Jukwaa la Wakristo vs CCM nani zaidi?

Jukwaa la Wakristo vs CCM nani zaidi?

lendila

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2012
Posts
5,806
Reaction score
4,370
Leo katika makanisa yote ya kikrstor tumesomewa waraka wa kichungaji au kwa jina lingine unaweza kuwiita waraka wa kinabidii,waraka huo ulibeba maudhui mengi mazuri sana lkn kilichonifurahisha ni wakristo wote nchini tanzania kuhamasisha kujiandikisha kwa wingi katika daftari la wapiga kura ili tuweze kupiga kura ya hapana kwenye rasim ya chenge
sasa mm nauliza wanajamii kati ya ccm na jukwaa la wakristor tanzania ipi taasisi yenye nguvu na ushawishi tanzania?
 
Mbona unauliza majibu?

Tangu lini Sungura akalinganishwa na Tembo kwa ukubwa?!

You must be kidding!
 
Karibia nusu ya wanafisiemu ni wakristo.
 
leo katika makanisa yote ya kikrstor tumesomewa waraka wa kichungaji au kwa jina lingine unaweza kuwiita waraka wa kinabidii,waraka huo ulibeba maudhui mengi mazuri sana lkn kilichonifurahisha ni wakristo wote nchini tanzania kuhamasisha kujiandikisha kwa wingi katika daftari la wapiga kura ili tuweze kupiga kura ya hapana kwenye rasim ya chenge
sasa mm nauliza wanajamii kati ya ccm na jukwaa la wakristor tanzania ipi taasisi yenye nguvu na ushawishi tanzania?

pepo litakuwa limewatembelea hao, mtu mcha mungu hawezi kukana kuheshimu mamlaka ya dunia, hata biblia inawataka viongozi wa dini na hata waumini kutii mamlaka za duniani. Wanatakiwa kuombewa hao ili pepo hilo liwatoke.
 
Leo katika makanisa yote ya kikrstor tumesomewa waraka wa kichungaji au kwa jina lingine unaweza kuwiita waraka wa kinabidii,waraka huo ulibeba maudhui mengi mazuri sana lkn kilichonifurahisha ni wakristo wote nchini tanzania kuhamasisha kujiandikisha kwa wingi katika daftari la wapiga kura ili tuweze kupiga kura ya hapana kwenye rasim ya chenge
sasa mm nauliza wanajamii kati ya ccm na jukwaa la wakristor tanzania ipi taasisi yenye nguvu na ushawishi tanzania?

Jukwaa ka Wakristo sio Miungu watu, hawawezi kuwaamulia masuala kama hayo, hao ni watumishi wa Mungu, rejea kauli aliyoitoa Kadinali Pengo 15/03/2015.
 
Leo katika makanisa yote ya kikrstor tumesomewa waraka wa kichungaji au kwa jina lingine unaweza kuwiita waraka wa kinabidii,waraka huo ulibeba maudhui mengi mazuri sana lkn kilichonifurahisha ni wakristo wote nchini tanzania kuhamasisha kujiandikisha kwa wingi katika daftari la wapiga kura ili tuweze kupiga kura ya hapana kwenye rasim ya chenge
sasa mm nauliza wanajamii kati ya ccm na jukwaa la wakristor tanzania ipi taasisi yenye nguvu na ushawishi tanzania?

Sii jukumu la jukwaa la wakristo kuwaamulia waumini wao juu ya mustakabali wa taifa lao. Wananchi wenyewe wanauelewa wa kutosha juu ya nini wanapaswa kufanya ili nchi iendelee kuwa ya amani. Acha tabia ya kuchonganisha Watanzania. Katiba ni ya watu wote wenye dini na wasio na dini, wenye vyama na wasiona vyama. Ni jukumu letu kuwaelimisha wananchi waweze kufanya uamuzi sahihi.
 
pepo litakuwa limewatembelea hao, mtu mcha mungu hawezi kukana kuheshimu mamlaka ya dunia, hata biblia inawataka viongozi wa dini na hata waumini kutii mamlaka za duniani. Wanatakiwa kuombewa hao ili pepo hilo liwatoke.

Hata mamlaka ya Nebukadneza na Farao tuitii?
 
Biblia Takatifu katika Kitabu cha WARUMI 13, Viongozi wa Dini wanaambiwa kuheshimu na kutii Mamlaka kwa maana mamlaka zote zinatoka kwa Mungu. Aya yenyewe inasema hivi, "Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu. [SUP]2 [/SUP]Kwa hiyo anayepinga mamlaka inayotawala ana pinga chombo kilichowekwa na Mungu; na watu wanaoasi watajiletea hukumu. [SUP]3 [/SUP]Kwa maana watawala hawatishi watu wanaotenda mema bali wale wanaotenda maovu. Kama hupendi kuishi kwa kumwogopa mwenye mamlaka, basi tenda mema naye atakusifu. [SUP]4 [/SUP]Maana mwenye mamlaka ni mtumishi wa Mungu kwa manufaa yako. Lakini kama ukitenda maovu, basi ogopa kwa maana hatembei na silaha bure. Yeye ni mtumishi wa Mungu anayetekeleza adhabu ya Mungu juu ya watenda maovu. [SUP]5 [/SUP]Kwa hiyo ni lazima kutii wenye mamlaka, si kwa sababu ya kuogopa adhabu tu bali pia kwa ajili ya dhamiri.
 
Hatujadili utii unaoufikiria wewe, kasome biblia katika hiyo sehemu inayomwataka viongozi wa dini na waumini kuzitii mamlaka za duniani, lakini pia tafuta sehemu Yesu aliposema ya Kaisari mwachie kaisari na ya Mungu mpe Mungu.

Naelewa vizuri sana,inaposema kuwa ya Mungu mpe Mungu na Kaisari mpe kaisari biblia inatutaka Tuwajibike kiroho kwa Mungu lakini pia tuwajibike kwa mamlaka iliyopo juu yetu kama kulipa kodi n.k

ILA sii kwa namna ya kuitii na kukubaliana na mamlaka iliyoweka kwa namna ya ukandamizaji na dhuluma kwa wananchi wanyonge.Hiyo ni sawasawa na waliyoyafanya Mafarisayo kwa unafiki wao. Soma biblia ila omba upate tafsiri sahihi pia.
 
Ndo maana nimekuwekea mstari unahusiana na ishu uloitaka, isome na kama una hoja zaidi weka ujibiwe, tusibase katika dini lete hoja zinazohusiana na Katiba nikuelimishe.
 
Biblia Takatifu katika Kitabu cha WARUMI 13, Viongozi wa Dini wanaambiwa kuheshimu na kutii Mamlaka kwa maana mamlaka zote zinatoka kwa Mungu. Aya yenyewe inasema hivi, "Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu. [SUP]2 [/SUP]Kwa hiyo anayepinga mamlaka inayotawala ana pinga chombo kilichowekwa na Mungu; na watu wanaoasi watajiletea hukumu. [SUP]3 [/SUP]Kwa maana watawala hawatishi watu wanaotenda mema bali wale wanaotenda maovu. Kama hupendi kuishi kwa kumwogopa mwenye mamlaka, basi tenda mema naye atakusifu. [SUP]4 [/SUP]Maana mwenye mamlaka ni mtumishi wa Mungu kwa manufaa yako. Lakini kama ukitenda maovu, basi ogopa kwa maana hatembei na silaha bure. Yeye ni mtumishi wa Mungu anayetekeleza adhabu ya Mungu juu ya watenda maovu. [SUP]5 [/SUP]Kwa hiyo ni lazima kutii wenye mamlaka, si kwa sababu ya kuogopa adhabu tu bali pia kwa ajili ya dhamiri.

".....Wafalme wakitenda yasiyo HAKI ni chukizo, Maana kiti cha enzi huthibitika kwa HAKI....."-Mithali 16:12
 
Wakristo wa madhehebu yote tuungane kuikataa kata kata KATIBA PENDEKEZWA. Katiba pendekezwa imeacha mambo ya msingi kama Mbunge kutokuwa Waziri, Muda wa Mbunge, Tunu za Taifa, maadili ya viongozi, Wananchi kumwajibisha mbunge wao nk. KATAENI KATA KATA.
 
Tulishaikataa siku nyingi tunasubiri kupiga kura ya HAPANA!
 
Sii jukumu la jukwaa la wakristo kuwaamulia waumini wao juu ya mustakabali wa taifa lao. Wananchi wenyewe wanauelewa wa kutosha juu ya nini wanapaswa kufanya ili nchi iendelee kuwa ya amani. Acha tabia ya kuchonganisha Watanzania. Katiba ni ya watu wote wenye dini na wasio na dini, wenye vyama na wasiona vyama. Ni jukumu letu kuwaelimisha wananchi waweze kufanya uamuzi sahihi.
Vp kuhusu mahakama ya kadhi IPO???
 
Back
Top Bottom