Julius Mtatiro: Mawaziri wa CCM wanaendesha vikao vya siri na kugawa bahasha kwa wajumbe!

Julius Mtatiro: Mawaziri wa CCM wanaendesha vikao vya siri na kugawa bahasha kwa wajumbe!

Majaji wa mahakama wanateuliwa na mwenyekiti wa CCM aliyepo madarakani. Upo hapo?

Nchi hii solution pekee ni mapinduzi kama ya Misri,Libya na Tunisia.

CCM hawawezi kutoka madarakani kupitia sanduku la kura!

CCM watabaka mchakato huu ili wapate katiba itakayowasaidia wao kubaki madarakani.
 
naludia kusema CCM hawana nia ya dhati na njema kwa taifahili wao wanajali vyeo ,na kuungwa mkono,viva Mtatiro walipue tu ndio maana Mwalimu Nyerere alipinga sana rushwa kwa vitendo sio JK na genge lao la ccm kazi kubwa ni kutoa rushwa kwa mashinikizo na maagizo ya chama.
ndugu SITTA simamia haya kwa uwazi ili watanzania tujue tupo na nani na nani yupo genge gani
ili 2015 tufanye maamuzi ya busara
 
Porojo tu na maneno ya vijiwe vya chai

Wewe unasema ni porojo! Mtikila kajionea mapema kuwa hili ni bunge la kihuni halijapata kutokea, namwamini Mtikila katika hilo 100%. Wala msihangaike kumuuliza rais, anayajua yote vizuri tu. Ngoja sisi tunaoamini kwamba kila chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho tuangalie CCM wanavyopambana kuzuia mwisho wao usitokee kama watafanikiwa.
 
Hizo ndizo true colours za CCM.......The end justify the means. Iwe kwa rushwa, vitisho, ulaghai na namna nyingine yoyote.
 
Hiki chama cha c.c.yem kilaaniwe kwa kuhodhi mchakato mzima wa katiba yetu tuitakayo na pia hao wahusika nawaombea mungu awavune vyema kwani wamekuwa ni miti isiyo na matunda mbele za mungu!

Akina majembe,kalambwa na lowaza wanaenda kufanya nini makanisani na misikitini ikiwa wana roho mbaya kiasi hiki?

hata hiyo mijitu iliyoenda kuwakilisha makundi ina njaa sana! I wonder kwamba laki 3 per day, still wana price tag!! Hii nchi ina tatizo kubwa si kwa viongozi pekee bali hata kwa wananchi wenyewe. Usishangae wakati wa kupiga kura ya kuipitisha watanzania wakapewa hongo za vyakula na kapero, kanga n.k wakaipitisha!
 
Da watu wamemsahau Mungu kabisa ila viongozi na waTz ni wanafiki.Kwenye nyumba za ibada wanajazana kama kumuomba Mungu vile kumbe wameenda kama fasheni.
 
go go mtatiro, nilishasema tusitegemee katiba mpya chini ya ccm, bora bunge livunjwe tu, yani hao wajumbe wakitoka huko ni matajiri maana watakula pesa za ccm mpaka basi, na ccm wameshajua wananchi wana njaa, ndio maana utumia pesa kuwanunua, ndio maana pia hawataki kuwapa maendeleo ili wabaki na njaa yao.
 
Takukuru watakuwa wanakaz gan kila lisemwalo na wanasiasa lisiwape usingiz?chakula kumualika MTU c dhamb yy anahic km ananjaa akale uyo mapua
 
Majaji wa mahakama wanateuliwa na mwenyekiti wa CCM aliyepo madarakani. Upo hapo?

Ambae alikiendesha kikao cha nec kilichotoka na msimamo wa kuhakikisha muungano wa serikali mbili unaendelea..!
 
CCM wanapotamka neno "wananchi" wanamaanisha "wanaCCM".Sisi wengine tulie tu! kwa hiyo wakisema Serikali Tatu sio maoni ya "wananchi", mjue kuwa hao wananchi ni wale wa kwao tu.CCM imeshatugawa watanzania.wanatumia "divide and rule" principles katika hili. Hebu ifike mahali, tujitafakari kwa kina, tuangalie tulipotoka, tulipo sasa, na tunapotaka kwenda, na kisha tufanye uamuzi wa dhati kabisa toka mioyoni mwetu, ni TAIFA la namna gani tunalihitaji. Sababu tunayo, Uwezo Mwenyezi Mungu katujalia Tunao, na NIA hiyo pia Tunayo, tumpige adui vita, huyu adui UBAGUZI,RUSHWA, UMASIKINI,DHULUMA, MABAVU, na ULEVI WA MADARAKA!
 
CCM ni zaidi ya shetani...
 
Mkiona hali sio nzuri mtoke (msuse)mrudi kwa wenye inchi. Sisi tutajua cha kufanya.
 
Ambae alikiendesha kikao cha nec kilichotoka na msimamo wa kuhakikisha muungano wa serikali mbili unaendelea..!

We acha tu. Yaani kazi tunayo sana sisi walipa kodi wa nchi hii tukufu
 
wanatoa rushwa kwasababu wanajua rasimu ya katiba iliyowasilishwa na tume ya jaji Warioba ni chungu kwao kwa maana wengi baada ya 2015 watakuwa nje ya uongozi.
hongera Mtatiro wewe ni mpiganaji
 
Back
Top Bottom