Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Kwenye ukurasa wake wa facebook,Mtatiro ameandika ujumbe ufuatao akiwatuhumu mawaziri wa CCM kuhujumu mchakato wa katiba mpya.
Mh.Mtatiro ameandika:
Jana waziri Maghembe amewaita wawakilishi wa wafugaji waliomo kwenye bunge la katiba,amewaandalia chakula cha kutosha,vinywaji vya kutosha na viburudisho vingine,huku wakipewa bahasha za nauli baada ya vikao vya siri.
Waziri wa elimu,Shukuru Kawambwa,jana pia amewaita wawakilishi wa vyuo vya elimu ya juu walioko katika bunge la katiba na kuendelea na mchezo huo.
Mhe.Lowassa pia leo amekutana na wafugaji na wakulima walio wajumbe wa bunge la katiba kwa mfumo huo huo.
Hoja zao wanapokutana na makundi hayo ni kupiga chapuo kura ya wazi na kupinga ya siri,huku wakieleza namna CCM inavyopinga baadhi ya mapendekezo muhimu yaliyomo katika rasimu ya katiba.
Mh.Mtatiro ameongeza kuwa,wanachofanya mawaziri hawa ndicho kinachofanywa na mawaziri wengine wa CCM,ni agizo la lazima ambalo hivi sasa linatumika hapa Dodoma.
Leo,CCM na mawaziri wanatumia fedha na kutoa rushwa ili kupitisha matakwa yao.Masuala haya yana ushahidi,kesho nitayasema bungeni kwa uwazi kabisa.
MY TAKE:
Hizi ni tuhuma nzito sana!
Je,TAKUKURU wanachukua hatua gani?
Je,Raisi Kikwete hajua kinachoendelea?
Je,ni kweli Raisi Kikwete ana nia njema ya kupata katiba mpya kama anavyosifiwa?
Yetu macho na masikio!