Juma Nature:Singeli ni muziki wa kihuni.

Juma Nature:Singeli ni muziki wa kihuni.

Kwa kuwa we ni mzaramo, ngoja nikubali, msaga sumu anaimba singeli, ila singeli yake ni tofauti na ya kina man fongo., hapo je!!
Hata Ney wa Mitego Anafanya hip Hop ila Hip Hop yake ipo tofauti na hip hop ya kina Songa,Nikki Mbishi na Fid Q.

Asante kwa kukubaliana na Msaga Sumu kuwa ndio Muhasisi wa Singeli.
 
Kila singeli utasikia: eeh baba eeeh baba eeeeeeh baba!
Mziki wa hovyo kabisa huu, naupa miezi miwili iliyobaki sidhani kama utafika mwaka mpya huu mziki, kila singeli beats zile zile isipokuwa lyrics tu, na lyrics zenyewe eeeh baba eeeh baba, mara shemeji na uhuni mtupu! Upuuzi kabisa!
By the way, msaga sumu haimbi singeli ndo maana ataendelea kuwapo.
Au niambie baharia wangu..
 
Singeli ni muziki wa muda tu kama ilivokuja trap or clanky music,,,ni fasion ya muda kama ilivyokuwa viatu vya supra tu
 
Kipindi anatoa wimbo wa kigheto gheto muziki wa bongo flava ulikuwa considered kama muziki wa kihuni pia
 
Watanzania ndivyo tulivyo

Aliwahi kupotea mtu muhimu sana kwenye game...Lucas Mkenda 'Mr.Nice' eti kwa sababu tu watu hawakupenda 'kuku kapanda baiskel'

Ooh hakuna sense hakuna sense...utajiuliza...kwani lazima kila msanii aimbe sense???

Watu hao hao walikata viuno kwenye 'abaaba aba abaaba prakata atumba'

Tumelaaniwa sisi
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] gudo[emoji23][emoji23][emoji23]
 
singeli ina watu wake..
imeanza muda sana ,sema maredioni wameiskia mwaka huu..
ila kwa wale wapenda shuguli ,vigodoro kitaambo!!!
kama huu mziki una watu wake basi hautaisha..
sisi wapenda rusha roho tuliupinga weeh kipindi unaanza kwenye shuguli..
ila skuizi tyshauzoea bila kisingeli shuguli hakuna.

masela huku kwetu bananaaa[emoji446][emoji23][emoji23][emoji23]
ukicheza singeli hata kama una shida ni zaidi ya pombe na alosto
unasahau zote
maana unarusha sana, na ni moja wapo ya zoezi
 
Ule uhuni kuanzia kucheza na maneno yake 'hainaga ushemeji,tunakulaga zamu ya nani Leo!' Huwezi sikiliza au kutazama na mama mkwe.
siku hizi hakuna nyimbo za kutazama na familia..
ukikaa kideoni familia itoe maana hizo bongo fleva ndo chupi zimejaa mnooo..
na kushikana shikana ni upuuzi tupu jamani
 
....Nature si wa kuongea maneno hayo kabisa!
..angalau angeshauri namna ya kuboresha;vinginevyo alichoongea ni nonsense!
 
Wanatumia nguvu kubwa ikubalike ukweli ni kuwa haina maisha marefu
 
We msic gani hadi uchezeshe kalio kwaz zam mara la kushoto,mara la kulia...
 
Sidhani Kama Utakufa!Tujifunze Kukubali Vipaji Vilivyo Ndani ya Wengine!Mathalani,Mie Nampenda Shollo Mwamba na Kazi Zake!Kama Haitoshi Bila Mziki Huu,Kuna Watu Wangetupiga Roba Mtaani!
je wajua hicho wanachokiimba ni hatari, aibu, uchafu na sumu zaidi ya kupigwa kabari mtaani
 
Yeye anauona ni muziki wa kihuni lakini vijana wenzie wameiona fursa wameanza kuitumia na wanapiga mpunga manfongo toka fiesta imeanza mbaka inaisha atakuwa kaingiza si chini ya milioni 20 sio pesa ndogo na akizidi kujitahidi ataingiza pesa nyingi zaidi wakati huo Nature amekaa kijiweni anawaponda!

-Nyerere-
 
Kifupi ni kwamba waimba singeli wameshindwa jua asili ya singeli,imetoka wap?na kwann inaitwa singeli...ukisoma fasihi simulizi,mashairi ni moja ya tanzu za fasihi simulizi,mashairi yamegawanyika mara mbili kuna mashairi ya zamani(yenye vina) na mashairi ya kisasa(yasio na vina), kwanini singeli?kwasababu ktk mashairi ya zaman wanatumia vina...so kati ya tungo na mwisho wa tungo kuna kitu kinaitwa NGELI..mf..katoka baba mmoja,toka safari ya mbali.kavimba yake mapaja na kutetemeka mwili...hizo ja na li ndio ngeli(vina) but kwenye mashair ya kisasa hakuna hvyo ngeli ndio maana wanaita singeli yana unazungumzi lolote lile ili bila kufuata vina ili mradi ilete maana..huko ndipo asili ya singeli..ndio maana unaona kama wanapiga kelele tu bit kwa wanaojua tunajua wanafanya nini,all in all kila muziki una hadhira yake(walengwa) ww unaweza ona upuuzi kwa wenzio ikawa tiba,pia naunga na ww hii ni fursa lazima itumiwe so watu msiubeze kila muziki una pakuanzia pakufia hatujui hata hyo mnaiita bongo flavour si ilianza hatujui itakufa lini.
 
Umenifungua Macho!
Asante kwa Hii Adhimu Historia ya Singeli!
 
mi sina tatzo nao huo mziki, ila tu nachukia kuona wanauleta mpka huku kwa wanyakyusa sasa watafanya nin na makalele hyo hata kukata viuno hawajui yn, kwa kifup cjawah kuona huku kwetu mtu akiushobokea huo mziki! therefore;
Naomba hizo kelele ziwe zinaishia hukohuko kwenu,
Ovyo kabisa nyie..! aaaarrgghh
 
Back
Top Bottom