SI KWELI Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limetoa taarifa kwa umma likiishutumu LHRC kwa ubaguzi wakati wa kutetea haki za binadamu

SI KWELI Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limetoa taarifa kwa umma likiishutumu LHRC kwa ubaguzi wakati wa kutetea haki za binadamu

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limeeleza masikitiko yake na kulaani vitendo vya upendeleo vinavyodaiwa kufanywa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC). TEF limezitaka taasisi zote zinazojihusisha na haki za binadamu, kama LHRC, kulaani vitendo vya ukiukwaji wa haki bila kuegemea upande wowote.

TEF imetoa wito kwa LHRC kutoa kauli ya wazi dhidi ya mauaji, utekaji, na vitendo vya ukiukwaji wa haki kwa watu wasio na hatia. Pia, TEF imeshauri LHRC kufanya maboresho ya kimkakati ili kuepuka upendeleo wa aina yoyote unaoweza kudhoofisha lengo lake la kutetea haki kwa uwazi na usawa.

TEF inaamini kuwa hatua hii ni muhimu katika kujenga jamii yenye misingi bora ya haki na usawa kwa wote.

TEF SI KWELI (1).jpg
 
Tunachokijua
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) ni taasisi isiyo ya kiserikali inayoundwa na wanachama wa kujitolea wa wahariri, viongozi wa vyombo vya habari, wanahabari wazoefu na wakufunzi wa uandishi wa habari kutoka jumuiya ya wanahabari Tanzania. Vilevile TEF inatetea uhuru wa kujieleza na kukuza weledi, ubora, uendelevu, maadili na mabadiliko katika vyombo vya habari vya Tanzania.

TEF imekuwa ni moja ya taasisi ambazo zimekua zikipigania uhuru wa vyombo vya habari ili kuchochea upatikanaji wa taarifa kwa wananchi, mathalani Oktoba 02, 2024 Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitoa taarifa ya kusitisha kwa siku 30 leseni za huduma za maudhui mtandaoni za kampuni ya Mwananchi Communications Limited kutoa huduma za maudhui mtandaoni nchini, TEF ilikuwa ni moja taasisi zilizoonesha kushtushwa na uamuzi huo huku wakilalamikia sheria kutoa mamlaka makubwa kwa wakuu wa taasisi ambayo yamekuwa yakitumika kuminya uhuru wa habari.

Kadhalika imekuwa ikiangazia masuala mbalimbali ambayo yamekuwa yakitokea nchini huku ikitoa matamko yenye mapendekezo ya nini kifanyike ili kuimarisha demokrasia, utawala bora, usimamizi wa haki za binadamu nk.

Kumekuwapo na barua inayosambaa mtandaoni ikidaiwa kutolewa na TEF ikiwa na kichwa cha habari kinachosema “Taarifa ya kulaani vitendo vya kibaguzi katika utetezi wa haki za binadamu”

Je, ni upi uhalisia wa barua hiyo?

Ufualitiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa barua hiyo haijatolewa na Jukwaa la wahariri Tanzania TEF, vilevile haijachapishwa kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii.

Aidha barua hiyo ambayo imekuwa ikisambazwa kwa kutumia nembo (logo) na utambulisho wa vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo Wasafi Media, Mwananchi na Watetezi TV, ambavyo pia havijachapisha taarifa hiyo katika kurasa rasmi bali wapotoshaji wametumia utambulisho wa vyombo hivyo ili kuwaaminisha wananchi taarifa ambayo si ya kweli. Rejea hapa, hapa na hapa.

Barua hiyo isiyo ya kweli imeonesha kukilalamikia Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ikidai kuwa na ubaguzi katika wakati wa kutetea haki za binadamu, ikitaja ukimya, na upendeleo kwa baadhi ya matukio yanayotokea katika jamii. Tuhuma hizi zinaonekana kuwa si za kweli kwa LHRC kwani imekuwa mstari wa mbele katika kukemea matukio mbalimbali nchini yanayovunja haki za binadamu bila ubaguzi. Rejea hapa baadhi ya matamko ya LHRC kukemea ukamataji unaofanywa na Jeshi la polisi bila kuzingatia sheria, tamko dhidi ya mauaji ya Christina Kibiki, katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, tamko kupinga kauli zenye mlengo wa mgawanyo wa kidini.

Hivyo barua hiyo si ya kweli na haijatolewa na TEF, imetengenezwa na watu wenye nia ovu ya kuupotosha umma.​
🛑 HABARI MPASUKO:

TEF WALAANI VITENDO VYA KIBAGUZI KATIKA UTEKELEZAJI WA HAKI ZA BINADAMU KWA BAADHI YA MASHIRIKA YA KIJAMII WAKIWEMO LHRC NA THRDC
 
Attachments

  • IMG-20241206-WA0673(2).jpg
    IMG-20241206-WA0673(2).jpg
    289.5 KB · Views: 9
  • IMG-20241206-WA0668(1).jpg
    IMG-20241206-WA0668(1).jpg
    193.3 KB · Views: 6
View attachment 3170547
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limeeleza masikitiko yake na kulaani vitendo vya upendeleo vinavyodaiwa kufanywa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC). TEF limezitaka taasisi zote zinazojihusisha na haki za binadamu, kama LHRC, kulaani vitendo vya ukiukwaji wa haki bila kuegemea upande wowote.

TEF imetoa wito kwa LHRC kutoa kauli ya wazi dhidi ya mauaji, utekaji, na vitendo vya ukiukwaji wa haki kwa watu wasio na hatia. Pia, TEF imeshauri LHRC kufanya maboresho ya kimkakati ili kuepuka upendeleo wa aina yoyote unaoweza kudhoofisha lengo lake la kutetea haki kwa uwazi na usawa.

TEF inaamini kuwa hatua hii ni muhimu katika kujenga jamii yenye misingi bora ya haki na usawa kwa wote.
SItaki hata kupoteza muda na MB zangu kusoma vitu kama hivi
 
Back
Top Bottom