Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Aliyekuwa Katibu wa Sekretarieti ya CHADEMA, Julius Mwita, amewapongeza Tundu Lissu na John Heche kwa ujasiri wao, akisema ni viongozi wanaoweza kuleta hamasa kubwa wakati wa uchaguzi. Akizungumza kupitia Clouds FM, Mwita amesema wawili hao ni kama simba, na kwamba wakiamua kuhamasisha wananchi kulinda kura zao dhidi ya wizi wa uchaguzi, wanaweza kusababisha mabadiliko makubwa.
"Hawa jamaa wawili Mwenyekiti na Makamu ni watu majasiri sana. Ni watu ambao wakizungumza katikati ya 'temperature' ya uchaguzi kwenye ile 'momentum' ya uchaguzi kwamba tutakufa wote kama wataibiwa kura...
"Tundu Lissu na John Heche ni Simba na wakiaamua katikati ya uchaguzi wakahamasisha wanachama, wananchi na wapiga kura kwamba hii ngoma hawa jamaa wakifanya chochote cha kuiba kura na kuondoa thamani ya mpiga kura tunakula nao...
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
"Hiyo ni katikati ya kampeni za uchaguzi. Ni ule wakati ambao mna mgombea wa Urais, ubunge, udiwani wanasema hawana ilani ya uchaguzi na ilani ni thamani ya kura ya Mtanzania. Ndio inapaswa kuwa ilani ya CHADEMA wakati wa uchaguzi"