Juma Nature:Singeli ni muziki wa kihuni.

Sidhani Kama Utakufa!Tujifunze Kukubali Vipaji Vilivyo Ndani ya Wengine!Mathalani,Mie Nampenda Shollo Mwamba na Kazi Zake!Kama Haitoshi Bila Mziki Huu,Kuna Watu Wangetupiga Roba Mtaani!
 
Muziki wa ovyo kuwahi kutokea Tanzania
 
Hakuna shaka katika hili..
Hata wanaoimba na kuupenda pia ni wahuni..
 
Ule uhuni kuanzia kucheza na maneno yake 'hainaga ushemeji,tunakulaga zamu ya nani Leo!' Huwezi sikiliza au kutazama na mama mkwe.
 
Binafsi sio shabiki wa Singeli wala huyo Juma nature,lkn kwangu naiona fursa ktk aina hiyo ya muziki,kama vijana wanaweza kupata fedha kupitia mziki huo sio vibaya kuuendeleza na kuuombea mazuri,maana hata Mimi nilikuwa naona muziki ya nature kama ya wavuta bangi lkn haikuzuia Juma nature kupata sapoti kwa watu wengi
 
Ule uhuni kuanzia kucheza na maneno yake 'hainaga ushemeji,tunakulaga zamu ya nani Leo!' Huwezi sikiliza au kutazama na mama mkwe.
mkuu kama umekuwa zama zetu nyimbo nyingi za hiphop ulikuwa uwezi sikiliza na wazee ila wat happened leo ?
 
Wengi wamepotezwa.
 
Msaga sumu minanda huko

Waasisi wa singeli Dogo niga simela mtoto wa kigogo,halafu akina sholo

Msaga kwa vigodoro sawa ni mkongwe lkn singeli no.
kwa hiyo umeamua kubishana na Msaga Sumu kuwa yeye sio muhasisi wa Singeli?!

Wasanii wa Singeli wenyewe hawajambishia kuwa jamaa ndio baba yao
 
Msaga sumu anaimba mchiriku/ mnanda, au tuseme kina Man fongo wanaimba "modernized songeli", msaga sumu ANAIMBA, "harap" kama kina sholo mwamba, man fongo etc!
kwa hiyo umeamua kubishana na Msaga Sumu?
 
sasa yeye mziki wake ndo wa kistaarabu? hili jamaa kumbe lina roho ya mkunjo eeh? aache wivu zama zake zimekwishapita..
 
Ukiangalia waimba singeli wote wana option mbili tu. 'Kukaba' au 'singeli'. Sasa tuchague wenyewe............tukabwe au tuimbiwe singeli!!!
 
Hata bongofleva zamani tulikuwa tunaona ni uhuni, dada video vixen akionekana kwenye nyimbo alikuwa anaonekana hajatulia. Miaka ya 90 na mwanzoni mwa mwaka 2000 ukisikia mtu anarap hiphop alijulikana ni muhuni, wasanii wengi walikuwa wanavuta bangi kabla hawajapanda stejini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…