SPYMATE
JF-Expert Member
- Apr 17, 2013
- 2,382
- 2,407
Wameoana Boma au kimila ?Msanii wa R&B Juma Jux hatimaye amepata nafasi ya kumtambulisha rasmi mke wake, Prisca ama priscy, kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, pamoja na mke wake Mama Salma Kikwete.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Jux ameweka video hii na kuandika;
"Hatimaye nimepata nafasi na baraka kubwa za kumtambulisha rasmi mke wangu kipenzi Priscy kwa Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na mke wake mpendwa Mama Salma Kikwete."
"Pia nilipata nafasi ya kumfikishia rasmi mualiko wa tafrija zetu kubwa zijazo za #JP2025. Ambapo tunatarajia kuwa na sherehe maalum mwezi April huko Nigeria, na tamati itakuwa hapa nyumbani Tanzania mwezi May."
"Ilikuwa ni furaha na baraka kubwa kupokelewa nyumbani kwao na kupata nafasi ya kipekee kushiriki nao kumbukumbu hii muhimu kwenye safari yetu mpya ya ndoa."
Mimi pamoja na mke wangu Priscy tunatoa shukrani za dhati kwa Mzee wetu Mhe. Dkt. Kikwete na Mama Salma kwa mapokezi yao ya upendo."
View attachment 3276779
View attachment 3276778
Maana naona Dini Tofauti