombo vingi vya habari vitapotea kama hawatajipambanua kutoa habari TECHNICAL!

Vyombo vya habari vinahoji watu walewale kama chanzo cha taarifa pasipo kujikita katika uchunguzi wa tatizo lenye

Duniani kote hakuna chombo cha habari chochote kilichowahi kufanikiwa kukubalika kwa kujipendekeza kwa Serikali tu mda woote...sana sana huwa wanaojipendekeza huwa wanapata raha za muda mfupi lakini impact huwa ni mbaya kupita kiasi kwa mda mrefu. Wengi wetu siku hizi tumeacha kabisa kusoma magazeti ya nchini...mara ya mwisho nakumbuka kununua gazeti la Tanzania Daima kabla halijapotezwa...Kwa upande wa TV siku hizi mie na DSTV..DSTV na mie..AZAM nimeibakiza kwa ajili ya kuangalia mechi za Simba na Yanga au Simba wakienda kimataifa.. vinginevyo silipii tena AZAM Kifurushi. Leo kwa mfano nimestuka nataka kulipia kifurushi cha 18,000 (7,000) kwa wiki kusudi niangalie mechi ya Simba kwa leo tu nikaambiwa kimepada mpaka (20,000) yaani 9,000 kwa wiki...basi nikalipia tu kifurushi cha wilki ila kwa ajili ya mechi ya leo..baada ya hapo narudi zangu DSTV ...
 
Back
Top Bottom