Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
TAARIFA KWA UMMA
JUKATA kwa majonzi makubwa inatoa pole za dhati kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote ambao wapendwa wao wameuawa, kujeruhiwa au kutoweka wakati wa maandamano yaliyozuka siku ya uchaguzi tarehe 29/10/2025. Tunalaani vikali vitendo vya kikatili vya kuwapiga risasi wananchi wasio na hatia wengi wao vijana wa kizazi cha Gen Z. Mauaji haya ya kinyama yameharibu maisha ya Watanzania, kudhalilisha nchi yetu kimataifa na yataathiri vibaya uchumi wa taifa letu. Maafa haya ni ya kujutia sana kwani ni matokeo ya viongozi wenye dhamana kupuuza malalamiko na matakwa ya msingi ya wananchi kwa muda mrefu.
1. MAELEZO YA VITENDO VYA UKATILI
2. UKOSEFU WA UHALALI WA KUTUMIA SILAHA ZA MOTO
Matumizi ya nguvu ya kikatili yanakiuka:
1. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977
Kilichofanyika sio tu ni uhalifu wa kisheria, bali ni unyama dhidi ya binadamu unaostahiki uchunguzi wa kimataifa.
3. MADAI YA MSINGI YA WANANCHI
Watanzania wamedai kwa muda mrefu:
Serikali inawajibika kuanza mara moja kutimiza madai haya badala ya kuwakamata kiholela na kuwafungulia mashataka wanaoshukiwa kuwa walifanya fujo huku viongozi wa upinzani. wakilengwa zaidi. Hii ni dhulma inayozidisha chuki, na mgawanyiko kiasi cha kuzua machafuko tena.
4. HATUA ZA HARAKA KUCHUKULIWA
Kwa niaba ya JUKATA

- Wakati wa maandamano ya amani ya Watanzania waliokuwa wamekasirishwa na hali ya mambo nchini, vyombo vya dola vilitumia nguvu isiyo na mipaka na ya kikatili, ikiwemo risasi za moto zilizopigwa kiholela kwa waandamanaji na wasio waandamanaji.
- Watanzania wengi wameuawa, wengine wamejeruhiwa vibaya, na wengine wametoweka bila kujulikana waliko.
- Uthibitisho: Picha, video, shuhuda na vilio vya wananchi wanaowatafuta au kuwaomboleza wapendwa wao vinasambaa kwenye mitandao ya kijamii.
2. UKOSEFU WA UHALALI WA KUTUMIA SILAHA ZA MOTO
Matumizi ya nguvu ya kikatili yanakiuka:
1. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977
- Ibara ya 14 (haki ya kuishi)
- Ibara ya 18 (uhuru wa kujieleza)
- Ibara ya 20 (uhuru wa kukusanyika)
Matumizi ya nguvu yanapaswa kuwa ya mwisho na yenye uwiano. Ushahidi wa picha mnato,picha mjongeo na shuhuda mbalimbali unaonyesha risasi zilipigwa kiholela kwa lengo la kuua - hata kwa waliokuwa majumbani mwao.
3. Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa (ICCPR) ambapo Tanzania ni mwanachama.
Kilichofanyika sio tu ni uhalifu wa kisheria, bali ni unyama dhidi ya binadamu unaostahiki uchunguzi wa kimataifa.
3. MADAI YA MSINGI YA WANANCHI
Watanzania wamedai kwa muda mrefu:
a. Katiba Mpya ya Wananchi inayotokana na maoni ya umma.
b. Tume Huru ya Uchaguzi isiyo na upendeleo wa serikali.
c. Mazingira huru na salama ya kisiasa na kiraia yaisyo na vitisho, uonevu na ukandamizaji,
Serikali inawajibika kuanza mara moja kutimiza madai haya badala ya kuwakamata kiholela na kuwafungulia mashataka wanaoshukiwa kuwa walifanya fujo huku viongozi wa upinzani. wakilengwa zaidi. Hii ni dhulma inayozidisha chuki, na mgawanyiko kiasi cha kuzua machafuko tena.
4. HATUA ZA HARAKA KUCHUKULIWA
a. Uchunguzi wa kina na wa kimataifa kufanyika na Tume Huru (pamoja na wataalamu wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika).
b. Kuchukuliwa hatua za kisheria wote waliopanga, kufadhili na kutekeleza mauaji bila kujali cheo
c. Fidia kwa familia zilizofiwa, waliopata ulemavu na waliopoteza mali.
d. Kuanzishwa mara moja kwa mchakato wa Katiba Mpya utakaoleta suluhu ya matatizo ya msingi nay a muda mrefu ya kimfumo yanayolamikiwa ikiwemo:
- Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi
- Muundo wa Muungano
- Mgawanyo wa Madaraka
- Maadili katika Utawala
Kwa niaba ya JUKATA