Julius Mtatiro: Mawaziri wa CCM wanaendesha vikao vya siri na kugawa bahasha kwa wajumbe!

Julius Mtatiro: Mawaziri wa CCM wanaendesha vikao vya siri na kugawa bahasha kwa wajumbe!

wanatoa rushwa kwasababu wanajua rasimu ya katiba iliyowasilishwa na tume ya jaji Warioba ni chungu kwao kwa maana wengi baada ya 2015 watakuwa nje ya uongozi.
hongera Mtatiro wewe ni mpiganaji

Well said.
 
Niliangalia bunge jana kwa kweli ni aibu tupu! Yule Werema sijui kichwani mwake kuna nini!
 
MAWAZIRI Profesa Jumanne Maghembe (Maji) na Dk. Shukuru Kawambwa (Elimu na Mafunzo ya Ufundi), wanadaiwa kuwahonga makundi ya wafugaji, wavuvi na wawakilishi wa elimu ya juu ili washikilie msimamo wa kupigwa kura ya wazi.Mawaziri hao wanadaiwa kushiriki njama hizo baada ya kuona kundi kubwa la wapinzani linalotaka ipigwe kura ya siri kuamua masuala mbalimbali wameanza kuungwa mkono na makundi maalumu ambayo yana wajumbe 201.
Viongozi hao wanadaiwa pia kuyashawishi makundi hayo waunge mkono muundo wa serikali mbili pamoja na kupinga taarifa kinzani ambayo inatoa fursa kwa mawazo ya wajumbe wachache kusomwa ndani ya Bunge na kujadiliwa.
mawaziri1.jpg
 
Nchi yetu haina serikali hivyo dola letu ni kama mbwa koko halina uwezo wa kung'ata japo linabweka sana. Mawaziri endeleeni kutoa rushwa. Kwanza nani kawaambia hawa watu kuwa takrima ni rushwa?
.
 
Hivi upigaji kura umamuliwa vipi (Siri au adharani?)
 
Hivi kweli maprofesa waliochaguliwa huko wanakubali kutumika kwa kuhongwa na wachumia tumbo? Profesa wangu Romuald Haule unaweza kweli ukatumika na Kawambwa?Napata shida sana kujua hizo.
 
Kwenye ukurasa wake wa facebook,Mtatiro ameandika ujumbe ufuatao akiwatuhumu mawaziri wa CCM kuhujumu mchakato wa katiba mpya.

Mh.Mtatiro ameandika:

Jana waziri Maghembe amewaita wawakilishi wa wafugaji waliomo kwenye bunge la katiba,amewaandalia chakula cha kutosha,vinywaji vya kutosha na viburudisho vingine,huku wakipewa bahasha za nauli baada ya vikao vya siri.

Waziri wa elimu,Shukuru Kawambwa,jana pia amewaita wawakilishi wa vyuo vya elimu ya juu walioko katika bunge la katiba na kuendelea na mchezo huo.
Mhe.Lowassa pia leo amekutana na wafugaji na wakulima walio wajumbe wa bunge la katiba kwa mfumo huo huo.

Hoja zao wanapokutana na makundi hayo ni kupiga chapuo kura ya wazi na kupinga ya siri,huku wakieleza namna CCM inavyopinga baadhi ya mapendekezo muhimu yaliyomo katika rasimu ya katiba.

Mh.Mtatiro ameongeza kuwa,wanachofanya mawaziri hawa ndicho kinachofanywa na mawaziri wengine wa CCM,ni agizo la lazima ambalo hivi sasa linatumika hapa Dodoma.

Leo,CCM na mawaziri wanatumia fedha na kutoa rushwa ili kupitisha matakwa yao.Masuala haya yana ushahidi,kesho nitayasema bungeni kwa uwazi kabisa.

MY TAKE:
Hizi ni tuhuma nzito sana!
 
Watanzania ni nani aliyewaroga? Piga chini CCM
 
Kazi kweli kweli, hilo bunge la katiba halina maana tena bora livunjike, kule Kenya bunge la katiba hawa watu mawaziri na wabunge kwenye mchakato wa bunge la katiba waliwekwa nje kwa kuhofia mambo haya haya., sasa huku ni kuwaumiza wananchi wanaoteseka mda mrefu kwa maslahi ya wachache CCM ni zaidi ya Wakoloni
 
Kama tumeituma misukule itakubali itahongwa na itahujumu katiba, lakini kama tumetuma watu, watafanya kazi, hakika ccm ni mashetani, na bila kusahau, hizo hela ni kodi zetu.
 
Kwenye ukurasa wake wa facebook,Mtatiro ameandika ujumbe ufuatao akiwatuhumu mawaziri wa CCM kuhujumu mchakato wa katiba mpya.

Mh.Mtatiro ameandika:

Jana waziri Maghembe amewaita wawakilishi wa wafugaji waliomo kwenye bunge la katiba,amewaandalia chakula cha kutosha,vinywaji vya kutosha na viburudisho vingine,huku wakipewa bahasha za nauli baada ya vikao vya siri.

Waziri wa elimu,Shukuru Kawambwa,jana pia amewaita wawakilishi wa vyuo vya elimu ya juu walioko katika bunge la katiba na kuendelea na mchezo huo.
Mhe.Lowassa pia leo amekutana na wafugaji na wakulima walio wajumbe wa bunge la katiba kwa mfumo huo huo.

Hoja zao wanapokutana na makundi hayo ni kupiga chapuo kura ya wazi na kupinga ya siri,huku wakieleza namna CCM inavyopinga baadhi ya mapendekezo muhimu yaliyomo katika rasimu ya katiba.

Mh.Mtatiro ameongeza kuwa,wanachofanya mawaziri hawa ndicho kinachofanywa na mawaziri wengine wa CCM,ni agizo la lazima ambalo hivi sasa linatumika hapa Dodoma.

Leo,CCM na mawaziri wanatumia fedha na kutoa rushwa ili kupitisha matakwa yao.Masuala haya yana ushahidi,kesho nitayasema bungeni kwa uwazi kabisa.

MY TAKE:
Hizi ni tuhuma nzito sana!

Kumbe ndio maana mizigo ilibakizwa ili kutumwa ktk kazi kama hizi! Ktk bahasha wanawekewa ngapi? Wajumbe wapiga dili watafaidi sana mpaka kikao kinamalizika.
 
Back
Top Bottom