Profesa Juma Athuman Kapuya amejitokeza na kuwakemea wote wanaomchafua kwa kumhusisha na Taaisi ya Athuman Kapuya ambayo ilifungiwa na serikali kwa kuhusika na kashfa ya ushoga.
Kapuya amesema kwamba yeye jina lake ni Juma Athuman Kapuya, huku baba yake akiitwa Athuman Kapuya. Mama yake alipofariki dunia, baba yake mzazi alioa mwanamke mwingine na wakapata watoto. Kati ya hao watoto yupo Yasin Athuman Kapuya ambaye katika kumuenzi Baba yake mzazi akaamua kuanzisha Athuman Kapuya Foundation.
Profesa Kapuya kasema si yeye, mke wake au watoto wake wanaojihusisha na foundation hiyo. Anadai siku taasisi hiyo inafunguliwa alishiriki kuifungua na aliitwa aje kueleza Mzee Athuman Kapuya alikuwa mtu wa namna gani.
Profesa Kapuya amedai kuwa ana miaka zaidi ya 20 hajaonana na ndugu yake huyo mhusika wa taasisi hiyo kwani Yasini Kapuya anaishi Marekani.
Ameongeza kuwa watu wanaweza kwenda Serikalini kufuatilia hasa nani mmiliki wa hiyo Taasisi ili waache kuchafua jina lake kwa jambo lisilomhusu.
Pia soma