Yohana Kilimba
JF-Expert Member
- Dec 25, 2012
- 8,105
- 5,629
Sidhani Kama Utakufa!Tujifunze Kukubali Vipaji Vilivyo Ndani ya Wengine!Mathalani,Mie Nampenda Shollo Mwamba na Kazi Zake!Kama Haitoshi Bila Mziki Huu,Kuna Watu Wangetupiga Roba Mtaani!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hawa wanaosema SINGELI itakufa ni wale walioanza kuisikia E fm...singeli inamashabiki wake special. haiwezi kufa. zile kelele ndiyo raha yenyewe
Wekaaaaa Mwamba wekaaaa!"Zamu yako inakuja kesho baharia wangu usikonde"
Nature simuamini. Hata MKUBWA aliwahi kumuita muhuni.Hakuna mziki usiokuwa na uhuni,ila aseme tu wamezidiana uhuni
Binafsi sio shabiki wa Singeli wala huyo Juma nature,lkn kwangu naiona fursa ktk aina hiyo ya muziki,kama vijana wanaweza kupata fedha kupitia mziki huo sio vibaya kuuendeleza na kuuombea mazuri,maana hata Mimi nilikuwa naona muziki ya nature kama ya wavuta bangi lkn haikuzuia Juma nature kupata sapoti kwa watu wengi![]()
Licha ya Singeli kuwa muziki ulioibuka kwa kasi na kujizolea mashabiki lukuki na kufanikiwa kuzalisha vipaji kadhaa mwanamuziki Mkongwe Juma Kasim Nature ameibuka na kusema muziki huo ni wa kihuni na hautadumu.
Akiongea katika studio zake za Halisi Records mapema wiki hii na mwandishi wa habari hizi, Juma Nature amedai kuwa Singeli ni muziki ambao hautoishi kuwa muziki wa kudumu kwa muda mrefu bali unapita tu kwasababu ni muziki wa kihuni.
Akaongeza pia kuwa mahabiki hawapendi mambo ya kipumbavu ambayo yanaletwa na baadhi ya wahuni wanaovamia muziki.
“Singeli itapita tu kwasababu ya uhuni,” alisema.
“Unajua raia wengi wa Bongo hawapendi mambo ya kipumbavu pumbavu na mashabiki wetu wengi sana sio wahuni ila wahuni wanakuja katika hizi section, so wakija kwenye section hapo muziki hakuna tena,” alisema Nature.
Source: Bongo5
Ni kama huu wa Manfongo:
mkuu kama umekuwa zama zetu nyimbo nyingi za hiphop ulikuwa uwezi sikiliza na wazee ila wat happened leo ?Ule uhuni kuanzia kucheza na maneno yake 'hainaga ushemeji,tunakulaga zamu ya nani Leo!' Huwezi sikiliza au kutazama na mama mkwe.
Wengi wamepotezwa.Watanzania ndivyo tulivyo
Aliwahi kupotea mtu muhimu sana kwenye game...Lucas Mkenda 'Mr.Nice' eti kwa sababu tu watu hawakupenda 'kuku kapanda baiskel'
Ooh hakuna sense hakuna sense...utajiuliza...kwani lazima kila msanii aimbe sense???
Watu hao hao walikata viuno kwenye 'abaaba aba abaaba prakata atumba'
Tumelaaniwa sisi
kwa hiyo umeamua kubishana na Msaga Sumu kuwa yeye sio muhasisi wa Singeli?!Msaga sumu minanda huko
Waasisi wa singeli Dogo niga simela mtoto wa kigogo,halafu akina sholo
Msaga kwa vigodoro sawa ni mkongwe lkn singeli no.
kwa hiyo umeamua kubishana na Msaga Sumu?Msaga sumu anaimba mchiriku/ mnanda, au tuseme kina Man fongo wanaimba "modernized songeli", msaga sumu ANAIMBA, "harap" kama kina sholo mwamba, man fongo etc!
sasa yeye mziki wake ndo wa kistaarabu? hili jamaa kumbe lina roho ya mkunjo eeh? aache wivu zama zake zimekwishapita..![]()