CCM wanapotamka neno "wananchi" wanamaanisha "wanaCCM".Sisi wengine tulie tu! kwa hiyo wakisema Serikali Tatu sio maoni ya "wananchi", mjue kuwa hao wananchi ni wale wa kwao tu.CCM imeshatugawa watanzania.wanatumia "divide and rule" principles katika hili. Hebu ifike mahali, tujitafakari kwa kina, tuangalie tulipotoka, tulipo sasa, na tunapotaka kwenda, na kisha tufanye uamuzi wa dhati kabisa toka mioyoni mwetu, ni TAIFA la namna gani tunalihitaji. Sababu tunayo, Uwezo Mwenyezi Mungu katujalia Tunao, na NIA hiyo pia Tunayo, tumpige adui vita, huyu adui UBAGUZI,RUSHWA, UMASIKINI,DHULUMA, MABAVU, na ULEVI WA MADARAKA!