Juma Nature:Singeli ni muziki wa kihuni.

Juma Nature:Singeli ni muziki wa kihuni.

UOTE="mtoto wa maskini, post: 18253083, member: 153722"]Singeli kwanza sio mziki ni makelele tu ya wahuni asante juma nature[/QUOTE]
Well said...
 
Nhie wkoote hamnazo,kilasiku mnalalamika vijana wajikomboe kimaisha na hasa kuwa wabunifu sasa wamekuja na hiyo singeli mnawaponda mnataka waje kula kwenu???toeni ushamba hapa
 
Wanaweza wakauboresha na kuutoa kwenye huo muonekano was kihuni na kuufanya ukubalike na wengi.
Wasikatishwe tamaa ila waongeze ubunifu.

Hata nywele zilizopo kwenye mazingira tata katika mwili huwa zinaendelea kuota.Mugabe
 
Halafu uimbaji wa singeli hata sio kazi, yaani wote wanapita kwenye njia 1 hata mi naweza
 
Kila singeli utasikia: eeh baba eeeh baba eeeeeeh baba!
Mziki wa hovyo kabisa huu, naupa miezi miwili iliyobaki sidhani kama utafika mwaka mpya huu mziki, kila singeli beats zile zile isipokuwa lyrics tu, na lyrics zenyewe eeeh baba eeeh baba, mara shemeji na uhuni mtupu! Upuuzi kabisa!
By the way, msaga sumu haimbi singeli ndo maana ataendelea kuwapo.
Kama tunavosikia

Yooo
Wasap
Yu no wat amu sei
Yo no wat ai mini

Kwenye hiphop...kila mtu na fleva yake...waachwe watu na singeli yao waweke mguu moja chini

Umesahau
'Baharia wangu'
 
Wanaweza wakauboresha na kuutoa kwenye huo muonekano was kihuni na kuufanya ukubalike na wengi.
Wasikatishwe tamaa ila waongeze ubunifu.

Hata nywele zilizopo kwenye mazingira tata katika mwili huwa zinaendelea kuota.Mugabe
Watanzania ndivyo tulivyo

Aliwahi kupotea mtu muhimu sana kwenye game...Lucas Mkenda 'Mr.Nice' eti kwa sababu tu watu hawakupenda 'kuku kapanda baiskel'

Ooh hakuna sense hakuna sense...utajiuliza...kwani lazima kila msanii aimbe sense???

Watu hao hao walikata viuno kwenye 'abaaba aba abaaba prakata atumba'

Tumelaaniwa sisi
 
Mwaka juzi nami nilifikiri hivyo lakini kwa sasa hapana. Huu mziki upo na una nguvu sana
 
Watanzania ndivyo tulivyo

Aliwahi kupotea mtu muhimu sana kwenye game...Lucas Mkenda 'Mr.Nice' eti kwa sababu tu watu hawakupenda 'kuku kapanda baiskel'

Ooh hakuna sense hakuna sense...utajiuliza...kwani lazima kila msanii aimbe sense???

Watu hao hao walikata viuno kwenye 'abaaba aba abaaba prakata atumba'

Tumelaaniwa sisi
Kweli kuwakatisha tamaa sio vyema.
 
x13549629_1051489578275396_561623312_n.jpg.pagespeed.ic.rXibwinwLc.jpg

Licha ya Singeli kuwa muziki ulioibuka kwa kasi na kujizolea mashabiki lukuki na kufanikiwa kuzalisha vipaji kadhaa mwanamuziki Mkongwe Juma Kasim Nature ameibuka na kusema muziki huo ni wa kihuni na hautadumu.

Akiongea katika studio zake za Halisi Records mapema wiki hii na mwandishi wa habari hizi, Juma Nature amedai kuwa Singeli ni muziki ambao hautoishi kuwa muziki wa kudumu kwa muda mrefu bali unapita tu kwasababu ni muziki wa kihuni.

Akaongeza pia kuwa mahabiki hawapendi mambo ya kipumbavu ambayo yanaletwa na baadhi ya wahuni wanaovamia muziki.

“Singeli itapita tu kwasababu ya uhuni,” alisema.

“Unajua raia wengi wa Bongo hawapendi mambo ya kipumbavu pumbavu na mashabiki wetu wengi sana sio wahuni ila wahuni wanakuja katika hizi section, so wakija kwenye section hapo muziki hakuna tena,” alisema Nature.

Source: Bongo5

Binafi siupendi na nikisikia unapigwa redioni huwa naswit oof radio.
 
Mzee Kirobotoooh, nakumbuka hata wao walivyoanza mziki wao wa rap, wengi waliuona ni mziki wa wahuni. Binafsi niliona kama ni watu wanaojihangaisha na kupoteza muda. Kipindi kile mziki wa dansi ulikuwa juu. Nakumbuka Juma Nature alipotoa singo zake zilianza kubamba taratibu. Na mziki wa Mtoto wa Geti kali uliotungwa na Inspekta Haroon ulitingisha sana, mdogomdogo Bongo Fleva ikaanza kuupiku Mziki wa Dansi na matokeo yake hivi sasa Bongo Fleva sio uhuni imekuwa ajira na kazi halali.
Ila huu mziki wa singeli ni vigumu kuuelewa. Ni mziki usio na mpangilio wa ala na sauti. Kelele nyingi na ni vigumu kuelewa mantiki iliyo katika nyimo za singeli. Namsapoti sana Kirobotoh, singeli haina muda itapotea kama ulivyopotea Mziki wa Beni na Chakacha.
 
Back
Top Bottom