Pre GE2025 Juliana Masaburi: Yaliyofanywa na Rais Samia Yanatosha Kuendelea Kuiamini CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

JULIANA MASABURI: YALIYOFANYWA NA RAIS SAMIA YANATOSHA KUENDELEA KUIAMINI CCM

Mbunge wa Viti Maalum Vijana Tanzania, Mhe. Juliana Didas Masaburi akihutubia mkutano wa hadhara amewaambia wananchi kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imefanya kazi kubwa hivyo kukifanya Chama Cha Mapinduzi kuendelea kuaminiwa kupewa dhamana ya wananchi kuongoza Serikali

Mbunge Masaburi amefanya Mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kibosho, Kata ya Kisutu Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani na ameendelea kuwanadi na kuwaombea kura za kishindo Wagombea wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Unaotarajiwa Kufanyika tarehe 27 Novemba, 2024.

"Serikali imejenga Vituo vya Afya 367 na Majengo ya Zahanati 980. Imefikisha Umeme Vijijini kwa asilimia 96.37% hivyo kufanya Vijiji 11,837 kati ya Vijiji 12,318 kupata huduma ya umeme. Zimejengwa Shule mpya za Msingi na Sekondari 3,631 na jumla ya Madarasa mapya 21,912" Amesema Juliana Didas Masaburi, Mbunge wa Viti Maalum Vijana Tanzania

Vilevile, Juliana Masaburi amezindua Shina la Njia Panda ya Vikawe, Kata ya Mapinga la Umoja wa Vijana wa CCM ambalo amelizindua rasmi tarehe 23.11.2024

#KaziIendelee
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-11-24 at 10.40.00.jpeg
    93.9 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-11-24 at 10.40.01.jpeg
    117.6 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-11-24 at 10.38.46.jpeg
    174.6 KB · Views: 5
Binti anawaza kama Mh. Masabauri, kupitia ile formula yake maarufu.
 
Kweli aliyoyafanya Samia yanatosha, kamuua Soka na Kibao ccm oyeeeeeeee
 
Huu ndo ujinga ,Rais hafanyi kwa mapenzi yake anatekeleza ilani ya chama chake ila pia kodi za wananchi. ,Rais ndani ya chama ni mdogo kama Puriton, hatoi pesa zake mfukoni tekeleza kile anataka ,bali hutekeleza tokana na kodi za wananchi .
Ccm vilaza sana kama hata mambo madogo hawawezi kuvavaduua ,pumbavu period
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…