Juma Jux amtambulisha mkewe Prisca kwa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete

Juma Jux amtambulisha mkewe Prisca kwa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Msanii wa R&B Juma Jux hatimaye amepata nafasi ya kumtambulisha rasmi mke wake, Prisca ama priscy, kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, pamoja na mke wake Mama Salma Kikwete.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Jux ameweka video hii na kuandika;

"Hatimaye nimepata nafasi na baraka kubwa za kumtambulisha rasmi mke wangu kipenzi Priscy kwa Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na mke wake mpendwa Mama Salma Kikwete."

"Pia nilipata nafasi ya kumfikishia rasmi mualiko wa tafrija zetu kubwa zijazo za #JP2025. Ambapo tunatarajia kuwa na sherehe maalum mwezi April huko Nigeria, na tamati itakuwa hapa nyumbani Tanzania mwezi May."

"Ilikuwa ni furaha na baraka kubwa kupokelewa nyumbani kwao na kupata nafasi ya kipekee kushiriki nao kumbukumbu hii muhimu kwenye safari yetu mpya ya ndoa."

Mimi pamoja na mke wangu Priscy tunatoa shukrani za dhati kwa Mzee wetu Mhe. Dkt. Kikwete na Mama Salma kwa mapokezi yao ya upendo."

IMG_3604.jpeg

Mbona hatujaona picha ya Jux akienda kumtambulisha huyo mpenzi wake Kwa Wazee wake, ama walipoteza maisha wote??

By the way, tuwatakie Kila la heri kwenye maisha yao mapya ya Ndoa.
 
Mambo gani tena mkuu😂
Kikwete alituwakilisha mpaka kimataifa tukammiliki Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, mwanamama mmoja hivii, mpaka habari ikataka kuleta diplomatic scandal, ila uzuri Museveni mtu wetu tunammiliki tangu zamani akaimaliza kijirani tu 😂😂😂

Leo unampelekea mke wako?

Labda vijana wanaona kazeeka mpaka kafika John's Hopkins kutibiwa atakuwa karudisha mpira kwa Mama Salma siku hizi.
 
Hahaha............lakini si unajua Wanaume hatuzeeki hadi siku tunafukiwa.

Itakuwa Jux hajui hayo 😅
 
Jux atajutia huu uamuzi siku akikuta sms za mzee wetu kwenye simu ya mkewe
Huyu mzee namkubali sana hazeeki umri wala tabia na anajua kucheza na naneno
 
Back
Top Bottom